Serikali ya Magufuli inajiandalia anguko kama sio aibu siku zijazo

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,706
149,945
Dhana ya utumbua majibu inayoonekana kufanywa kwa nia njema na wakati mwingine kwa dhamira ya kisiasa zaidi bila kuchukua kwanza tahadhari ya kutosha,inaiweza kuja kuiweka serikali hii katika mtihani mgumu sana siku za usoni pale mambo yatakapoanza kuharibika na watu kuanza kukimbiana na wengine kugeukana.

Ziko sababu kadhaa zinazoweza kuja muifanya serikali iiumbuke ikiwa ni pamoja na kushindwa kesi pale itaposhitakiwa.

Makosa ya serikali yenyewe

Kuna baadhi ya shughuli za serikali katika Taasisi na Mashirika ya Umma zimefanywa chini ya kiwango au kutotekelezwa kabisa kutokana na serikali kupeleka fedha kidogo tena kwa mafungu mafungu na wakati mwingine kutopelekwa kabisa licha ya kuwa Taasisi husika ilitengewa bajeti. Hili linaweza kuja kujitokeza katika Taasisi kama Bodi ya Mikopo na nyinginezo ingawa ursasimu,uzembe na utendaji mbovu wa watumishi unaweza kuwa sehemu ya tatizo

Influence ya wanasiasa

Kuna sehemu watendaji wanawajibishwa lakini mwisho wa siku uchunguzi unaweza kuja kubainisha kuwa kulegalega au utendaji mbovu katika Mashirika / Taasisi hizi kumechangiwa na maamuzi ya wanasiasa kuingilia utendaji wa ma-CEO,manegement na hata Bodi zinazosimamia Mashirika haya na hivyo itafika wakati baadhi ya ma-CEO hawa watakuja kuonekana hawana hatia na kulazimika kurudishwa kazini au kupangiwa kazi nyingine.

Sheria za Utumishi wa Umma

Kuna watendaji leo hii wanaweza kusimamishwa kazi au kufukuzwa kazi lakini taratibu na sheria za utumishi zikifuatwa,huenda baadhi yao ikaja kuonekana kuwa waliadhibiwa kimakosa na Mahakama ya kazi inaweza kuagiza warudishwe kazini mara moja.Serikali inabidi na ilipaswa kutazama vizuri sheria hizi za utumishi wa umma na kuzirekebisha kwanza kabla ya kuendelea na fukuzafukuza hii au huku kusimamisha watu kazi kila kukicha.

Agenda za Kisiasa

Wakati unakuja siasa hazitakwepeka katika hili zoezi la utumbuaji majipu. Wanaotumbuliwa waliwekwa na wanasiasa na wanaowatumbua ni wana siasa ila nao wana ya kwao hivyo itafika hatu mmoja akimwaga ugali mwingine atamwaga mbogo kwani sidhani kama kuna msafi miongoni mwao na wataanza kutoleana siri.

Wanaotumbuliwa kuamua kutoa ya mayoni:
Kuna baadhi ya wanaotumbuliwa ambao mambo yao yanaweza kuja kuisha kiani iwapo wataamua kufunguka kiasi cha kutaja majina makubwa na pale itakapoonekana mambo yameisha kiujanjaujanja, ndio serikali itajikuta ikiinyooshewa kidole na pengine hata kusutwa.Hawa wanaotumbuliwa wanaweza hata kupenyeza siri kwa waandishi wa habari.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu

Kushinda kesi nyingi zitakazoibuka hapo baadae kufuatia maamuzi yanayofanywa sasa na serikali,itategemea na ufanisi na uwezo wa Ofisi hii kusimamia kesi ambazo serikali inaweza kushitakiwa.Kama watakuwa hawajajipanga vizuri kwa kuwa na wanasheria competent na wa kutosha huku serikali ikikabiliwa na kesi nyingi,kuna hatari ya serikali kuja kushindwa kesi nyingi zitakazifunguliwa na watumishi,watu binafsi ama makampuni.Katika kipindi hiki, Ofisi hii inatakiwa ipewe kipaumbele kuliko Taasisi nyingine yote ya umma.

