Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
Na Malisa Godlisten.
Umewahi kuona mchezo wa mazingaombwe? Ni mchezo unaotoa matumaini yasiyokuwepo. Ni mchezo wa kiini macho. Fundi wa mazingaombwe anaweza kuchukua makaratasi na kuyageuza kuwa pesa nyingi sana. Unajiuliza kama ana uwezo wa kugeuza karatasi kuwa fedha mbona tumelipa kiingilio kuja kumuona? Unagundua mazingaombwe si jambo halisi, hutoa matumaini lakini hewa.
Tangu serikali ya Rais Magufuli imeingia madarakani imetoa matumaini makubwa kwa watanzania, lakini matumaini haya hayaonekani kuakisi maisha halisi ya mtanzania. Je ni matumani hewa kama ilivyo mchezo wa mazingaombwe?
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 8.1 (b) inasema "lengo kuu la serikali litakua ni maendeleo na ustawi wa wananchi". Hii ina maana kwamba matokeo ya juhudi zote za serikali lazima yalete maendeleo na ustawi wa wananchi. Lakini je, mbona serikali ya Magufuli inatoa matumaini tu lakini hatuoni ustawi wa wananchi?
Hadi sasa serikali imeokoa fedha nyingi sana kutoka sekta mbalimbali. Imeokoa fedha za safari za njea kwa watumishi wake, imeokoa fedha za semina warsha na makongamano, imeokoa kodi kutoka kwa wafanyabiashara waliokwepa kinyemela.
Kuna kodi ya makontena bandarini, kuna kodi ya kampuni moja ya mafuta iliyokwepa Tsh. Bilioni 8 baada ya kugundulika kuwa ilifanya udanganyifu kuwa inasafirisha mafuta nje ya nchi kumbe inayauza hapahapa nchini.
Kwa ujumla kuna fedha nyingi sana zimeokolewa na serikali ya Rais Magufuli ambazo wananchi wanategemea zilete unafuu wa maisha kwao. Lakini badala yake maisha yanazidi kuwa magumu. Je serikali ya Magufuli inafanya mazingaombwe?
Watu wanajiuliza kwanini kunatokea mfumko wa bei katika bidhaa wakati serikali inajinadi kwamba imeweza kudhibiti uchumi vizuri? Kwa mfano kwanini bei ya sukari inapanda kila siku wakati serikali inajinadi kuokoa fedha nyingi? Kwanini serikali isitoe ruzuku kwa viwanda inavyozalisha sukari ili kupunguza gharama za uzalishaji na hatimaye bei kwa mwananchi ipungue?
Kama hiyo haitoshi kwanini fedha hizo zinazookolewa kila siku zisitumike kusaidia wanafunzi wa vyuo vya elimu ya juu kwa kuwapa mikopo?
Kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya vyuo vikuu nchini (TCU) zaidi ya wanafunz 65,000 walidahiliwa kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2015/16. Kati yao ni wanafunzi 40,836 waliofanikiwa kupata mkopo kati ya wanafunzi wote wenye sifa.
Hii ina maana kuwa takribani wanafunzi 20,000 walioko vyuo vya elimu ya juu mwaka wa kwanza hawana mikopo japo wana sifa ya kupata. Lakini wamekosa kwa sababu serikali haina fedha za kutosha kuwapa mikopo wanafunzi wote hao.
Lakini ni kweli serikali haina fedha? Kama ni kweli haya "mabilioni" yanayookolewa kila siku yanatumika kwa shughuli gani?
Katika moja ya kampeni zake wakati wa uchaguzi Rais Magufuli akiwa viwanja vya Mashujaa mjini Moshi alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa ikiwa atashinda hakuna mwanafunzi wa elimu ya juu atakayekosa mkopo.
Katika kufafanua hoja yake Rais Magufuli alihoji kwa kusema "pesa yenyewe ni mkopo, kwanini umnyime mtu wakati ni pesa atakayokuja kulipa? Bila mikopo watoto wa maskini hawawezi kusoma"
Haya ni maneno yaliyoibua matumaini makubwa kwa watanzania. Na bila shaka hoja hii ni miongoni mwa hoja zilizoshawishi wananchi kumpigia kura.
