Serikali ya Korea Kusini kuendelea kuisaidia Tanzania katika miradi ya maendeleo

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,557
21,497
sai.png

Balozi wa Korea Kusini hapa nchini Mheshimiwa Song,Geum Young amesema serikali ya nchi hiyo itaendelea kuisadia Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo ili ili kuiinua Tanzania kiuchumi.

Ameyasema hayo baada ya kukagua na kuzindua mradi wa ujenzi wa kituo cha elimu Mbinga mkoani Ruvuma utakaogharimu dola za kimarekani Milioni 150 ambacho kitafundisha walimu wa chekechea,walimu wa shule ya msingi na waganga ili kupunguza upungufu wa walimu na waganga nchini.

Balozi huyo amemwagia sifa Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli kutokana na kulinda railimali za Tanzania na utendaji kazi wake na kusema kuwa anaamini katika uongozi wake nchi ya Tanzania inaweza kuwa na maendeleo makubwa kwa kuwa miaka ya nyuma Korea Kusini ilikuwa maskini sawa na Tanzania lakini kutokana na uchapakazi wa watu wake na uongozi bora imepiga hatua kubwa ya maendeleo.

Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mbinga Bw.Cosmas Nshenye amesema kuwa kituo hicho cha elimu kitadumisha uhusiano kati ya Tanzania na Korea Kusini na kusaidia wananchi wa Mbinga.

Licha ya kushukuru kwa hatua ya ujenzi wa kituo cha elimu Mbinga Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya mji wa Mbinga Bw.Robert Mageni ameiomba serikali ya Korea kuisaidia halmashauri hiyo gari la kubeba wagonjwa ili kuokoa maisha ya wananchi wa vijijini.

Naye mdau wa maendeleo wa wilaya ya Mbinga Bw.Gaudence Kayombo amesema kuwa ujenzi wa kituo hicho umeanza kwa kusawazisha eneo kutakapojengwa chuo hicho katika kata ya Ruhuwiko wilayani Mbinga.

ITV
 
Tangu hawa wakorea waazimie kujenga daraja la koko bichi, niliwachukia sana wakati kuna maeneo mengi ya kupunguza foleni za maana hawajayazingatia, sasa huko mbinga si wangepeleka kiwanda hata cha nguo? wanapeleka vitu ambavyo hata serikali yetu inavimudu, hopeless kabisa
 
Kati ya nchi nilizotembea duniani nikazipenda ya kwanza ni hii, naipenda sana S.Korea niliishipo kama miaka mitatu. Serikali yao inavyojiendesha imejipanga sana na hakuna udikteta uchwara, wananchi wakisema hatumtaki Rais anatoka fasta anakaa mwingine. Kufanya kazi na hawa jamaa mara nyingi hua wapo honest na straight forward, mara mia mkosane ila hakudanganyi, anakupa live tu face to face. Sishangai walipofikia kiuchumi huku miaka ya sitini wote tulikua level moja, wanajituma sana, inabidi tuwaige. Nilikua natembea hata saa kumi usiku napishana na wadada wanatembea wenyewe kwenye vichochoro bila kua na uoga wowote, crime rate ipo chini balaa. Hiyo amani hata US sijaiona.
 
utakuwa na ghubu dunia nzima hakuna.
 
unakoelekea siko kabisa, unataka unitukane wakati sina rekodi ya kutukanana na watu
unahisi hutukani maana hujafundwa fanyia kazi ushauli wangu ili ni jukwaa la GT sio vihio, kujenga chuo kuleta wakufuzi ili kufuta ujinga watoto wetu wewe unabeza kama sio hasara ya tumbo lililokuzaa
 
Kati ya nchi nilizotembea duniani nikazipenda ya kwanza ni hii, naipenda sana S.Korea niliishipo kama miaka mitatu. Serikali yao inavyojiendesha imejipanga sana na hakuna udikteta uchwara, wananchi wakisema hatumtaki Rais anatoka fasta anakaa mwingine. Kufanya kazi na hawa jamaa mara nyingi hua wapo honest na straight forward, mara mia mkosane ila hakudanganyi, anakupa live tu face to face. Sishangai walipofikia kiuchumi huku miaka ya sitini wote tulikua level moja, wanajituma sana, inabidi tuwaige. Nilikua natembea hata saa kumi usiku napishana na wadada wanatembea wenyewe kwenye vichochoro bila kua na uoga wowote, crime rate ipo chini balaa. Hiyo amani hata US sijaiona.
kinachotugharimu mpaka tusifikie hayo mafanikio yao ni siasa chafu na uongozi mbaya. kumbuka nyerere aliwahi ku-quote development drivers akisema 1.watu (educated and literate) 2. ardhi (yenye rutuba na natural resources nyinginezo) 3. siasa safi na 4. uongozi bora

sasa tunakwamia wapi?
 
Back
Top Bottom