Ukifukuza watumishi,ukinyang'anya watu mashamba,ukivunjia watu nyumba na ukanyang'anya watu leseni,ofisi pekee itakayobeba mzigo wa kesi zitakazofunguliwa ni hii ofisi ya AG labda kama kuna utaratibu wa serikali kuweza kukodi makampuni binafsi ya uwakili kuisadia kusimamia baadhi ya kesi zitakazofunguliwa.

Maamuzi ya bila umakini

Hivi sasa mawaziri wako busy kusimamisha watu kazi na sidhani kama wanachukua tahadhari ya kutosha kabla ya kufikia maamuzi haya.Mfano mzuri ni kusimamishwa yule mtumishi aliyekuwa kiongozi wa bomoaboma alafa baada ya siku chache ikitako taarifa kuwa amerejeshwa katika nafasi yake(kama sikosei Nipashe ndio iliripoti habari ya mtumishi huyu kurudishwa kazini).

Kusimamia nidhamu na uwajibikaji ndani ya serikali ni jambo jema na linalopaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo, lakini katika zama hizi za haki za binadamu na utwala wa sheria plus sheria zetu za utumishi wa umma, maamuzi haya ya leo yanaweza kuja kuwa "counterproductive " kwa serikali yenyewe yasipofanywa kwa umakini na kwa kutaka kujijenga kisiasa.

Katika kesi/mashauri kumi,serikali inatakiwa kushinda si chini ya saba au nane tofauti na hapo itakuja kuishi kubezwa kuwa ilikurupuka.
 
Dhana ya utumbua majibu inayoonekana kufanywa kwa nia njema na wakati mwingine kwa dhamira ya kisiasa zaidi bila kuchukua kwanza tahadhari ya kutosha,inaiweza kuja kuiweka serikali hii katika mtihani mgumu sana siku za usoni pale mambo yatakapoanza kuharibika na watu kuanza kukimbiana na wengine kugeukana.

Ziko sababu kadhaa zinazoweza kuja muifanya serikali iiumbuke ikiwa ni pamoja na kushindwa kesi pale itaposhitakiwa.

Makosa ya serikali yenyewe:

Kuna baadhi ya shughuli za serikali katika Taasisi na Mashirika ya Umma zimefanywa chini ya kiwango au kutotekelezwa kabisa kutokana na serikali kupeleka fedha kidogo tena kwa mafungu mafungu na wakati mwingine kutopelekwa kabisa licha ya kuwa Taasisi husika ilitengewa bajeti. Hili linaweza kuja kujitokeza katika Taasisi kama Bodi ya Mikopo na nyinginezo ingawa ursasimu,uzembe na utendaji mbovu wa watumishi unaweza kuwa sehemu ya tatizo

Influence ya wanasiasa:

Kuna sehemu watendaji wanawajibishwa lakini mwisho wa siku uchunguzi unaweza kuja kubainisha kuwa kulegalega au utendaji mbovu katika Mashirika / Taasisi hizi kumechangiwa na maamuzi ya wanasiasa kuingilia utendaji wa ma-CEO,manegement na hata Bodi zinazosimamia Mashirika haya na hivyo itafika wakati baadhi ya ma-CEO hawa watakuja kuonekana hawana hatia na kulazimika kurudishwa kazini au kupangiwa kazi nyingine.

Sheria za Utumishi wa Umma:

Kuna watendaji leo hii wanaweza kusimamishwa kazi au kufukuzwa kazi lakini taratibu na sheria za utumishi zikifuata,itaonekana waliadhibiwa kimakosa na Mahakama ya kazi inaweza kuagiza warudishwe kazini mara moja.Serikali inabidi na ilipaswa kutazama vizuri sheria za utumishi wa umma na kuzibadili kwanza kabla ya kuendelea na fukuzafukuza hii au huku kusimamisha watu kazi kila kukicha.

