Ng'wanza Madaso
JF-Expert Member
- Oct 21, 2008
- 2,268
- 333
Ndugu zanguni wana JF nilikuwa ninaperuzi kwa Michuzi nimekutana na habari hii Serikali ya Libya yajitokeza kusaidia Athari za mafiriko kilosa kuwa itawajengea nyumba 200 waathirika zenye thamani ya shilingi 1.5 bilioni.
Nikajiuliza serikali hii iliyosaidiwa imegharimika kumjengea mtu mmoja (Gavana) nyumba yenye thamani ya nyumba 200 ambazo wangejengewa watu wa kilosa lakini Serikali hii hii imeshindwa kuwajengea hawa waathirika na kuomba msaada. Je kama waliweza kumjengea Gavana nyumba yenye thamani hiyo imekuwaje wameshindwa kuwajengea hawa waathirika?
=====
Jamhuri ya watu wa Libya imetoa msaada wa vifaa mbalimbali kwa wahanga wa mafuriko ya Kilosa mkoani Morogoro. ikiwa ni pamoja na kuwajengea nyumba 200 zenye thamani ya shilingi bilioni 1.5.
Akiongea na wanahabari katika uwanja wa ndege Dar es Salaam Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Uratibu na Bunge) Mheshimiwa Philip Marmo alisema msaada huo umekuja wakati muafaka kwani hali ya wahanga hao si ya kuridhisha
Aidha Waziri Marmo alizitaka nchi rafiki,Jumuiya za Kimataifa pamoja na Watanzania kwa ujumla kutoa misaada kwa hiari yao kwa kadri wanavyoguswa kwa wahanga wa mafuriko ya Kilosa.
“Uwezo wa Serikali ni mdogo na hauwezi kutosheleza kila kitu hivyo tunaomba Jumuiya mabalimbali za Kimataifa na Watanzania Kushirikiana katika kutoa misaada”.Alisema.
Pia alizitaka Kamati za maafa husika kutekeleza wajibu wao kwa kufikisha misaada hiyo kwa wahusika na alimhakikishia balozi wa Libya nchini Ahmed Abdusalaam Al Ashaab ambaye alikabidhi msaada huo kwa niaba ya nchi yake kuwa itawafikia walengwa na magari yataanza kupeleka misaada hiyo kesho.
Akikabidhi msaada huo balozi wa Libya nchini bwana Ahmed Abdulsalaam Al Ashaab alisema msaada huo umetolewa na jumuiya mbalimbali nchini humo kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Libya.
Vifaa vilivyotolewa ni magaro 1100, Blanketi 400, Mahema 1300, Mito 1200, Maboksi 500 ya madawa ikiwa ni pamoja na vifaa vya huduma ya kwanza.
Source: Michuzi Blog
Soma

Pinda kukagua mafuriko Kilosa
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda leo mchana (Ijumaa, Januari 8, 2010) anatarajiwa kufanya ziara ya siku moja katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro kukagua athari za mafuriko na jitihada ambazo Serikali imefanya hadi sasa ili kuwasaidia waathirika wa maafa hayo. Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na...
www.jamiiforums.com
Leo JK yupo Kilosa!
Kwa habari nilizonazo, Leo JK yupo Kilosa mkoani Morogoro kuwafariji wahanga wa mafuriko. Pinda alianza yeye anafuatia! Pia soma https://www.jamiiforums.com/threads/pinda-kukagua-mafuriko-kilosa.49292/...
www.jamiiforums.com
Wahanga na Waathirika wa Mafuriko na Makanisa na Misikiti Yetu
Wakuu, Hivi tunafanya nini Makanisani na Misikitini kwetu katika kuwasaidia Watanzania wenzetu waliokumbwa na kuathiriwa na mafuriko makubwa hasa huko Kilosa na Dodoma?
www.jamiiforums.com