Serikali ya Marekani hatarini kuishiwa fedha Mwezi Oktoba

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen ametahadharisha kwamba serikali ya Marekani inaweza kuishiwa fedha mwezi ujao na amelitaka bunge la nchi hiyo liongeze uwezo wa serikali wa kukopa. Waziri Yellen ametoa tahadahri hiyo katika barua aliyomwandikia spika wa bunge Nancy Pelosi.

Katika barua hiyo waziri huyo amesema ikiwa bunge halitaongeza kima cha mikopo, serikali ya Marekani itaishiwa fedha mwezi ujao wa Oktoba na kwamba kwa mara ya kwanza katika historia yake Marekani haitakuwa na uwezo wa kutimiza dhima zake za kifedha.

Deni la serikali ya Marekani liliongezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa janga la COVID-19 baada ya serikali hiyo kupitisha mipango mitatu ya matumizi makubwa ili kupunguza athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga hilo.
 
Mbona ilishawahi kutokea kipindi kile cha Trump mpaka wakafunga shughuli za serikali kwa muda hivi, maana hawakuwa na fedha za hata kulipa mishahara ya wafanya kazi.
Nafikiri umechanganya, Trump alifunga shughuli za kiserikali ili kulishinikiza bunge likubaliane na mpango wake wa kuidhinisha fedha kwa ajili ya kujenga ukuta mpakani mwake na Mexico ili kuzuia wahamiaji haramu.
 
Kuishiwa fedha kwa selikal ya marekani ni jambo la kusikitsha kidgo,je wakiongezewa kiwango cha mkopo watatimiza mipango yao kwan hata uchumi wa nchi hauko sawa.
 
Nafikiri umechanganya, Trump alifunga shughuli za kiserikali ili kulishinikiza bunge likubaliane na mpango wake wa kuidhinisha fedha kwa ajili ya kujenga ukuta mpakani mwake na Mexico ili kuzuia wahamiaji haramu.
Ni kweli. Asante kwa kunirekebisha. Lakini nakumbuka issue hii ilijitokeza labda wakati wa Obama
 
Obama pia ilikua siyo sababu ya kuishiwa hela, bali ni katika kutokubaliana hivyo na yeye aliwaambia wasipopitisha atakayo basi atafunga shughuli za serikali kitu kilichopelekea hata bunge kukosa pesa na wafanyakazi kubaki majumbani
 
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen ametahadharisha kwamba serikali ya Marekani inaweza kuishiwa fedha mwezi ujao na amelitaka bunge la nchi hiyo liongeze uwezo wa serikali wa kukopa. Waziri Yellen ametoa tahadahri hiyo katika barua aliyomwandikia spika wa bunge Nancy Pelosi.

Katika barua hiyo waziri huyo amesema ikiwa bunge halitaongeza kima cha mikopo, serikali ya Marekani itaishiwa fedha mwezi ujao wa Oktoba na kwamba kwa mara ya kwanza katika historia yake Marekani haitakuwa na uwezo wa kutimiza dhima zake za kifedha.

Deni la serikali ya Marekani liliongezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa janga la COVID-19 baada ya serikali hiyo kupitisha mipango mitatu ya matumizi makubwa ili kupunguza athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga hilo.
Bujibuji nipo, nitawapigieni fedha za kutosha, bila ya riba Wala masharti yoyote
 
Kwani hapa kwetu pako salama, nasikia uchumi unakua kwa chini ya asilimia mbili lakini kama kawaida serikali inaficha ukweli huo.
 
Obama pia ilikua siyo sababu ya kuishiwa hela, bali ni katika kutokubaliana hivyo na yeye aliwaambia wasipopitisha atakayo basi atafunga shughuli za serikali kitu kilichopelekea hata bunge kukosa pesa na wafanyakazi kubaki majumbani
Ilikua mpango wa ObamaCare ndio walikua hawataki kuupitisha bungeni
 
Waziri wa fedha wa Marekani Janet Yellen ametahadharisha kwamba serikali ya Marekani inaweza kuishiwa fedha mwezi ujao na amelitaka bunge la nchi hiyo liongeze uwezo wa serikali wa kukopa. Waziri Yellen ametoa tahadahri hiyo katika barua aliyomwandikia spika wa bunge Nancy Pelosi.

Katika barua hiyo waziri huyo amesema ikiwa bunge halitaongeza kima cha mikopo, serikali ya Marekani itaishiwa fedha mwezi ujao wa Oktoba na kwamba kwa mara ya kwanza katika historia yake Marekani haitakuwa na uwezo wa kutimiza dhima zake za kifedha.

Deni la serikali ya Marekani liliongezeka kwa kiwango kikubwa wakati wa janga la COVID-19 baada ya serikali hiyo kupitisha mipango mitatu ya matumizi makubwa ili kupunguza athari za kiuchumi zilizosababishwa na janga hilo.

USA kuna Federal Reserve System, wengi hamjui hii system, hii ndio Financial System to come in action in case of any US Financial Crisis na haitatokea Fedha iishe katika Serikali ya U.S.A

US sio wenzetu jamani, wako dunia nyingine.

Nadhani ni kile kitu wana ita deadlock kwenye senate ikitokea bajeti imeshindwa kupitishwa, ina tokea mara nyingi rep na dems wasipo kubaliana kupitisha vifungu flani kwenye budget ila kuishiwa hela haita kaa itokee. Watu wana gold reserve mara tatu ya iliyo duniani
 
Back
Top Bottom