Serikali ya Libya yajitokeza Kusaidia Athari Za Mafuriko Kilosa kuwajengea Nyumba 200 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Libya yajitokeza Kusaidia Athari Za Mafuriko Kilosa kuwajengea Nyumba 200

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ng'wanza Madaso, Jan 17, 2010.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ndugu zanguni wana JF nilikuwa ninaperuzi kwa Michuzi nimekutana na habari hii Serikali ya Libya yajitokeza kusaidia Athari za mafiriko kilosa kuwa itawajengea nyumba 200 waathirika zenye thamani ya shilingi 1.5 bilioni.

  Nikajiuliza serikali hii iliyosaidiwa imegharimika kumjengea mtu mmoja (Gavana) nyumba yenye thamani ya nyumba 200 ambazo wangejengewa watu wa kilosa lakini Serikali hii hii imeshindwa kuwajengea hawa waathirika na kuomba msaada. Je kama waliweza kumjengea Gavana nyumba yenye thamani hiyo imekuwaje wameshindwa kuwajengea hawa waathirika?

  Soma hapa http://issamichuzi.blogspot.com/2010/01/serikali-ya-libya-yajitokeza-kusaidia.html#comments
   
 2. Sanctus Mtsimbe

  Sanctus Mtsimbe Tanzanite Member

  #2
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 14, 2008
  Messages: 1,815
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Jan 17, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Hawa si binadamu, wana mikono ya damu
  Ni walafi sina hamu, wastahili kali hukumu
  Tumuachie kaumu, yeye ataamua yao dumu!
   
 4. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #4
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  I know this is irrelevant, lakini ni vyema kulisema hili ili tusije tukawaacha baadhi ya watu wasiotaka kujua gravity ya vitu wanavyoviona kwa nje bila kujua undani wake. Agenda ya Muamar al Qud'dhafi ni kueneza Uislamu ili baadae kuanzisha dola ya Kisilamu ulimwenguni, na nashawishika hii ni mojawapo ya strategy, na tumeshaona sarakasi za namna hii nyingi ktk siku za karibuni. Uzuri tu hatujafikia hatua ya kulazimishana kwa upanga, ila maandalizi twayaona. Tuombee Mungu yote iwe kheri bila shari.
   
 5. Mpendanchi-2

  Mpendanchi-2 JF-Expert Member

  #5
  Jan 17, 2010
  Joined: Apr 4, 2009
  Messages: 305
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Kwanza tujiulize Libya imeanza lini urafiki na Tanzania!!!!, au baada ya Nyerere kufariki ndipo Libya inajitokeza tokeza je, ni kwa mazuri au kwa lengo gani!!!? TUJIULIZE!!!!
   
 6. b

  bitimkongwe JF-Expert Member

  #6
  Jan 17, 2010
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 3,034
  Likes Received: 211
  Trophy Points: 160
  Ndugu Mpendanchi, kwani ule msikiti ulioko Musoma kijijini kwa Nyerere si umefadhiliwa na Gaddafi? Tena wakati huo Nyerere bado alikuwa hai.

  Sasa kusaidia hizo nyumba imekuwa kuna ajenda ya siri?

  Najaribu tu kutafakari jinsi tulivo ndumilakuwili
   
 7. K

  KHATIBU New Member

  #7
  Jan 17, 2010
  Joined: Apr 13, 2009
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kusaidiwa sio tatizo ila ni kwa mazingir yapi,maana tusijikute tunabanwa na utumwa mamboleo.
   
 8. S

  Sumaku Member

  #8
  Jan 17, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani kuna mambo ya ajabu,lakini pia yapo ya kushangaza. Hii post yako inanishangaza? Hivi yale mafuriko yalibagua huyu Muislam na huyu Muanglikana au huyu hafuati dini yoyote? mm!chuki hufunika busara.
  Unaonaje endapo taasisi rasmi za kidini kama Vatican na nyinginezo zingetoa misaada hiyo,suala la kueneza Uislamu lingekuwepo?
  Binadamu yeyote anayepatwa na matatizo ni muhimu wenzake wakamsaidia. Je,umechangia kiasi gani ili kuwanusuru na Uislamu ambao kwako inaonekana ni nongwa kubwa?
   