Ni kweli kuwa bila mikopo ni vigumu sana kwa watoto wa maskini kusoma elimu ya juu. Kwahiyo maskini wengi walitarajia watoto wao kunufaika na mikopo ya elimu na kuwapunguzia mzigo ikiwa Magufuli angeshinda Urais.
Lakini Magufuli akashinda Urais na bado mikopo ikaendelea kuwa changamoto. Mwaka wa kwanza peke yake zaidi ya wanafunzi elfu 20 wamekosa mikopo. Je Rais Magufuli amesahau ahadi zake wakati wa kampeni?
Tulitegemea kuwa katika kutimiza azma yake kwa wanafunzi wa elimu ya juu basi angalau wanafunzi wote walioanza mwaka wa kwanza mwaka jana wangepata mikopo.
Ikiwa kila mwanafunzi atalipiwa ada ya shilingi milioni mbili kwa mwaka (makisio) itahitajika jumla ya Shilingi bilioni 40 tu kutoa mikopo kwa wanafunzi 20,000 wa mwaka wa kwanza waliokosa.
Sasa ikiwa serikali inaokoa mabilioni kila siku imeshindwa kupata bilioni 40 ili watoto wa maskini waweze kusoma? Mabilioni yanayookolewa kila siku yanaenda wapi? Sio kiini macho??
Siku chache baada ya kuingia madarakani Rais Magufuli alitembelea hospitali ya taifa ya Muhimbili. Baada ya ziara ile zikasambaa habari mitandaoni kuwa Rais ametatua kero ya muda mrefu ya vitanda hospitali ya Muhimbili. Habari hizo ziliambatana na picha za vitanda vipya vya kisasa kwa ajili ya wagonjwa. Kiongozi mmoja wa serikali alinukuliwa akisema "sasa hivi Muhimbili idadi ya vitanda ni kubwa kuliko idadi ya wagonjwa"
Taarifa ile ilienea kwa kasi na kufanya watu waamini kuwa kweli tatizo la vitanda Muhimbili limekwisha. Lakii siku chache zilizopita Rais Magufuli alipofanya ziara tena hospitalini hapo alikuta wagonjwa wanalala chini. Hakuna vitanda vya kutosha, hata wodi ya kujifungulia kuna akina mama wanajifungulia chini. Kwa ujumla hali ni mbaya sana tofauti na ilivyoelezwa awali.
Sasa je taarifa ile ya awali kuwa Shida ya vitanda Mubimbili imekwisha ilisambazwa na nani? Kw lengo gani? Na kwanini serikali itoe matumaini ambayo hayapo? Serikali inafanya mazingaombwe?
Serikali kuokoa fedha nyingi ambazo zingetumika kwenye matumizi yasiyo na tija, kunakokwenda sambamba na juhudi za kukuza uchumi ni mambo ambayo yanatakiwa kumnufaisha mwananchi moja kwa moja.
Kwa mfano hakuna sababu ya kuendelea kutoza kodi kubwa kwa wafanyakazi wakati serikali inaweza kubuni vyanzo vingine vya mapato na kudhibiti matumizi vizuri.
Ikumbukwe Tanzania ndio nchi pekee Afrika Masharik ambayo hutoza kodi kubwa zaidi kwa wafanyakazi kuliko nchi nyingine za Afrika Mashariki. Kenya hutoza 9% (PAYE) kwa wenye mshahara chini ya Milioni moja za kitanzania, Uganda hutoza 11%, Rwanda 6% lakini Tanzania hutoza 18% kwa wenye mishahara chini ya Milioni moja.
Hii ina maana kwa Mwalimu wa kitanzania mwenye shahada ambaye mshahara wake unakadiriwa kuwa shilingi laki 7 kwa mwezi anakatwa kodi ya sh.126,000/= wakati mwalimu mwenzie wa Rwanda mwenye mshahara kama huo atakatwa 42,000/= tu kama kodi kwa mwezi.
Sasa jiulize huyu Mwalimu anayekatwa 126,000/= kama kodi, bado hajakatwa fedha za mifuko ya hifadhi ya jamii, hajakatwa mkopo wa elimu ya chuo kikuu kutoka bodi ya mikopo, hajalipa nauli ya daladala, hajalipa kodi ya nyumba, umeme na maji, anaishije?
