Serikali ya mseto huenda ikajadiliwa na kikao maalum | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya mseto huenda ikajadiliwa na kikao maalum

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Jun 6, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame.  Marekebisho ya Katiba ya Zanzibar yatakayoruhusu kuundwa kwa serikali ya Umoja wa Kitaifa yatalazimika kujadiliwa na kikao maalum cha dharura kutokana na Baraza la Wawakilishi kumaliza muda wake kabla ya kufanyika kura ya maoni, Julai 31 mwaka huu.
  Hayo yalielezwa jana na Katibu wa Baraza la Wawakilishi, Ibrahim Mzee Ibrahim, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kikao cha bajeti kwa mwaka fedha 2010/11 mjini Zanzibar.
  Alisema iwapo wananchi wa Zanzibar wataamua iwepo Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar, kikao cha dharura kitalazimika kuitishwa kwa kwa sababu Baraza linatakiwa kuvunjwa Julai 16 wakati kura ya maoni itafanyika Julai 31 mwaka huu
  “Kama wananchi walio wengi wataunga mkono kuwepo kwa mabadiliko ya muundo wa Serikali, itabidi kuitishwa kikao cha dharura cha marekebisho ya katiba,” alisema katibu huyo.
  Alisema Baraza la Wawakilishi baada ya kuvunjwa wajumbe wote watalazimika kurudi katika majimbo yao kujitayarisha na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu
  Tayari Tume ya Uchaguzi Zanzibara imeanza kutoa mafunzo kwa wadau wa uchaguzi kuhusu kura ya maoni itakayoamua kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa ama la.
  Hata hivyo, wazo la kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa kitaifa Zanzibar linaonekana kuwagawa viongozi wa Serikali na CCM Zanzibar kwa madai kwamba suala hilo linakwenda kinyume na sera ya CCM na misingi ya Mapinduzi ya mwaka 1964
  Kuhusu bajeti kuu ya Serikali ya mwaka wa Fedha 2010/1011 Katibu wa Baraza hilo alisema inatarajiwa kuwasilishwa na Waziri wa Nchi Afisi ya Rais (Fedha na Uchumi), Dk. Mwinyihaji Makame Juni 9 mwaka huu.  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...