Serikali ya Kikwete yapoteza umaarufu

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,006
Utakuwaje na umaarufu wakati ahadi walizoahidiwa Watanzania hazijatimia na wala hazina dalili ya mafanikio, rushwa imeshamiri ndani ya CCM na siri kali, kashfa mbali mbali dhidi ya Mkapa, BOT, mikataba ya madini vyote hivi havielekei kuchunguzwa katika hali itakayowaridhisha wananchi na viongozi bado wanaongea katika lugha ambayo haina mvuto kwa Watnzania

Serikali ya Kikwete yapoteza umaarufu

na Charles Mullinda
Tanzania Daima

MWENENDO wa kisiasa hapa nchini umeanza kuonyesha dalili mbaya kwa Serikali ya Awamu ya Nne kiasi cha kuifanya ianze kupoteza umaarufu mkubwa ilioingia nao miaka takriban miwili iliyopita.
Matukio ya hivi karibuni yanayoonyesha kupanda kwa haraka haraka kwa umaarufu wa kambi ya upinzani, yanayokwenda sambamba na wananchi kukata tama, yanatoa picha moja ya wazi kuwa, ‘ushindi wa kishindo' unaanza kuonekana kuwa ni ruba kwa serikali iliyoingia madarakani kwa ahadi na mbwembwe nyingi.

Jeuri inayoanza kuonyeshwa na wananchi dhidi ya viongozi wa serikali ambao katika kipindi cha miaka 40 na ushei sasa kwa kiwango kikubwa imeanza kuwafanya wadadisi wa mambo kuanza kuiangalia kwa jicho tofauti Serikali ya Awamu ya Nne ambayo iliingia madarakani kwa gia ya ‘Maisha bora kwa kila Mtanzania.

Aidha, kutoonekana katika vitendo kwa kaulimbiu ya Kasi Mpya, Ari Mpya na Nguvu Mpya kumewafanya baadhi ya Watanzania, wakiwamo wasomi kuanza kuiona serikali kuwa iliyoshindwa kutekeleza ahadi lukuki ilizotoa kwa wananchi.

Ingawa viongozi takriban wote wakuu wamekuwa wakitoa kauli za kujiamini kuhusu kile wanachojaribu kuwaaminisha wananchi wakikubali, maamuzi yao ya hivi sasa yanaanza kuonyesha waziwazi kuwapo kwa hofu ya dhahiri kuwa upo uwezekano wa vyama vinne vya upinzani vinavyoshirikiana kuendelea kupata nguvu dhidi ya chama tawala na serikali yake.

Uamuzi wa Serikali na ule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwasambaza viongozi na makada wake katika mikoa mbalimbali nchini, pasipo kuangalia gharama za kufanya hivyo na pengine athari zake kisiasa, kiuchumi au kijamii kwa lengo linalotajwa kuwa ni kueleza kuhusu uzuri wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2007/08 na kuwajibu wapinzani wa vyama vine, unaonyesha dhahiri kulemewa kwa serikali.

Sasa ni wazi kwamba, serikali ambayo siku zote imekuwa ikipanga ajenda zinazojibiwa na wapinzani, yenyewe ndiyo imegeuka na kuanza kujibu hoja na ajenda zilizoandaliwa na wapinzani.

Kwa namna yoyote ile, kuzomewa kwa baadhi ya mawaziri, manaibu mawaziri, wabunge na viongozi wengine wa kiserikali katika mikutano ya hadhara, matukio ambayo sasa yanaonekana kushika kasi ya aina yake, hata baada ya kuwapo kwa jitihada za makusudi za kupindisha ukweli ni vielelezo vya wazi kuwa, ushindani wa kisiasa na hoja kati ya serikali na upinzani umeendelea kuwa mkali pengine kuliko wakati wowote wa uhai wa miaka 15 wa mfumo wa vyama vingi.

Kwa upande mwingine ni wazi kwamba, Rais Kikwete ambaye alitarajiwa kurejea nchini jana, akitoka katika ziara ndefu ya Marekani na Ulaya atakutana na matukio kadhaa ya mawaziri wake kuzomewa na wananachi wakati wakiwa katika ziara za kuelezea ubora wa bajeti ambayo tangu iliposomwa na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji miezi kadhaa iliyopita, ilionekana kuwa na dosari dhidi ya azima ya serikali ya kuwaletea wananchi maisha bora.