Agenda za Kisiasa:

Wakati unakuja siasa hazitakwepeka katika hili zoezi la utumbuaji majipu. Wanaotumbuliwa waliwekwa na wanasiasa na wanaowatumbua ni wana siasa ila nao wana ya kwao hivyo itafika hatu mmoja akimwaga ugali mwingine atamwaga mbogo kwani sidhani kama kuna msafi miongoni mwao na wataanza kutoleana siri.

Wanaotumbuliwa kuamua kutoa ya mayoni:

Kuna baadhi ya wanaotumbuliwa ambao mambo yao yanaweza kuja kuisha kiani iwapo wataamua kufunguka kiasi cha kutaja majina makubwa na pale itakapoonekana mambo yameisha kiujanjaujanja, ndio serikali itajikuta ikiinyooshewa kidole na pengine hata kusutwa.Hawa wanaotumbuliwa wanaweza hata kupenyeza siri kwa waandishi wa habari.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu:

Kushinda kesi nyingi zitakazoibuka hapo baadae kufuatia maamuzi yanayofanywa sasa na serikali,itategemea na ufanisi na uwezo wa Ofisi hii kusimamia kesi ambazo serikali inaweza kushitakiwa.Kama watakuwa hawajajipanga vizuri kwa kuwa na wanasheria competent na wa kutosha huku serikali ikikabiliwa na kesi nyingi,kuna hatari ya serikali kuja kushindwa kesi nyingi zitakazifunguliwa na watumishi,watu binafsi ama makampuni.Katika kipindi hiki, Ofisi hii inatakiwa ipewe kipaumbele kuliko Taasisi nyingine yote ya umma.

Ukifukuza watumishi,ukinyang'anya watu mashamba,ukivunjia watu nyumba na ukanyang'anya watu leseni,ofisi pekee itakayobeba mzigo wa kesi zitakazofunguliwa ni hii ofisi ya AG labda kama kuna utaratibu wa serikali kuweza kukodi makampuni binafsi ya uwakili kuisadia kusimamia baadhi ya kesi zitakazofunguliwa.

Maamuzi ya bila umakini:

Hivi sasa mawaziri wako busy kusimamisha watu kazi na sidhani kama wanachukua tahadhari ya kutosha kabla ya kufikia maamuzi haya.Mfano mzuri ni kusimamishwa yule mtumishi aliyekuwa kiongozi wa bomoaboma alafa baada ya siku chache ikitako taarifa kuwa amerejeshwa katika nafasi yake(kama sikosei Nipashe ndio iliripoti habari ya mtumishi huyu kurudishwa kazini?

Kusimamia nidhamu na uwajibikaji ndani ya serikali ni jambo jema na linalopaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo, lakini katika zama hizi za haki za binadamu na utwala wa sheria plus sheria zetu za utumishi wa umma, maamuzi haya ya leo yanaweza kuja kuwa "counterproductive " kwa serikali yenyewe yasipofanywa kwa umakini na kwa kutaka kujijenga kisiasa.

Katika kesi/mashauri kumi,serikali inatakiwa kushinda si chini ya saba au nane tofauti na hapo itakuja kuishi kubezwa kuwa ilikurupuka.
Woga ni dhambi ya mauti; usitufundishe woga unless wewe ni muhanga au mnufaika wa mkakati huu wa "Kutumbua majipu"?! We shall cross the bridge when we come to it, not b4! Kwa sasa hivi ni mwendo mdundo kwa KUTUMBUA MAJIPU tu mpaka kieleweke; mijitu milafi imeliumiza sana taifa hili, kumbuka: "There has never been a revolution without sacrifices; never". You name it; be it industrial, socio-political or economic!
 
