Serikali ya Mh JK inaonekana kushindwa kila mahali na katika sekta zote.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Mh JK inaonekana kushindwa kila mahali na katika sekta zote....

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Emma Lukosi, Aug 2, 2012.

 1. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #1
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hali ya nchi imekuwa tete,kila idara ya utumishi wa umma imeingia kwenye mgomo,kinacho lalamikiwa ni madai ya msingi ya haki za watumishi,alkini serikali inayachukulia madai haya kama kero na kelele za mpangaji hazimzui mwenye nyumba kukosa usingizi.Tumeona mgomo wa madaktari na sasa mgomo wa waalimu.

  Imekuwa ni kawaida sasa kwa serikali yetu sikivu kushindwa kutumia usikivu wake kukaa meza moja na watumishi wake ili kupata suluhisho la madai yao.Suluhisho limekuwa ni mahakama huku serikali ikitumika kutoa kauli ambazo mwisho wa siku mhimili wa mahakama uhitimisha kwa hukumu iliyo kwisha kutamkwa na serikali. Nini hatari yake,hatari yake ni mgongano wa madaraka na kuingilia uhuru wa mahakama.

  Sisi sote ni mashahidi,tumeona serikali sikivu mara zote ikishindwa na kukimbilia mahakamani wakati huo huo kesi haijatajwa wao hukimbilia kwenye media na kutangaza migomo hiyo ni batili.Kuna haja gani basi ya kukimbilia mahakamani ikiwa tayari imeshatekeleza hukumu itakayo tolewa na mahakama? Hali kama hii athari yake kubwa ni uvunjivu wa amani tuliyo jivunia kwa miongo zaidi ya mitano.Ifike wakati kila mhimili mmoja uheshimu mhimili mwingine ili kulinda mgongano wa kimadaraka unao fanywa na serikali yetu sikivu.

  Serikali hiyo hiyo sikivu kupitia kiongozi wa mhimili wa bunge imekuwa ikitumia rungu lake ipasavyo kuhakikisha hoja zote zinazo husiana na migogoro ya watumishi na serikali haijadiliwi bungeni kwa kigezo cha hoja hiyo iko mahakamani ilihali serikali ikitoa hukumu nje ya mahakama.Naomba wakuu wa JF tuliangalie hili kwa umakini ili kunusuru uchafuzi huu wa hali ya hewa kwa mgongano wa madarakaw unao fanywa makusudi na serikali yetu sikivu kwa mustakabali wa amnai ya nchi yetu.

  Naomba kuwakilisha.

   
 2. L

  LIWALONALIWE Member

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 29, 2012
  Messages: 69
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Mbona unashindwa kumalizia umeshatoka kupata ndovu mbilitatu unavyoonyesha.Niambia lipi kubwa kati ya hayo lilishawahi kutekelezwa kikamilifu katika vipindi vyote vya maraisi hapa TZ.
  Jk jembee wewe.
  Mwacheni ****** watu amalize muda wake na kwahabari yenu anamwaga lami kila barabara ya mkoa hapa tz.mnataka awafanyie nini.
  Tatizo la wa tz hata ukiwamwagia asali hawatosheki
   
 3. a

  andrews JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
 4. k

  kibugumo JF-Expert Member

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Jun 19, 2011
  Messages: 1,347
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Ahadi zake nyingi hazitekelezeki.
   
 5. Emma Lukosi

  Emma Lukosi Verified User

  #5
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 22, 2009
  Messages: 932
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Tunataka Chuo kikuu kila mkoa
  Tunataka elimu sawa kwa wote
  Tunataka mafisi (mafisadi) wote waondolewewe
  Tunataka madini yetu
  Tunataka kulipwa kwa madaktari
  Tunataka kulipwa kwa walimu
  Nataka urith wangu wa EAC.
  Tunataka Chuo kikuu kila mkoa
  Tunataka elimu sawa kwa wote
  Tunataka mafisi (mafisadi) wote waondolewewe
  Tunataka madini yetu
  Tunataka kulipwa kwa madaktari
  Tunataka kulipwa kwa walimu
  [FONT=&quot]Nataka urith wangu wa EAC.[/FONT]
   
 6. STALLEY

  STALLEY JF-Expert Member

  #6
  Aug 2, 2012
  Joined: May 5, 2012
  Messages: 530
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Naomba kufahamu nini vipaumbele vyetu maana kila sekta watu wanalalamika
   
 7. P

  Prince Hope JF-Expert Member

  #7
  Aug 2, 2012
  Joined: Jul 21, 2012
  Messages: 2,167
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Hapooooooooooooooooooo kwenye red. Chukua jembe kalime hiyo lami tuone kama utavuna mpunga ili kupunguza bei ya mchele!
   