Mlolongo wa matukio haya, pamoja na shinikizo kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje, viongozi wa dini, wanaharakati na wananchi wanaotaka serikali ijisafishe dhidi ya tuhuma za ufisadi zinazoiandama, unaelezwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa utamtesa Rais Kikwete kwa sababu anawajibika kuisafisha serikali yake ili kurejesha imani ya serikali yake kwa makundi hayo.

Baadhi ya wanasiasa wamelieleza gazeti hili kuwa, Kikwete ndiye atakayetakiwa kujibu swali la mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pius Msekwa alilomuuliza Waziri Mkuu Edward Lowassa hivi karibuni mkoani Mwanza kuwa, ni kwa nini kauli za viongozi haziwiani na matendo yao na sababu zilizomfanya rais ateue watu kama wabunge kuwa wakuu wa mikoa ilhali Tanzania ikiwa na watu wengi wenye uwezo.

Mwanafunzi huyo alimuhoji Lowassa kuwa yeye na wasaidizi wake wanahimiza vijana kusoma kwa bidii na maarifa ili wawe viongozi wa taifa la kesho, lakini hawaoni hayo katika matendo yao. Lowassa alishindwa kujibu swali hilo.

Tukio jingine ambalo Rais Kikwete anapaswa kulifanyia kazi haraka ni la wasaidizi wake kutoa takwimu zisizo sahihi kwa viongozi wakuu wa serikali, jambo ambalo sasa limeanza kupingwa hadharani na wananchi pamoja na wabunge wao.

Kutofautiana hadharani kwa Mbunge wa Ukerewe, Gertrude Mongella na Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, dhidi ya ubora wa kivuko cha Sabasaba ambapo wananchi waliungana na mbunge wao kumpinga waziri huyo, ni doa jingine kwa Rais Kikwete linaloashiria kuwa wasaidizi wake hawana kauli za kweli.

Tofauti na matukio ya kuzomewa kwa makada wa CCM waliokuwa wakiandamana na Rais Kikwete kuomba kura za kuwa wabunge mwaka 2005, matukio yanaondelea hivi sasa ya kuzomewa kwa mawaziri wake wanaojaribu kuondoa sumu ya kuwepo ufisadi serikalini iliyomwaga na viongozi wa kambi ya upinzani nayo yanaashiria hasira walizonazo wananchi dhidi ya serikali.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa, katika hili, Rais Kikwete anapaswa ama kuwaondoa katika serikali yake mawaziri na viongozi wengine wanaookana kutokubaliwa na wananchi au kuanza kuzunguka mikoani kuyeyusha sumu iliyowatia matatani mawaziri wake, jambo ambalo linaweza kumgharimu kisiasa iwapo hoja atakazokwenda nazo kwa wananchi zitashindwa na zile walizoshibishwa wananchi na viongozi wa kambi ya upinzani.

Jambo jingine linalotarajiwa kumtesa Rais Kikwete ni namna nzuri ya kushughulikia shutuma za ufisadi kwa serikali ambazo zimewafanya mabalozi na viongozi wa dini kuionyeshea kidole serikali wakiitaka ijisafishe dhidi ya tuhuma hizo.

Haina shaka kwamba Rais Kikwete ambaye wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, aliungwa mkono kwa kiasi kikubwa na viongozi wa madhehebu ya dini, atalazika kutozitolea maelezo tuhuma hizo ili kutochafua uhusiano wake na viongozi hao.

Sambamba na viongozi wa dini, Rais Kikwete pia atapaswa kutumia ushawishi wake kuwalainisha mabalozi wa nchi za nje ambao wameonyesha kuguswa na tuhuma za ufisadi serikalini ili kuondoa uwezekano wa serikali kunyimwa misaada na mataifa wahisani.

Wafuatiliaji wa mambo wanaeleza kuwa Rais Kikwete atakuwa na wakati mgumu kukabiliana na wimbi la mabadiliko ya tabia za Watanzania za kukosa uvumilivu kwa viongozi wa serikali wanaoonyesha kutofautiana nao katika masuala mbalimbali.

