Serikali ya mapinduzi Zanzibar inatoa wapi madaraka ya kuridhia matumizi ya bendera ya Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya mapinduzi Zanzibar inatoa wapi madaraka ya kuridhia matumizi ya bendera ya Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Jul 7, 2012.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wakati akitoa ufafanuzi kuhusu tishio la Marekani kuiwekea vikwazo vya kiuchumi Tanzania, kutokana na nchi hiyo kuruhusu Iran kupeperusha bendera yake kwenye manowali zake za mafuta, waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa wa Tanzania, Membe, ananukuliwa kuelezea kwamba serikali ya mapinduzi Zanzibar inao mkataba na kampuni moja ya Dubei unaoipa kampuni hiyo madaraka ya kuingia kwenye mkataba na nchi mbali mbali duniani kwa lengo la kuruhusu nchi hizo kupeperusha bendera ya Tanzania kwenye meli zao bila shaka kwa malipo. Swali langu ni je hayo madaraka ya kutumia bendera ya Tanzania kibihashara serikali ya mapinduzi Zanzibar imeyapata wapi?
   
 2. O

  Ongeauchoke Senior Member

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Hawa wana matatizo sana waulize wameingiza kiasi gani hakuna ajuaye.unaweza ukaambiwa wamepewa mazulia
   
 3. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Au tende tani 5 kwa ajili ya maandalizi ya mwezi mtukufu.
   
 4. k

  kicha JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 506
  Likes Received: 532
  Trophy Points: 180
  nahisi malipo yatakua kama yale ya asili mia moja ya dhahabu.
   
 5. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #5
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  na wewe kama nani unae tuhoji hakuna kaka katika muungano sote sawa, tuna haki ya kutumia raslimali za muungano tunavyotaka hampeni rudisheni Tanganyika yetu, hakuna aliyewatuma muingize yenu yote katika muungano ilikuwa hiari yenu, msitohuji tunachofanya mabadiliko ya 10 sisi ni nchi kamili, na hatuna sababu ya kuwaambia tumepata kiasi gani nyinyi huwa mnatuambia mkinunua rada mbovu? it is our business haiwahusu watanganyika.

  tatizo lenu mnashindwa kutofautisha hapa hakuna suala la mambo ye nje ni uchumi, ni vikwazo vilivyopo ni vya USA na EU sio vya UN ndio maan China inaendelea kununua mafuta Iran, lakini la msingi meli sio za Iran nenda kaangalie hansard za baraza la wawakilisi waziri ametoa tamko, umeyapata wapi mamlaka ya kuhoji Zanzibar wanachofanya tanganyika iliojificha kwenye mgongo wa muungano?
   
 6. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #6
  Jul 7, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,595
  Likes Received: 4,709
  Trophy Points: 280
  Wametumia udhaifu wa Rais wa JMT.
   
 7. S

  Simbaarobaini7 Member

  #7
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani hasa ndugu zangu wa Tanganyika tudai Tanganyika yetu irudi tu mambo yote hayo yataisha. Hawa akina Membe na wengine tuliowapa madaraka wanaibembeleza sana zanzibar na nasikia wote hao wana vimada kwenye balozi zetu nje amabvyo wamevitoa kutoka huko visiwani. Some years back I was London in the UK na ilipofika 2006 ukienda pale ubalozini kuna wasichana wengi na kila ukiuliza huyu kaja lini unaambiwa huyo ni wa JK au huyo ni wa fulani kati ya hao rafiki zake. I'm telling a true storry na niliwafahamu kwa majina kabisaa. I even new where JK alipokuwa anafikia na hao vimada wanamfuata. Tuwaache Zanzibar na nchi yao tuvunje huu Muungano usio na Tija bali wa wanasiasa pekke wanaoufaidi ndio maana wanautetea kwa nguvu zote. I tell you tutaishi kwa amani zaidi kuliko kuwanga'ang'ania Wanzanzibari kwanza wao hawatutaki!
   
 8. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #8
  Jul 7, 2012
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,124
  Trophy Points: 280
  Zanzibar si dola (Soveirgn state) ila kwa miaka mingi imekuwa ikipenyeza jambo moja moja kuelekea kuwa dola.
   