Kwa akili ya harakaharaka na shauku ulionayo kama hao watumbuaji majibu hili unaweza usilione kwa sasa ila muda ndio utakakuja kukujibu vizuri.

Kwa mfano,niambie tu yule aliesimamisha kwa kusimamia zoezi la bomaboma karudi ofisini au yuko nyumbanni?
 
Who cares! Kuna watakaoumia na kuna watakaonufaika, at the end of the day TANZANIA itakuwa imeshinda na kujikwamua kutoka kwenye mikono ya mijizi; mifisadi, mijangili na mijitu michoyo. Kama ni kuwalipa fidia watalipwa kutokana na mapato yaliyookolewa kwa kuwatumbua hao hao majizi na kisha kuwaretrench for good wakaibe na kufisadi mihogo na mitama huko uswazi kwao. Period
 
Dhana ya utumbua majibu inayoonekana kufanywa kwa nia njema na wakati mwingine kwa dhamira ya kisiasa zaidi bila kuchukua kwanza tahadhari ya kutosha,inaiweza kuja kuiweka serikali hii katika mtihani mgumu sana siku za usoni pale mambo yatakapoanza kuharibika na watu kuanza kukimbiana na wengine kugeukana.

Ziko sababu kadhaa zinazoweza kuja muifanya serikali iiumbuke ikiwa ni pamoja na kushindwa kesi pale itaposhitakiwa.

Makosa ya serikali yenyewe:

Kuna baadhi ya shughuli za serikali katika Taasisi na Mashirika ya Umma zimefanywa chini ya kiwango au kutotekelezwa kabisa kutokana na serikali kupeleka fedha kidogo tena kwa mafungu mafungu na wakati mwingine kutopelekwa kabisa licha ya kuwa Taasisi husika ilitengewa bajeti. Hili linaweza kuja kujitokeza katika Taasisi kama Bodi ya Mikopo na nyinginezo ingawa ursasimu,uzembe na utendaji mbovu wa watumishi unaweza kuwa sehemu ya tatizo

Influence ya wanasiasa:

Kuna sehemu watendaji wanawajibishwa lakini mwisho wa siku uchunguzi unaweza kuja kubainisha kuwa kulegalega au utendaji mbovu katika Mashirika / Taasisi hizi kumechangiwa na maamuzi ya wanasiasa kuingilia utendaji wa ma-CEO,manegement na hata Bodi zinazosimamia Mashirika haya na hivyo itafika wakati baadhi ya ma-CEO hawa watakuja kuonekana hawana hatia na kulazimika kurudishwa kazini au kupangiwa kazi nyingine.

Sheria za Utumishi wa Umma:

Kuna watendaji leo hii wanaweza kusimamishwa kazi au kufukuzwa kazi lakini taratibu na sheria za utumishi zikifuatwa,huenda baadhi yao ikaja kuonekana kuwa waliadhibiwa kimakosa na Mahakama ya kazi inaweza kuagiza warudishwe kazini mara moja.Serikali inabidi na ilipaswa kutazama vizuri sheria hizi za utumishi wa umma na kuzirekebisha kwanza kabla ya kuendelea na fukuzafukuza hii au huku kusimamisha watu kazi kila kukicha.

Agenda za Kisiasa:

Wakati unakuja siasa hazitakwepeka katika hili zoezi la utumbuaji majipu. Wanaotumbuliwa waliwekwa na wanasiasa na wanaowatumbua ni wana siasa ila nao wana ya kwao hivyo itafika hatu mmoja akimwaga ugali mwingine atamwaga mbogo kwani sidhani kama kuna msafi miongoni mwao na wataanza kutoleana siri.

