Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia shirika lake la biashara la ZSTC imeanza kuwalipa fidia wanananchi ambazo wakati wa uchumaji wa karafuu walipata ajali ya kuanguka na kuumia wakati wa uchumaji wa karafuu akiwemo mmoja aliyefariki katika zoezi hilo.
Zoezi hilo la kuwalipa wananchi hao lilifanyika afisi kuu ya ZSTC hapa zanzibar ambapo mwenyekiti wa bodi ya shirika hilo la Taifa la biashara Maalim Kassim Seleman alikabidhi fedha milioni 11.5 kwa waathirika hao na kusisitiza kuwa serikali imetenga fedha maalum ambazo zinatokana na mauzo ya karafuu kufidia malipo inapotokezea ajali na zoezi hilo awali lilisitishwa lakini sasa serikali imelirejesha tena.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo amezitaka familia kuacha mara moja mtindo wa kuwatumia watoto wadogo katika zoezi la uchumaji wa karafuu kwakuwa ndiyo waathirika wakubwa na kusisitiza sheria hairuhusu watoto wadogo kufanya kazi.
Naye mmoja ya mwananchi ambaye familia yake imeathirika katika zoezi hilo Mwadini Ally mbali ya kuishukuru serikali kwa msaada huo ambao hawakuutarajia amekiri kuwa wamefanya makosa kuwatumia watoto wadogo kuchuma karafuu.
Katika zoezi hilo wananchi hao saba akiwemo mmoja aliyepokea kwa niaba ya marehemu aliyefariki walipokea fedha taslimu huku familia ya marehemu ikipokea shilingi milioni tano,shirika hilo la biashara latoa ofa kwa sasa hunuua karafuu kilo moja shilingi 14,000.
Chanzo: ITV