 9. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #9
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  JK anajua yote haya?, mamlaka wamejipa wenyewe, Liwalo na liwe!
   
 10. Ndoa

  Ndoa JF-Expert Member

  #10
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 2, 2011
  Messages: 985
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Huu muungano kila siku utakuwa jinamizi linalowasumbua wanaoung'ang'ania.
   
 11. S

  Simbaarobaini7 Member

  #11
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tanga kwetu wewe unaishi wapi tena? Juzi mwanasheria Mkuu amesema Zanzibar ni nchi kule bungeni Dodoma mbele ya Waziri Mkuu Pinda aliyewahi kusema Zanzibar si nchi. Huyo Pinda alikaa kimya kukubaliana na maneno ya Attorney General. Kwani wewe hukusikia habari hizo mbona unaturudisha nyuma tena? Vunja Muungano Tanganyika yetu ije bana!
   
 12. a

  alfazulu JF-Expert Member

  #12
  Jul 7, 2012
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 735
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Swali gumu sana kwa mtanzania wa kawaida kulijibu, lingekuwa rahisi iwapo HATI YA MUUNGANO
  wetu inge kuwa wazi.
   
 13. F

  Falconer JF-Expert Member

  #13
  Jul 7, 2012
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 658
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  Hhahahah, Hakika munafurahisha baraza kwelikweli. Munajuwa kinachoendelea?. Au bado mumelala tu?. Wazanzibari wamo kuchangia katiba mpya ya muungano. Munasikia wanavotamka huko?. Hawataki muungano. Wanataka UHURU wao. eeehhhh, wanataka UHURU wao. Basi Muungano.
   
 14. I

  IWILL JF-Expert Member

  #14
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Wamarekani wamuweke kikwete kuwa anasuport terrorist, tuone kama atapiga picha na 50cents
   
 15. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #15
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  JK mtu swafi hana majungu, mpenda haki, na mpenda muungano ndio maana akateuwa wajumbe sawa wa tume ya katiba kwa kujua hili, wewe ndio katika mafisadi wa muungano lakini sasa tunautengeneza uwe wa mkataba, na JK yupo na haondoki mpaka mwisho, na yeye ndio atatwambia who next kama ulidhani Mbowe mtu hajenda hata shule sahau tangu uhuru maraisi wote wana degree mbowe haiwezekani mpelekeni chuo kikuu huria kwanza akasome.
   
 16. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #16
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Jamani muangalieni huyu kwani kupiga picha na 50 cents ndio big deal, Kiwkete ana picha na Bill Gates na haikuwa kitu kuliko huyo 5 cents mlemavu wa akili. inaonekana maradhi ya OCD Obsessive–compulsive disorder yanakunyemelea wewe? usiwe mvivu wa kufikiri na kupima lipi bora
   
 17. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #17
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Wafahamishe hao watanganyika wenzako wenye akili mgando na uvivu wa kufikiri, wanashindwa kujua nini cha Muungani nini sicho they have to read between the lines
   
 18. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #18
  Jul 7, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Acha kutoa povu! Lakini mbona Marekani imemuandikia barua rais Kikwete na siyo Sheni wenu?
   
 19. I

  IWILL JF-Expert Member

  #19
  Jul 7, 2012
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  huyo rais wako ni kivuli kama nyerere alivyokuwa anaweka miaka yake ya ndiyo au hapana...hopeless. futika na hiyo OCD yako.
   
 20. Mtumbatu

  Mtumbatu JF-Expert Member

  #20
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 327
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 45
  Hiyo barua umeiona wewe? au domo tu jumba maneno, nikidhani alimuandikia barua Obama kumbe mmarekani yahudi? hata hata hadhi ya kumuandikia Kikwete kama si kum-beg tu, hakumuandikia Rais wetu kwa sababu kwa sababu anajua majibu atakayopata sio anayotaka na pia hatayapata kwa kikwete pia, huyu mmarekani na tundu lisu hawana tofauti domo jumba maneno tu
   
Loading...