Serikali ya mseto kati ya CHADEMA na CCM ndiyo tiba ya TANZANIA inayougua

Jumakidogo

R I P
Jul 16, 2009
1,851
417
Ni jambo unaloweza kulitizama kwa mashaka na wepesi. Lakini kutokana na upepo wa kisiasa ulivyo hili si jambo la kushangaza kwani linaweza kutokea. Harakati za CDM zinaweza kufikia hatua ya kuundwa kwa serikali ya mseto katika chaguzi za usoni zijazo.

Bora hili litokee mapema ili kuleta chachu ya kuchochea maendeleo ya nchi hii. Naamini wale wanachama wa CDM wanaweza kuliona jambo hili kama upuuzi.

Hata kwa upande wa wale wa CCM wanaweza kuchukulia kuwa ni jambo gumu kwao. Lakini linaweza kutokea kutokana na nguvu na misigino ya kisiasa. Bora serikali ya mseto itokee kwanza kuliko CCM kuendelea kubaki madarakani milele.

CCM yenye watendaji wachache waadilifu inaweza kuwa na changamoto motomoto iwapo itaongezewa nguvu na watendaji kutoka CDM katika mseto. Hii inaweza kuwa tiba, au nusu tiba kwa Tanzania inayougua.
 
Naona Magamba Wamekutuma Kutafuta Suluhu Ya Hatima Yenu!! Ila katika Hali ya Kawaida Huwezi Kuishi Na nyoka katika Tundu Moja!! Lazima Mmojawapo Atoke!! Sasa Kama ni Magamba wamekutuma Kuomba suluhu ili waweze kuendelea Kufilisi nchi hii kawambie Nafasi Hiyo Milango imefungwa!!
 
Wewe nawe hujaachaga tu kutumia firigisi kufikiri? Unadhani hii ni R. Odinga or Tsvangirai?

Hapa lazma nyie magamba muachie ngazi, mtoke nasis tujue tuna anzia wapi kuwasweka rumande mkachukue mvua zenu,haiwezekani mtu fool all the time, keko mtaenda otherwise mtaani tunawapofoa mawe, wezi wakubwa,vibaka ninyi.
 
Tukubali au tukatae ukweli ndiyo huu, ikumbukwe tanzania siyo ya CCM wala CDM, ni ya watanzania wenyewe. Hivi vyama vya kisiasa tumevituma vikatuwakilishe tu Bungeni, Ndani ya bunge hukaa wabunge wa vyama vyote, wanajadiri pamoja mambo mbalimbali yahusuyo maendeleo ya tz na wanafikia mwafaka, iweje leo tuseme serikali ya mseto mshangae? kwa hapo ni kufikiri kidogo.
 
Hi ikitokea naona Tz kutakua hamana upinzani tena
maana hamna altenative yoyote
 
kwanza hiyo serikali mseto itoke wapi.mimi sina chama lakini hakuna chama cha upinzani kinachoweza kuingia kwenye mseto huku bara,chama ambacho kilianza kuonyesha njia kimejaa ubinafsi,ukabila,kufukuza wanachama na element za ukanisa...hii haiwezekani hata kidogo...vyama vijijenge viwe vya kitaifa ndio tutaviamini kuvipa mamlaka...kumbuka kushika dola sio sawa na kumpa mtu uenyekiti wa kamati ya maandalizi ya harusi au kipaimara.
 
mbona povu linakutoka kiasi hicho hebu nithibitishie hayo madai yako, inamaana hicho chama huwa wanafanya na ibada za kikanisa!?
 
Siku CDM ikiingia mseto na CCM namrudishia Slaa kadi ya Uanachama, maana CDM siyo Mama wala Baba yangu!
 
Chadema should agree with the idea of coalition government or else face the prospect of remaining as the opposition party indefinitely. With the ongoing process of constitution composition being held hostage by the governing CCM in order to dictate the process for the sake of entrenching their presence in power, CHADEMA should rule out any possibility of winning any one of the coming elections.

They have indeed no option but to inhume their own interests by coming to terms with CCM and set up a unity government for the good of the whole country.
 
Naona Magamba Wamekutuma Kutafuta Suluhu Ya Hatima Yenu!! Ila katika Hali ya Kawaida Huwezi Kuishi Na nyoka katika Tundu Moja!! Lazima Mmojawapo Atoke!! Sasa Kama ni Magamba wamekutuma Kuomba suluhu ili waweze kuendelea Kufilisi nchi hii kawambie Nafasi Hiyo Milango imefungwa!!

Nadhani fikra kwamba kila mwenye mtizamo tofauti na sisi ametumwa na magamba ni fikra mufilisi na tuziache.Tujadili hoja jamani!
 
Jumakidogo,
Naona umeamua kuunganisha kila kitu,
Umeanza na muungano wa Lowassa na Sitta, hapa unaleta CCM na CDM,
Ok, nasubiri thread nyingine, nahisi itakuwa kuungana kwa Dr. Kikwete na Dr. Slaa
 
Jumakidogo,
Naona umeamua kuunganisha kila kitu,
Umeanza na muungano wa Lowassa na Sitta, hapa unaleta CCM na CDM,
Ok, nasubiri thread nyingine, nahisi itakuwa kuungana kwa Dr. Kikwete na Dr. Slaa

kwenye bold unapomtaja Dr. Salaa acha kumwita JK dr because hazifanani bwana!
NA KUHUSU KUUNGANA MIMI MWENYEWE SIAFIKI, WOOTE WATAKUWA MAGAMBA TUU!
 
Hoja hupingwa na hoja. Kuna tofauti kubwa kati ya hoja za viongozi wa CDM na wafuasi wao. Inawezekana chama kikawa na viongozi makini kwa kujenga hoja lakini nyuma yao kukawa na kundi kubwa la watu wanaotumia milima nyama iliyo chini ya migongo yao kufikiri badala ya kichwa. Serikali mseto hulazimishwa na mazingira ya kisiasa kama ilivyotokea Kenya na Zimbabwe. Hayo yanaweza kutokea hapa pia. Mnadhani ikiwa hivyo wanachadema mtafanya nini? Achane kupiga picha hatua 2 mbele badala yake tumieni darubini kuona kilichopo kilomita nyingi mbele.
 
Jumakidogo,
Naona umeamua kuunganisha kila kitu,
Umeanza na muungano wa Lowassa na Sitta, hapa unaleta CCM na CDM,
Ok, nasubiri thread nyingine, nahisi itakuwa kuungana kwa Dr. Kikwete na Dr. Slaa

Unajua wengi hasa wanachadema wanasoma thread kwa kukurupuka. Sikusema waungane, wale sijashauri waungane. Nilisema kutokana na upepo wa kisiasa ulivyo hilo linaweza kutokea. Tumeona Kenya na Zimbabwe.
 
Mbona zanzibar wana serikali ya mseto kwani kuna nini walilobadilisha, usitake kuniaminisha kuwa serikali za mseto ndo suruhusho la matatizo yetu
 
Back
Top Bottom