Serikali ya Mseto ndo dawa ya "HAMAHAMA" ya Wanasiasa

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,791
3,360
Wanasiasa baadhi wamekuwa wakihama kutoka chama kimoja kwenda kingine. Hili limejitokeza sana siku za karibuni. Baadhi tayari wameshapewa nyadhifa kubwa tuu serikalini .Moja ya sababu kubwa kwa waliohama hivi karibuni ni " Kuunga mkono juhudi za Rais wetu". Nikimsikiliza wanayesema wanamuunga mkono anasema" maendeleo hayana chama"! Maswali ya kujiuliza ni haya, 1. Je, hawa wahamaji, hawamwelewi Raisi wetu?
2. Kama suala ni kumuunga mkono Rais wetu, je atakapoondoka madarakani watarudi kwenye vyama vyao?
3. Je, nini kifanyike ili mwanasiasa yeyote na kutoka chama chochote aweze kushirikiana moja kwa moja na dola katika kujenga nchi?
Kwa maoni yangu, ni vyema tukawa na katiba inayoruhusu Mtanzania yeyote bila kujali chama anachotoka,awe na nafasi sawa ya kulitumikia Taifa. Tuna mifano ya nchi mbalimbali hapa Afrika na nje zenye katiba inayoruhusu serikali ya vyama vingi na zimepiga hatua kubwa ya maendeleo.
Kwa katiba yetu kuwa vile, kungepunguza gharama kubwa ya mathalani chaguzi za marudio. Pia ingetoa fursa ya wanasiasa wazalendo na mahiri walioko vyama vingine kushiriki uongozi sehemu za kiserikali ili kutoa mchango kwa Taifa letu.
 
jiwe ndo chanzo cha mvurugo...ukiondoa jiwe ndo suluhu ya kila kitu
 
Back
Top Bottom