Hatua ya hivi karibuni ya wakazi wa eneo la Chasimba nje kidogo ya eneo la Jiji la Dar es Salaam kumtia masinki na kumshambulia kwa mawe Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kanali Fabian Masawe, aliyekuwa akiwataka wakubaliane na uamuzi wa mahakama wa kuondoka eneo hilo, ni kielelezo cha wananchi kuanza kukosa uvumilivu dhidi ya viongozi wa serikali.

Katika hatua nyingine, ziara za mawaziri na manaibu waziri zinazoendelea katika mikoa mbalimbali kuwaeleza wananchi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2007/8, zimeichafua zaidi serikali baada ya kubainika kuwa lengo la ziara hizo ni kinyume na inavyoelezwa.

Imebainika kuwa lengo la ziara hizo ni kuwashambulia viongozi wa upinzani ambao hivi karibuni walizunguka mikoani wakieleza mambo kadhaa, ikiwamo udhaifu wa serikali katika baadhi ya maeneo.

Baadhi ya mawaziri hao wamekuwa wakizidisha hasira za wananchi wanapoeleza kuwa ziara zao ni za kiserikali, lakini wanapanda majukwaani wakiwa wamevalia sare rasmi za chama chao CCM na kutoa hotuba zisizogusia kabisa ubora wa bajeti, hivyo kupoteza maana nzima ya ziara hizo.

Aidha, Rais Kikwete anaweza kulazimika kufanya mabadiliko makubwa katika safu yake ya uongozi ili wingu la shaka walilonalo Watanzania wa nje ambao katika za usoni wanaonekana kufuatilia kwa karibu matukio mbalimbali ya hapa nyumbani na kila mara akiwa katika ziara zake za ughaibuni, wamekuwa wakitaka kuonana naye na kumuuliza maswali kuhusu utawala wake.

Ni dhahiri kwamba Watanzania walio nje ya nchi sasa wanamtesa Rais Kikwete na maswali yao magumu hadi kufikia hatua ya kukwepa kuonana nao mara mbili, jambo linalotafsiriwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa ni kuogopo kukosolewa na kusutwa na wananchi wake akiwa nje ya nchi ambako amejijengea heshima kubwa.
 
mzee ameshikwa patamu sijui kama atawasaficha hao mawaziri kutoka kwenye viti vyao maana wote wanamtandao walioshilikiana kuweka madarakani
 
Utakuwaje na umaarufu wakati ahadi walizoahidiwa Watanzania hazijatimia na wala hazina dalili ya mafanikio, rushwa imeshamiri ndani ya CCM na siri kali, kashfa mbali mbali dhidi ya Mkapa, BOT, mikataba ya madini vyote hivi havielekei kuchunguzwa katika hali itakayowaridhisha wananchi na viongozi bado wanaongea katika lugha ambayo haina mvuto kwa Watnzania

Serikali ya Kikwete yapoteza umaarufu

na Charles Mullinda
Tanzania Daima

MWENENDO wa kisiasa hapa nchini umeanza kuonyesha dalili mbaya kwa Serikali ya Awamu ya Nne kiasi cha kuifanya ianze kupoteza umaarufu mkubwa ilioingia nao miaka takriban miwili iliyopita.
Matukio ya hivi karibuni yanayoonyesha kupanda kwa haraka haraka kwa umaarufu wa kambi ya upinzani, yanayokwenda sambamba na wananchi kukata tama, yanatoa picha moja ya wazi kuwa, &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];ushindi wa kishindo' unaanza kuonekana kuwa ni ruba kwa serikali iliyoingia madarakani kwa ahadi na mbwembwe nyingi.

Jeuri inayoanza kuonyeshwa na wananchi dhidi ya viongozi wa serikali ambao katika kipindi cha miaka 40 na ushei sasa kwa kiwango kikubwa imeanza kuwafanya wadadisi wa mambo kuanza kuiangalia kwa jicho tofauti Serikali ya Awamu ya Nne ambayo iliingia madarakani kwa gia ya &[HASHTAG]#8216[/HASHTAG];Maisha bora kwa kila Mtanzania.