Wanaotumbuliwa kuamua kutoa ya mayoni:

Kuna baadhi ya wanaotumbuliwa ambao mambo yao yanaweza kuja kuisha kiani iwapo wataamua kufunguka kiasi cha kutaja majina makubwa na pale itakapoonekana mambo yameisha kiujanjaujanja, ndio serikali itajikuta ikiinyooshewa kidole na pengine hata kusutwa.Hawa wanaotumbuliwa wanaweza hata kupenyeza siri kwa waandishi wa habari.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu:

Kushinda kesi nyingi zitakazoibuka hapo baadae kufuatia maamuzi yanayofanywa sasa na serikali,itategemea na ufanisi na uwezo wa Ofisi hii kusimamia kesi ambazo serikali inaweza kushitakiwa.Kama watakuwa hawajajipanga vizuri kwa kuwa na wanasheria competent na wa kutosha huku serikali ikikabiliwa na kesi nyingi,kuna hatari ya serikali kuja kushindwa kesi nyingi zitakazifunguliwa na watumishi,watu binafsi ama makampuni.Katika kipindi hiki, Ofisi hii inatakiwa ipewe kipaumbele kuliko Taasisi nyingine yote ya umma.

Ukifukuza watumishi,ukinyang'anya watu mashamba,ukivunjia watu nyumba na ukanyang'anya watu leseni,ofisi pekee itakayobeba mzigo wa kesi zitakazofunguliwa ni hii ofisi ya AG labda kama kuna utaratibu wa serikali kuweza kukodi makampuni binafsi ya uwakili kuisadia kusimamia baadhi ya kesi zitakazofunguliwa.

Maamuzi ya bila umakini:

Hivi sasa mawaziri wako busy kusimamisha watu kazi na sidhani kama wanachukua tahadhari ya kutosha kabla ya kufikia maamuzi haya.Mfano mzuri ni kusimamishwa yule mtumishi aliyekuwa kiongozi wa bomoaboma alafa baada ya siku chache ikitako taarifa kuwa amerejeshwa katika nafasi yake(kama sikosei Nipashe ndio iliripoti habari ya mtumishi huyu kurudishwa kazini).

Kusimamia nidhamu na uwajibikaji ndani ya serikali ni jambo jema na linalopaswa kuungwa mkono na kila mpenda maendeleo, lakini katika zama hizi za haki za binadamu na utwala wa sheria plus sheria zetu za utumishi wa umma, maamuzi haya ya leo yanaweza kuja kuwa "counterproductive " kwa serikali yenyewe yasipofanywa kwa umakini na kwa kutaka kujijenga kisiasa.

Katika kesi/mashauri kumi,serikali inatakiwa kushinda si chini ya saba au nane tofauti na hapo itakuja kuishi kubezwa kuwa ilikurupuka.

Kwa hiyo ikianguka wewe ndiyo utafurahia?
 
Vita haina macho! Ukiingia vitani hakuna masuala ya kubembelezana tena. Wote tunalalamika kuwa Tanzania ni shamba la bibi, sasa Magufuli anataka kudhibiti hali hiyo wengine wanataka awabembeleze wahujumu uchumi? Heri waumie wachache kwa ajili ya wengine wengi tena walala hoi.
 
NDUGU ANGU SALARY SLIP UTACHOKA SANA KUANZISHA THREAD HAPA KILASIKU KUMPINGA RAIS MAGUFULI...

KADRI UNAVYOMUOMBEA MABAYA RAIS MAGUFULI NDIVYO ANAVYOZIDI KUONGEZA UMAARUFU KUTOKANA NA UTENDAJI KAZI WAKE MZURI...
 
Ungekuwepo wakati wa Nyerere anataka kujiuzulu ungeshangaa sana
nchi nzima imechooka
kwenda mbeya tu kutoka Dar wiki nzima
barabara mbovu
foleni ya vyakula
lakini watu wanambembeleza Nyerere asiondoke...

