Wadau naanza kuogopa hili jipu la serikali ya awamu ya tano!
Jamaa wana chini ya miezi mitatu lkn sioni plans zao!
Kila asubuhi ni kufukuzana na amri!
Natoa mifano!
1. Mh Kigwangala alipoingia akaanza kumtafuta Dr. Mwaka na waziri wake akapambana na watu wa tradition medicine.
Kuna faida na hasara ya kufanya hivyo, alternative medicine kuangaliwa na watu pale modern medicine inapokuwa haina msaada kwa jamii! Dr. Mwaka anaweza kufungiwa Ilala Boma lkn watu kama hawana imani na Amana au Muhimbili bado watamtafuta mwaka au mwingine yeyote anayefanya kazi kama hizo!
Hoja na kigwangala na waziri wake ilipaswa ni kufanya utafiti japo mdogo kujua kwanini Mwaka ni popular kuliko maprof pale Muhimbili, KCMC au hospitali nyingine!
2. Bomoabomoa za mabondeni na maeneo mengine
Jamaa wameanza kwa kasi, wamevunja vibanda vya watu bila huruma!
Hawakutazama wananchi wangapi walipatiwa stahiki zao na kuhamishwa huko mabondeni! Less than 15% walilipwa, wizara ilipaswa kujua hatma ya 85% ya wananchi wanaotakiwa kuhamishwa, serikali kazi yake ni kusafe guard interest za watu wake na sio kuwa terrorise watu wake! After all wao pia wana la kujibu ktk sakata hili! Now wamesitisha ile justification ya watu kufa imepotelea wapi? Nani atalipa fidia endapo wakienda mahakamani na kushinda? Kwanini maamuzi ya kukurupuka yailetee serikali hasara kiasi hiki?
3. Ada elekezi, ujenzi holela wa shule na kufungia vyuo vikuu visivyo na sifa
Elimu bure ni failure, ada za shule za umma wala haziwasumbui watu vichwa, tatizo ni ubora wa elimu ipatikanayo ktk hizo shule zetu! Manispaa ya kinondoni inahamasishana kufyatua shule 7 in few months ili zipokee wanafunzi wa form 1 mwaka 2016! Kwanini tunapenda kujengajenga vibanda elimu kila uchochoro? What is the use of having shule kila kata in Dar? Ina make sense ukiwa Manyara, Moro au Arusha na sehemu nyingine mikoani maana kata n kubwa na in btn unaweza kukuta mbuga za wanyama! Dar unaweza kuzunguka kata 20 kwa baiskeli in just 1 hour! Hebu tazama Tambaza, Azania, Jangwani etc ambazo zina zaidi ya miaka 70, zina ubora wa kimandhari sababu ya location zipo more academic, zinachukua wanafunzi wengi zaidi, zina maeneo kwa ajili ya recreational activities na kwa uwezo wake wa kuchukua wanafunzi wengi sehemu moja, pia zinaweza kutoa nafasi ya walimu wengi kuwa pamoja! Vibanda elimu (shule za kata) zinajengwa ktk masoko, au vichochoro vingine ambavyo haviko friendly na elimu kabisa hivyo kuongeza risk kwa watoto kuharibika! Leo wamekuja na hoja ya kufunga vyuo, what about wadogo zetu ambao wameshaanza au wanakaribia kumalizia elimu zao? Je vipi kuhusu wale waliohitimu ktk vyuo hivyo na leo wameshaanza ajiriwa? Busara ya mambo haya iko wapi?
4. Dramatic administration
Leo kila anayefanya kazi anakuja na camera!
Tcra wanamsomea mtu makosa yake wanaonesha kama mchezo wa kuigiza, ubaya wake ni kuwa serikali anapoteza credibility! Mtu anayefanya kazi na serikali lazima aheshimiwe kama business partner, na kwa kuwa serikali ndio mtoa huduma basi issue ya kuhandle client with respect haina mjadala!
Mazungumzo yanakuwa ndani, ukija kwa media unasummarize maazimo ya mkataba wenu au ufuatiliaji wenu! Sio sasa, na kwa bahati mbaya wanatoa amri na wanaolalamikiwa wanakuwa wabishi na kuonesha dharau juu ya maofisa wenyg mamlaka! Lile la waziri na mtu aliyevamia kiwanja huko tandika sijui, jamaa amebishia maagizo na anasema ana mkataba, wale wa 6 telecom nao wanaweza maamuzi tena huku serikali ikifanyiwa ukaidi ktk media!
Hiyo ni baadhi tu ya mifano!
Magufuli something is wrong with your govt, naomba mkae ile semina elekezi labda mnahitaji kuja na strategy ambayo ina maslahi mapana zaidi kwa umma!
Mnaweza kuwa ni wasimamiaji wazuri wa mali za umma, lakini hofu yangu ni kuwa si planners wazuri! Hamsikilizi ushauri na mnapenda sifa za kwenye media, please kaeni mjitafakari upya, huu si wakati wa campaign, ndio mnaongoza sasa!
Hadi sasa, hakuna wizara iliyotafiti eneo lake na kuja na results juu ya ustawishaji wa maisha ya wananchi au kuinua uchumi wa taifa! Wote ni amri tu, na majibu yanayotolewa kwa umma ni just opinions za jf na other social media, wekeni taskforce, mjipatie majibu kwa maswali mnayojiuliza sio kudandia mawazo yetu huku ktk media! Majibu siku zote tunayotoa ktk utafiti tu, iwe mini survey, sensa, etc...! Hakuna njia nyingine na hakuna msomi mwenye majibu, jamii inatoa majibu sahihi kuliko wasomi wote combined!
Kila la heri mh!