Aidha, kutoonekana katika vitendo kwa kaulimbiu ya Kasi Mpya, Ari Mpya na Nguvu Mpya kumewafanya baadhi ya Watanzania, wakiwamo wasomi kuanza kuiona serikali kuwa iliyoshindwa kutekeleza ahadi lukuki ilizotoa kwa wananchi.

Ingawa viongozi takriban wote wakuu wamekuwa wakitoa kauli za kujiamini kuhusu kile wanachojaribu kuwaaminisha wananchi wakikubali, maamuzi yao ya hivi sasa yanaanza kuonyesha waziwazi kuwapo kwa hofu ya dhahiri kuwa upo uwezekano wa vyama vinne vya upinzani vinavyoshirikiana kuendelea kupata nguvu dhidi ya chama tawala na serikali yake.

Uamuzi wa Serikali na ule wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwasambaza viongozi na makada wake katika mikoa mbalimbali nchini, pasipo kuangalia gharama za kufanya hivyo na pengine athari zake kisiasa, kiuchumi au kijamii kwa lengo linalotajwa kuwa ni kueleza kuhusu uzuri wa bajeti ya Serikali ya mwaka 2007/08 na kuwajibu wapinzani wa vyama vine, unaonyesha dhahiri kulemewa kwa serikali.

Sasa ni wazi kwamba, serikali ambayo siku zote imekuwa ikipanga ajenda zinazojibiwa na wapinzani, yenyewe ndiyo imegeuka na kuanza kujibu hoja na ajenda zilizoandaliwa na wapinzani.

Kwa namna yoyote ile, kuzomewa kwa baadhi ya mawaziri, manaibu mawaziri, wabunge na viongozi wengine wa kiserikali katika mikutano ya hadhara, matukio ambayo sasa yanaonekana kushika kasi ya aina yake, hata baada ya kuwapo kwa jitihada za makusudi za kupindisha ukweli ni vielelezo vya wazi kuwa, ushindani wa kisiasa na hoja kati ya serikali na upinzani umeendelea kuwa mkali pengine kuliko wakati wowote wa uhai wa miaka 15 wa mfumo wa vyama vingi.

Kwa upande mwingine ni wazi kwamba, Rais Kikwete ambaye alitarajiwa kurejea nchini jana, akitoka katika ziara ndefu ya Marekani na Ulaya atakutana na matukio kadhaa ya mawaziri wake kuzomewa na wananachi wakati wakiwa katika ziara za kuelezea ubora wa bajeti ambayo tangu iliposomwa na Waziri wa Fedha, Zakia Meghji miezi kadhaa iliyopita, ilionekana kuwa na dosari dhidi ya azima ya serikali ya kuwaletea wananchi maisha bora.

Mlolongo wa matukio haya, pamoja na shinikizo kutoka kwa mabalozi wa nchi za nje, viongozi wa dini, wanaharakati na wananchi wanaotaka serikali ijisafishe dhidi ya tuhuma za ufisadi zinazoiandama, unaelezwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa utamtesa Rais Kikwete kwa sababu anawajibika kuisafisha serikali yake ili kurejesha imani ya serikali yake kwa makundi hayo.

Baadhi ya wanasiasa wamelieleza gazeti hili kuwa, Kikwete ndiye atakayetakiwa kujibu swali la mwanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Pius Msekwa alilomuuliza Waziri Mkuu Edward Lowassa hivi karibuni mkoani Mwanza kuwa, ni kwa nini kauli za viongozi haziwiani na matendo yao na sababu zilizomfanya rais ateue watu kama wabunge kuwa wakuu wa mikoa ilhali Tanzania ikiwa na watu wengi wenye uwezo.

Mwanafunzi huyo alimuhoji Lowassa kuwa yeye na wasaidizi wake wanahimiza vijana kusoma kwa bidii na maarifa ili wawe viongozi wa taifa la kesho, lakini hawaoni hayo katika matendo yao. Lowassa alishindwa kujibu swali hilo.

Tukio jingine ambalo Rais Kikwete anapaswa kulifanyia kazi haraka ni la wasaidizi wake kutoa takwimu zisizo sahihi kwa viongozi wakuu wa serikali, jambo ambalo sasa limeanza kupingwa hadharani na wananchi pamoja na wabunge wao.

