norbit
JF-Expert Member
- Jul 30, 2007
- 835
- 699
Imetoa hapo kwenye red TANZANIA
Wakati akitoa ufafanuzi kuhusu tishio la Marekani kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Tanzania, kutokana na nchi hiyo kuruhusu Iran kupeperusha bendera yake kwenye manowali zake za mafuta, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania, Membe, ananukuliwa kuelezea kwamba serikali ya mapinduzi Zanzibar inao mkataba na kampuni moja ya Dubei unaoipa kampuni hiyo madaraka ya kuingia kwenye mkataba na nchi mbali mbali duniani kwa lengo la kuruhusu nchi hizo kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye meli zao bila shaka kwa malipo. Swali langu ni je hayo madaraka ya kutumia bendera ya Tanzania kibihashara serikali ya mapinduzi Zanzibar imeyapata wapi?