Magufuli jina lake la kwanza ni Pombe...ikishawakolea watu hata awachape bakora hatawakuelewa...
wait and see
 
Woga ni dhambi ya mauti; usitufundishe woga unless wewe ni muhanga au mnufaika wa mkakati huu wa "Kutumbua majipu"?! We shall cross the bridge when we come to it, not b4! Kwa sasa hivi ni mwendo mdundo kwa KUTUMBUA MAJIPU tu mpaka kieleweke; mijitu milafi imeliumiza sana taifa hili, kumbuka: "There has never been a revolution without sacrifices; never". You name it; be it industrial, socio-political or economic!
majipu yapi hayo? Mimi naona kukurupuka tu, majipu ni haya...escrow, epa, nyumba za serikali, epa....n.k. Na watuhumiw amewapa vyeo serikalini na wengine wenyeviti wa bunge. Mna macho lakini hamuoni. Ptuuuu!!
 
NDUGU ANGU SALARY SLIP UTACHOKA SANA KUANZISHA THREAD HAPA KILASIKU KUMPINGA RAIS MAGUFULI...

KADRI UNAVYOMUOMBEA MABAYA RAIS MAGUFULI NDIVYO ANAVYOZIDI KUONGEZA UMAARUFU KUTOKANA NA UTENDAJI KAZI WAKE MZURI...
Inawezekana sisi tunaokosoa/kushauri hivi tukawa na msaada mkubwa kwake kuilikoni nyinyi mnaodhani hawa viongozi wetu ni malaiko na ni makosa kuwakosoa.
.
Wakati wapinzani wanamkosao JK mliwatukana na kuwabeza sana mfano kuhusu safari zake za nje ya nchi lakini tuambieni leo hii nani alikuwa sahihi kati ya wapinzani na nyie wana-CCM?
 
Who cares! Kuna watakaoumia na kuna watakaonufaika, at the end of the day TANZANIA itakuwa imeshinda na kujikwamua kutoka kwenye mikono ya mijizi; mifisadi, mijangili na mijitu michoyo. Kama ni kuwalipa fidia watalipwa kutokana na mapato yaliyookolewa kwa kuwatumbua hao hao majizi na kisha kuwaretrench for good wakaibe na kufisadi mihogo na mitama huko uswazi kwao. Period
Thenki yu!

Ni bora mara bilioni kufanya maamuzi hata kama baadaye utaonekana umefanya kimakosa lakini siyo kukaa bila kufanya maamuzi eti unaogopa kufanya makosa.
 
Bavicha endeleeni kupiga ramli lakini sisi tuna songa mbele kabisa!

Uoga mlio nao juu ya mafisadi na kuogopa mahakama ndio umewafanya mmuogope na kumkumbatia Lowasa huko kwenu!

Waache waende mahakamani kama wanaona hivyo....
Wanao simamishwa kazi kupisha uchunguzi wanaendelea kulipwa mishara yao na ikithibitika hawana kosa watarejeshwa kazini!

Endeleeni kuogopa na kukumbatia mafisadi...
 
Rais ashasema kwenye vita hii kutatokea maumivu ila tuvumilie, kipi bora kumsimamisha mtu aliyetia hasara ya bilioni nyingi na anajiandaa kutia hasara zaid na kuja kumlipa milion 100 kama compasations? Rais ashasema kuna watu wanajaribu kuturudisha nyuma ila wataumbuka na tulipofikia lazima heshima ya kazi irudi, kuna watu mtaani walikuwa miungu, makazini ni zaid hata ya Rais kwa kujiona wao ndio kila kitu.
 
majipu yapi hayo? Mimi naona kukurupuka tu, majipu ni haya...escrow, epa, nyumba za serikali, epa....n.k. Na watuhumiw amewapa vyeo serikalini na wengine wenyeviti wa bunge. Mna macho lakini hamuoni. Ptuuuu!!

Asiyejua maana haambiwi maana; usiishi na kukwama jana, mla ni mla leo; mla jana kala nini?! wewe piga marktime wenzio tunachanja mbuga; mtindo ni kutumbua
majipu mpaka kieleweke; dont dwell too much on yesterday; take your lessons from yesterday to face the challenges of today and tommorow!
 
Back
Top Bottom