Kutofautiana hadharani kwa Mbunge wa Ukerewe, Gertrude Mongella na Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, dhidi ya ubora wa kivuko cha Sabasaba ambapo wananchi waliungana na mbunge wao kumpinga waziri huyo, ni doa jingine kwa Rais Kikwete linaloashiria kuwa wasaidizi wake hawana kauli za kweli.

Tofauti na matukio ya kuzomewa kwa makada wa CCM waliokuwa wakiandamana na Rais Kikwete kuomba kura za kuwa wabunge mwaka 2005, matukio yanaondelea hivi sasa ya kuzomewa kwa mawaziri wake wanaojaribu kuondoa sumu ya kuwepo ufisadi serikalini iliyomwaga na viongozi wa kambi ya upinzani nayo yanaashiria hasira walizonazo wananchi dhidi ya serikali.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanaeleza kuwa, katika hili, Rais Kikwete anapaswa ama kuwaondoa katika serikali yake mawaziri na viongozi wengine wanaookana kutokubaliwa na wananchi au kuanza kuzunguka mikoani kuyeyusha sumu iliyowatia matatani mawaziri wake, jambo ambalo linaweza kumgharimu kisiasa iwapo hoja atakazokwenda nazo kwa wananchi zitashindwa na zile walizoshibishwa wananchi na viongozi wa kambi ya upinzani.

Jambo jingine linalotarajiwa kumtesa Rais Kikwete ni namna nzuri ya kushughulikia shutuma za ufisadi kwa serikali ambazo zimewafanya mabalozi na viongozi wa dini kuionyeshea kidole serikali wakiitaka ijisafishe dhidi ya tuhuma hizo.

Haina shaka kwamba Rais Kikwete ambaye wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, aliungwa mkono kwa kiasi kikubwa na viongozi wa madhehebu ya dini, atalazika kutozitolea maelezo tuhuma hizo ili kutochafua uhusiano wake na viongozi hao.

Sambamba na viongozi wa dini, Rais Kikwete pia atapaswa kutumia ushawishi wake kuwalainisha mabalozi wa nchi za nje ambao wameonyesha kuguswa na tuhuma za ufisadi serikalini ili kuondoa uwezekano wa serikali kunyimwa misaada na mataifa wahisani.

Wafuatiliaji wa mambo wanaeleza kuwa Rais Kikwete atakuwa na wakati mgumu kukabiliana na wimbi la mabadiliko ya tabia za Watanzania za kukosa uvumilivu kwa viongozi wa serikali wanaoonyesha kutofautiana nao katika masuala mbalimbali.

Hatua ya hivi karibuni ya wakazi wa eneo la Chasimba nje kidogo ya eneo la Jiji la Dar es Salaam kumtia masinki na kumshambulia kwa mawe Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Kanali Fabian Masawe, aliyekuwa akiwataka wakubaliane na uamuzi wa mahakama wa kuondoka eneo hilo, ni kielelezo cha wananchi kuanza kukosa uvumilivu dhidi ya viongozi wa serikali.

Katika hatua nyingine, ziara za mawaziri na manaibu waziri zinazoendelea katika mikoa mbalimbali kuwaeleza wananchi kuhusu utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2007/8, zimeichafua zaidi serikali baada ya kubainika kuwa lengo la ziara hizo ni kinyume na inavyoelezwa.

Imebainika kuwa lengo la ziara hizo ni kuwashambulia viongozi wa upinzani ambao hivi karibuni walizunguka mikoani wakieleza mambo kadhaa, ikiwamo udhaifu wa serikali katika baadhi ya maeneo.

Baadhi ya mawaziri hao wamekuwa wakizidisha hasira za wananchi wanapoeleza kuwa ziara zao ni za kiserikali, lakini wanapanda majukwaani wakiwa wamevalia sare rasmi za chama chao CCM na kutoa hotuba zisizogusia kabisa ubora wa bajeti, hivyo kupoteza maana nzima ya ziara hizo.

Aidha, Rais Kikwete anaweza kulazimika kufanya mabadiliko makubwa katika safu yake ya uongozi ili wingu la shaka walilonalo Watanzania wa nje ambao katika za usoni wanaonekana kufuatilia kwa karibu matukio mbalimbali ya hapa nyumbani na kila mara akiwa katika ziara zake za ughaibuni, wamekuwa wakitaka kuonana naye na kumuuliza maswali kuhusu utawala wake.