 8. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #8
  Aug 2, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  WanaJF, nimefuatilia kwa makini migomo yote miwili ya madaktari na waalimu, nimejiridhisha kuwa wamefuata taratibu zote lakni kesi zao zilipofika mahakamani serikali imeshinda. Nimekumbuka na maneno ya mheshimiwa Lisu kuwa majaji wanateuliwa watu wasio na sifa. Na tunajua kibinadamu ukiteuliwa wakati huna sifa lazima utaufyata mkia tu na kumtumikia aliyekuteua. Ninamalizia kwa kusema kuwa as long as JK ni rais wa nchi hii watu mnaodhani mahakama itawasaidia sahauni mpaka may be after 2015. JK ni mbabe sana japo anaonekana kuchekacheka. Ni JK huyu huyu aliymtaiti jaji Mkuu mstaafu Ramadhani hadi akakubali kuivua mahakama haki yake ya msingi ya kutafsiri sheria kwenye ile issue ya mgombea binafsi. Gone are Mkapas day wakati serikali ilikuwa inabwagwa mara kibao mahakamani. Mnaonaje?
   
 9. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #9
  Aug 2, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Uanachama CCM ni hatua muhimu ya awali katika ujenzi wa tabia chafu kimaadili.
  Ubunge CCM ni hatua ya pili inayotoa fursa katika kukomaza tabia chafu kimaadili.
  Uwaziri ni tuzo kwa kufuzu katika fani ya kujenga na kutetea tabia chafu kimaadili.
  Uraisi ni kulinda na kusimamia, kwa kutumia vyombo vya dola, tabia chafu kimaadili.


  Watanzania, chini ya CCM, tumeliwa!
   
 10. Mpitagwa

  Mpitagwa JF-Expert Member

  #10
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 10, 2012
  Messages: 2,296
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Kabisaa tunatakiwa kupata mbadala, mahakama inajifanya waalimu wameshindwa na walipe fidia, watalipa fidia na itaonekana balabala kwenye matokeo ya shule za serikali yanayokuja.
   
 11. Ernesto Che

  Ernesto Che JF-Expert Member

  #11
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,117
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Muulize vizuri aliahidi nini atakwambia hajui,
  muulize kanini Tz maskini atakwambia hajui,
  Muulize Znz ni nchi au si nchi atakwambia hajui,
  Muulize aliyemteka Dr Ulimboka ni nani, na serikali imefanmya nini atakwambia hajui,
  Muulize anaenda safari za nje kufanya nini atakwambia hajui,
  Muulize anafanya kazi gani akiwa ofisini atakwambia hajui
  ....
  ...
  N.k.

  Huyu ni JK zaidi ya umjuavyo!
   
 12. Msalagambwe

  Msalagambwe JF-Expert Member

  #12
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 11, 2012
  Messages: 716
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Mwandishi;Kwa nini nchi yako Tanzania pamoja na utajiri wote wa watu,ardhi, maji mengi, madini na mbuga za wanyama lakini bado ni masikini?

  Kikwete; Angazi! Hata mimi najiuliza hivyohivyo sielewe kwa nini watu wa nchi yangu ni malofa, labda ndugu mwandishi nisaidie jibu.
   
 13. Chaimaharage

  Chaimaharage JF-Expert Member

  #13
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 211
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Na bado, 2015 ni mbali wanatamani ifike. Walidhani walipo kuwa wanachakachua kura ili kwenda Ikulu ni kula bata tu! Watashika adabu yao. Mwisho wa siku chuichui nao watagoma..nadhani ndio utakuwa mwisho wa ******..sijui atakuwa mkimbizi wapi..
   
 14. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #14
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Serikali ya JK imeshindwa hata kulinda MIPAKA ya nchi yetu.

  Refer the recent claims by Malawians that the WHOLE LAKE NYASA belongs to Malawi and they will continue with oil and gas exploration with impunity.
   
Loading...