comrade igwe
JF-Expert Member
- Jan 12, 2015
- 7,295
- 3,945
Serikali ya mkoa wa Mtwara imekiri kuwapo kwa upungufu mkubwa wa nafaka ya mahindi hasa katika wilaya ya Masasi na Nanyumbu hali ambayo imesababisha kuuzwa kwa bei kubwa, na hivyo kuchangia bei ya unga kupanda kutoka shilingi elfu moja mpaka shilingi elfu moja na mia tano.
Wakizungumza na ITV iliyotembelea wafanyabiashara wa unga na mahindi wamesema mahindi yanayoingia mkoani humo yakitokea mkoani Ruvuma ni machache na hata yakipatikana gunia moja la mahindi linauzwa kwa bei ya shilingi laki moja hali inayochangia kwa sasa mitaji yao kuyumba.
Akizungumzia hilo kaimu katibu tawala uchumi na uzalishaji wa mkoa wa Mtwara Amani Lusake amekiri kuwapo kwa upungufu wa nafaka ya mahindi huku na kusisitiza kuwa kila mwaka miezi kama hii hali hii imekuwa ikijitokeza, na hivyo kulazimu wizara ya kilimo uvuvi na umwagiliaji kutoa tani 2400 ili kupunguza makali ya bei.
Hata hivyo amesema katika msimu uliyopita mkoa wa Mtwara ulifanikiwa kuzalisha ziada ya nafaka tani laki nane 69 elfu na 486 huku sehemu kubwa ikiwa ni zao la muhogo na mahindi hulimwa kwa sehemu ndogo sana.
Chanzo: ITV