SERIKALI YA KITAIFA - Sera mpya ya mafisadi

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
Sera mpya inayoonekana kuundwa na Serikali za Kiafrika ambazo baadhi ya viongozi wake wakuu wamekuwa wagumu kuachia madaraka ni kutokubali kuondoka madarakani wakiweka lengo la kuunda serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Tatizo hilo limeanza kujitokeza kwa nguvu na kila sehemu ya Afrika hivi sasa kumekuwa na migogoro ya Serikali kutokubali kuondoka madarakani na kusababisha mvutano unaopelekea mauaji ya raia wasio na hatia na baada ya mauaji utasikia wengine wakipendekeza kuundwe serikali ya Kitaifa.
Wanaopendekeza ndio walawale ambao Nchi wanazotoka kuna matatizo ya kukubali kuachia madaraka ,aidha huu ni mkakati unaoonekana wa kupangwa na viongozi hawa.
Kwa mwenendo huu tutegemee kutawaliwa tena na wakoloni ambao wanaonekana kuzirandia nchi zetu kwa mara nyingine ,aidha kwa kuwatumia waliko ndani ya madaraka vilevile kwa kuwatumia upande wa upinzani.
Hivyo wanatupa misaada mingi na kuzifanya bajeti za nchi zetu maisha ziwe tegemezi mbali ya utajiri tuliojaaliwa kuliko nchi zao bado ,wanatumia akili ndogo tu kutuchanganya akili na kutuweka mikononi mwao.
Tuna utajiri wa kila aina wenye akili na utaalamu wanachohitaji ni fedha Je hatuwezi kuutumia utajiri na hazina za nchi zetu kuwalipa wataalamu wachache kiwango kikubwa cha mshahara huku tukiwaajiri katika sehemu nyeti za kutuwezesha kupiga hatua moja mbele.
Kuna Nchi kama za Iran ,Korea ambazo zimewaajiri wataalamu wenye kiwango cha juu cha elimu aidha direct kutoka Urusi China au Pakistani na kuwawezesha kutengeneza mipango ambayo leo hii wanaonekana japo ni masikini lakini nchi zao zina msimamo na zinajitegemea wala haziyumbishwi kwa kuambiwa tutawapunguzia sapoti kuisaidia bajeti yenu.Marekani amemaliza vitisho vyote kwa Irani na Korea na bila ya mafanikio yeyote zaidi ya kupigwa chenga misimamo ya Irani na Korea haijatetereka.
Mnaweza kuwa na kiongozi huyohuyo mmoja mpaka afae lakini nchi na wananchi wake wakawa wanaheshimika na wenyewe wanajiamini ,mfano Libya kiongozi wake ni wa muda mrefu lakini leo ukienda Libya hali ya maisha iliyokuwepo kwa mwananchi wa kawaida haimpi sababu ya kupigia makelele uongozi uliokuwepo.
Lakini mfano wa hapa kwetu hatuwezi kukazania CCM itawale maisha wakati hali ya maisha ya mwananchi ni mbaya na inachakaza hatuwezi kuwaachia mafisadi waendelee kutubinya na kutukamua huku hatujui kesho tutakula nini haiwezekani kuikubali sera ya kuunda serikali ya Kitaifa kwa kuwarudisha mafisadi madarakani kwa kisingizio cha kuidumisha amani Karume lazima aondike na Kikwete ujitaarishe kwani kipimo chako kinakuja keshokutwa 2010.
 
Back
Top Bottom