Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 7,557
- 21,506
Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Mheshimiwa Song,Geum Young amesema serikali ya nchi hiyo itaendelea kuisadia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili ili kuiinua Tanzania kiuchumi.
Ameyasema hayo baada ya kukagua na kuzindua mradi wa ujenzi wa kituo cha elimu Mbinga mkoani Ruvuma utakaogharimu dola za kimarekani Milioni 150 ambacho kitafundisha walimu wa chekechea,walimu wa shule ya msingi na waganga ili kupunguza upungufu wa walimu na waganga nchini.
Balozi huyo amemwagia sifa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kutokana na kulinda railimali za Tanzania na utendaji kazi wake na kusema kuwa anaamini katika uongozi wake nchi ya Tanzania inaweza kuwa na maendeleo makubwa kwa kuwa miaka ya nyuma Korea Kusini ilikuwa maskini sawa na Tanzania lakini kutokana na uchapakazi wa watu wake na uongozi bora imepiga hatua kubwa ya maendeleo.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mbinga Bw.Cosmas Nshenye amesema kuwa kituo hicho cha elimu kitadumisha uhusiano kati ya Tanzania na Korea Kusini na kusaidia wananchi wa Mbinga.
Licha ya kushukuru kwa hatua ya ujenzi wa kituo cha elimu Mbinga Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Bw.Robert Mageni ameiomba serikali ya Korea kuisaidia halmashauri hiyo gari la kubeba wagonjwa ili kuokoa maisha ya wananchi wa vijijini.
Naye mdau wa maendeleo wa wilaya ya Mbinga Bw.Gaudence Kayombo amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho umeanza kwa kusawazisha eneo kutakapojengwa chuo hicho katika kata ya Ruhuwiko wilayani Mbinga.
ITV