Ni dhahiri kwamba Watanzania walio nje ya nchi sasa wanamtesa Rais Kikwete na maswali yao magumu hadi kufikia hatua ya kukwepa kuonana nao mara mbili, jambo linalotafsiriwa na wafuatiliaji wa mambo kuwa ni kuogopo kukosolewa na kusutwa na wananchi wake akiwa nje ya nchi ambako amejijengea heshima kubwa.

Habari hii ya kuisoma tena.
 
Kwani uongo? Mpaka kukoromewa na Mwinyi, Butiku, Warioba na Watanzania walio wengi wanaojitambua. Kumbuka EPA, Richmond, IPTL, Escrow, ari mpya nguvu mpya na kazi mpya pia maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana.

Huyu mwingine mkurupukaji, metekaji, mtesaji na uliza wapi alipo Ben Saanane mwaka sasa na shambulizi la Lissu unajua fika nini lilikuwa kusudio la shambulizi lile.

Na leo mmeanza tena kwa JPM..
 
Endeleeni kuilalamikia serikali siku zote. Maisha yanaenda

"Kabla ujauliza serikali imekufanyia nini, jiulize kwanza wewe umeifanyia nini serikali." By J.F Kennedy
 
Kwani uongo? Mpaka kukoromewa na Mwinyi, Butiku, Warioba na Watanzania walio wengi wanaojitambua. Kumbuka EPA, Richmond, IPTL, Escrow, ari mpya nguvu mpya na kazi mpya pia maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana.

Huyu mwingine mkurupukaji, metekaji, mtesaji na uliza wapi alipo Ben Saanane mwaka sasa na shambulizi la Lissu unajua fika nini lilikuwa kusudio la shambulizi lile.
Umewapa haki yao maana wameamua kufukua kaburi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Flexible in what sense? I call a spade by its original name there is no need to lie. Nilipoingia madarakani sukari ilikuwa 5,000 au pesa za Escrow si pesa za Serikali.

BAK jaribu kuwa flexible kwenye siasa don't be too extremely.
 
Mzandiki na mnafiki hawezi kuelewa maana ya "flexible" mkuu.
Huyu jamaa anakula matapishi yake kila kukicha. Hana lolote zaidi ya chuki na sumu ya ukabila inamtafuna.
Watu wa aina hii ni hatari sana katika jamii.
 
Kwani uongo? Mpaka kukoromewa na Mwinyi, Butiku, Warioba na Watanzania walio wengi wanaojitambua. Kumbuka EPA, Richmond, IPTL, Escrow, ari mpya nguvu mpya na kazi mpya pia maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana.

Huyu mwingine mkurupukaji, metekaji, mtesaji na uliza wapi alipo Ben Saanane mwaka sasa na shambulizi la Lissu unajua fika nini lilikuwa kusudio la shambulizi lile.
We lofa kweli! Mbona Kubenea anajua Ben alipo na huandiki ukweli? Si Kubenea aliandika Ben anaonekana usiku kwenye vijiwe vya kahawa na washkaji zake!! Bado unaleta chuki yako kwa JPM tu!! JPM is there to stay man! Switch your brain!
 
tapatalk_1506691448576.jpeg

Daaahhh!

Ukweli unauma sana.

Siku 90 sio nyingi, mpe hai JPM

Mwambie soon tutakuja kuomba ukumbi wa Ikulu tufanyie mkutano wetu wa Upinzani
 
Kwani uongo? Mpaka kukoromewa na Mwinyi, Butiku, Warioba na Watanzania walio wengi wanaojitambua. Kumbuka EPA, Richmond, IPTL, Escrow, ari mpya nguvu mpya na kazi mpya pia maisha bora kwa kila Mtanzania yanawezekana.

Huyu mwingine mkurupukaji, metekaji, mtesaji na uliza wapi alipo Ben Saanane mwaka sasa na shambulizi la Lissu unajua fika nini lilikuwa kusudio la shambulizi lile.
Ni ajabu sana. Pale usiku na mchana unampinga JPM; wakati huohuo umemkumbatia EL kama Maua Sama katika Mahaba Niuwe.
 
Back
Top Bottom