 9. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #9
  Jan 17, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Nakubaliana na wasemao hatukuwa na haja ya kuanza kutembeza bakuli la kujenga nyumba 200 kule kilosa wakati tuna uwezo wa kujenga nyumba 1 kwa mtu 1 yenye gharama sawia...Ila napatwa na ukakasi na kichefu chefu kwa wenzangu wanaoangalia msaada wa Libya km mtego wa kueneza dini....huo ni mtazamo finyu...Matonya anapotembeza bakuli lake hachagui ni muislamu au mkristo au hta huyo mchangiaji ana malengo gani ya kiimani kwa msaada anaopewa...la muhimu kwake msaada umepatikana na hako ni ka ugonjwa na nina wasiwasi Nchi yetu inayotimiza nusu karne tokea kupata uhuru imeanza kuugua...Kama hadithi ya Matonya, usishangae kuona na kesho yake tena yupo barabarani bila aibu yeyote hata km jana alipata pesa nyingi na akazitumia kuhonga wanawake au kulewa pombe....
   
 10. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #10
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Labda nikuulize..ati na wewe ni Great Thinker?? Hivi uliielewa post yangu au basi tu ili mradi uongeze post JF??
   
 11. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #11
  Jan 17, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hizo nyumba ni za aina gani?

  Amandla........
   
 12. b

  bnhai JF-Expert Member

  #12
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Kweli umeshasema wewe mwenyewe ni Irrelevant. Last year Gaddaf alikuwa Italy kwenye ziara yake ndefu nchini humo na nchi kadhaa. Huko alienda kueneza hiyo dini? Abdulhalim mbona unaota dini kila siku? Mie nadhani kila nchi inatafuta trading partner maana km unazalisha unahitaji kuwa na soko. Na kadiri siku zinavyoenda Afrika ndio linaonekana kuwa soko linalokuwa kwa nguvu.
   
 13. b

  bnhai JF-Expert Member

  #13
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Niadhani za 7.5mil. Hiyo inajenga kabisa nyumba vijijini, tena baadhi ya vijijini wanapata nyumba imara za matofali ya kuchomwa
   
 14. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #14
  Jan 17, 2010
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Nashauri waangalie aina za nyumba zinazoweza kumudu mafuriko. Nyumba za asili katika sehemu kama hizi zilijengwa kwenye milingoti. Hizo za matofali ya kuchoma zinaweza zikawa adha badala ya heri. Kumbuka New Orleans yaliyowapata pamoja na nyumba zao kuwa za kisasa! Wakiwapelekea prefabs. watakuwa hawajafanya kitu.

  Amandla........
   
 15. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #15
  Jan 17, 2010
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni serikali ya Chama Cha Majambazi kusahau wajibu wake wa kujenga makazi bora kwa raia wake.
   
 16. MKUNGA

  MKUNGA JF-Expert Member

  #16
  Jan 17, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 443
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  jamani, ifike hatua tuwe reasonable, mimi naamini msaada ni msaada tu hata kama umetoka wapi, kwani kuna tatizo gani tukisaidiwa na Gaddafi?mbona Obama amesaidia ktk janga la Haiti na mpo kimya?kunani Great Thinkers?Au kuna watu duniani ndio wana haki ya kusaidia wenzao panapokua na maafa kama hayo ya Kilosa?
   
 17. saitama_kein

  saitama_kein JF-Expert Member

  #17
  Jan 17, 2010
  Joined: Oct 29, 2009
  Messages: 982
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33

  unamaanisha chama kipi? hicho.............
   
 18. b

  bnhai JF-Expert Member

  #18
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Serikali kazi yake si kujenga bali ni kuwawezesha wananchi waweze kujenga nyumba bora. Wakati fulani nadhani watu wanavyotoa commens zao wanakuwa usingizini.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Nafuu wewe umeliona hili la kueneza dini. Maana wengine hawalioni hili na watakataa katakata hata kwa mjeledi hawatalikubali. Kwenye post yangu sijakataa watu kusaidiwa wanapokuwa na shida au wanapoletewa uchaguzi wa dini 'mpya' au vinginevyo, ndio maana nikamalizia na post yangu kuwa tuombe hizi sarakasi zote ziishie kwa kheri. Ila historia haiendani na hii dua yangu, na ukweli kwamba maazimio ya baadhi ya dini ya kutawala dunia is simply beyond dictatorship & fascism combined.
   
 20. b

  bnhai JF-Expert Member

  #20
  Jan 17, 2010
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Duh narekebisha post yangu. Kumbe unaweza kukosea kitu kidogo ukawa quoted wrong. Hakueneza dini bali aliizungumzia dini yake km unakumbukumbu vizuri. Weka alama ya kuuliza pls
   
Loading...