Kama serikali ya Magufuli imeweza kubuni vyanzo vingine vya mapato, imeweza pia kudhibiti matumizi holela, pamoja na kuokoa mabilioni yaliyokua yakipotea, kwanini isipunguze mzigo huu wa kodi kwa wafanyakazi wa kitanzania?
Nakumbuka mgombea Urais wa UKAWA Mhe.Edward Lowassa aliwahi kuahidi kuwa ikiwa angeshinda Urais angepunguza kodi kwa wafanyakazi hadi kufikia asilimia yenye tarakimu moja (single digit). Yani kutoka 18% ya sasa hadi kuwa chini ya 9%.
Sasa kwanini Rais Magufuli asimuulize Lowassa angetumia mbinu gani ili kufanikisha hilo? Kwa kuwa wote lengo lao lilikua ni kuleta maendeleo na ustawi kwa wananchi si vibaya akimuomba ushauri.
Watu wengi hawajui kuwa wafanyakazi ndio kundi linalonyonywa zaidi nchini kuliko makundi yote yanayoingiza kipato.
Mwalimu anayelipwa mshahara wa Shilingi 700,000/= anatozwa 126,000/= kama kodi. Maana yake ni kwamba kipato cha Mwalimu huyu kwa mwaka ni Milioni 8.4 ambapo anakatwa milioni 1.5 kama kodi.
Lakini mfanya biashara anayemiliki daladala inayomuingizia shilingi 60,000/= kwa siku analipa kodi ya leseni ya barabara (road license) shilingi 200,000/= kwa mwaka ikiwa gari yake ni chini ya cc 2500. Kisha analipa ushuru wa njia (TLB) shilingi 400,000/= kwa mwaka. Jumla atalipa Shilingi 600,000/= kwa mwaka.
Lakini mfanyabiashara huyu anaingiza shilingi 60,000/= kwa siku ambayo ni sawa na 1,800,000/= kwa mwezi.
Sasa jiulize mtumishi mwenye mshahara wa 700,000 kwa mwezi anatozwa zaidi ya 1,500,000/= kwa mwaka kama kodi, lakini mfanyabiashara wa daladala anayeingiza 1,800,000/= kila mwezi anatozwa 600,000/= tu kwa mwaka kama kodi.
Bila shaka mfumo wa kodi wa nchi hii hauna usawa na umemuelemea zaidi mfanyakazi kuliko mfanya biashara. Ni wakati sasa wa serikali kufanya marejeo ya sheria ya kodi ili iendane sambamba na vipato vya watu.
Ni ajabu kwamba bado serikali inamnyonya mfanyakazi, bado inashindwa kusaidia watoto wa maskini kusoma kwa kuwapa mikopo, bado wagonjwa wanalala chini, lakini serikali hiyo inajitapa kila siku kuokoa mabilioni. Je yanakwenda wapi?
Waswahili husema "elimu aisaiyo na faida ni mbaya kuliko ujinga usio na hasara". Kwa hiyo mabilioni yasiyo na faida kwa mwananchi hayana maana.
Hivi kuna haja gani ya kumwambia mkeo umeongezwa mshahara kazini, lakini mkeo haoni faida ya ongezeko lako la mshahara? Bado maisha yake ni ya tabu, anaomba hadi chumvi kwa jirani lakini wewe unajitapa umeongezwa mshahara. Si afadhali usingesema?
Serikali ya Magufuli iache kutangaza kuwa imeokoa mabilioni wakati wananchi hawaoni faida ya mabilioni hayo. Serikali iache kuwapa wananchi matumaini wakati maisha yao bado ni duni.
Kuliko kutangaza kila siku kuwa mabilioni yanaokolewa wakati nauli zinapanda, bei za bidhaa zinapanda, kodi kwa wafanyakazi bado iko juu, wanafunzi hawana mikopo, ni afadhali wasitangaze kabisa kuhusu "mabilioni" yao maana wananchi wataona kuwa serikali inafanya mazingaombwe tu. Mchezo wa kiini macho.!
[Imechapwa Mwananchi, Jumatano February 24, 2015, ukurasa wa 25].