Serikali ya Magufuli imebuni adhabu mpya kwa mafisadi

Akikamatwa alihonga nyumba za serikali nitakubali kuwa wapo siriazi
 
Vitendo vya kifisadi vimechangia kwa kiasi kibubwa kuharibu taswira ya hii nchi na kuirudisha nyuma kimaendeleo. Vimeichafua hii nchi kuliko hata kina Lissu inasemekana wanaichafua. Uzalendo namba moja kwa Mwananchi wa Tanzania ni kuchukia ufisadi na mafisadi.

Dokta Slaa enzi hizo CHADEMA wakiwa CHADEMA aliwahi kusema, ''Tatizo kubwa kuliko yote nchi hii sio CCM, wala Sio Elimu, wala Sio Magonjwa. Tatizo kubwa na linayoimaliza Tanzania ni Ufisadi na ndio maana wao wamejipanga kupambana nao mpaka pumzi ya mwisho"

Limekuwa ni jambo la kawaida sana kwa Wezi wa mali za umma nchi hii, kufunguliwa kesi na kutoka kilahisi kabisa tena kwa jeuli zote. Kesi zao wakiwa nje huunguruma lakini siku ya hukumu jambo moja huwa linajulikana ni kuwa watatoka nje na kuwa huru.

Matajiri wengi waliopata mali kwa wizi hutumia:

I.MIANYA YA SHERIA ZETU MBOVU (walizotunga wenyewe) Eg Kina Chenge jeur yao ipo hapa.
II. Nguvu ya fedha zao kutoa RUSHWA kwa Majaji na maofisa wa serikali kuharibu upelelezi na hata mlolongo wa Kesi nzima. Refer kesi ya Iddi Simbaa au ile Madabida na ARV feki.
III. Silaha yao nyingine huwa ni KUPATA MAWAIKILI BINAFSI WENYE UWEZO WA JUU KUWATETEA. Refer Kesi ya Mohamed Kirua na Lukuvi juzi juzi.
IV.Kesi zao kuwa na mkono wa RAIS ambaye ana kinga ya kutoshtakiwa Eg Mramba kesi na hata Jeuri ya EL kusema kama yye fisadi kwenye Richmond basi afunguliwe kesi mahakamani akijua fika walishirikiana na rafiki yake JK.


KWA KUONA HILO MAGUFULI na serikali yake wamekuja kivingine, Wao ni mwendo wa kukufungulia kesi nyingi nyingi ikiwamo ya uhujumu uchumi wakijua fika huwezi kupata dhamana. Then jarada la kesi yako litazungushwa kwa miaka kadhaa na mwisho wa siku utafutiwa Kesi yako/zenu na kuachiliwa huru.

Siku chache mbele utafunguliwa mashtaka mapya na cycle ya usumbufu huku wewe ukiwa ndani unaendelea mpaka ipite miaka kadhaa.
Kwa mbinu hizo Mafisadi na hela zao zote wanajikuta wapo ndani, mbinu zao zote wanazotegemea kuwachomoa zinaishia huko na zinakuwa hazifanyi kazi. Option itakayobaki ni either kurudisha mali ya umma kwa namna flani au uende na maji.
Kuna mtu mmoja aliwahi kusema, Sheria zimeundwa kuwafunga maskini, lakini zama hizi tunaona mengine kabisa.
Kama ni kweli basi UFISADI WA KOROSHO Wahusika wajiandae! Watunga sheria za mkononi kulee karibu na soko la sea food inawahusu!
 
Fisadi aliyehonga wabunge na madiwani wa CHADEMA wahame chama kisha chaguzi za marudio zifanyike mbona hakamakatwi?!.
Ni mabilioni mangapi yametumika kuhonga na kurudia chaguzi za wabunge na madiwani?!. TUNAWA-ZOOM TU NA MAIGIZO YENU!.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kwa CCM hii, hiyo ilikuwa CCM ya Nyerere
Narudia tena kusema mafisadi hawana chama, wao wana wapi pa kupata maslahi, hakuna chama chochote kitakachoingia madarakani hawa watu wakawa mbali na hicho chama , mfano mzuri Edo katukanwa kila aina ya matusi juu ya ufisadi lakini leo yuko wapi, sidhani kama alikuwa na mapenzi sana Chadema. Wana uwezo wa kuingia chama chochote na kwa muda wowote wanaotaka.
Tuiongelee tu CCM kwa sababu ndicho chama kinachotoa mashtakiwa wengi wa uhujumu uchumi na mambo ya kisiasa ya usimba na yanga (simaanishi michezo ya hizo timu mbili).
 
Back
Top Bottom