Serikali ya Kikwete yaja na itikadi ya kuhamasisha vyombo vya habari kuzomea wapinzani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Kikwete yaja na itikadi ya kuhamasisha vyombo vya habari kuzomea wapinzani

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Candid Scope, May 10, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  May 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Waziri Mkulo kwa dhamana yako kama waziri wa fedha umekiuka misingi ya uongozi kwa kuchochea na kuhamasisha umma na vyombo vya habari kumzomea Zito Kabwe. Tulitazamia ujibu hoja kiungwana lakini umeitisha vyombo vya habari kushinikiza na kuchochea vimzomee Zito Kabwe. Ndivyo CCM inavyokuja na sera ya zomea zomea kama chekechea jinsi wabunge wa ccm wanavyofanya bungeni dhidi ya wabunge wa upinzani.

  Mkulo umesema wongo mkubwa kwa kuainisha kwamba mapato ya kodi serikalini yanatosheleza kulipa mishahara na kubaki kinyume na hotuba yako ya bunge la mwaka jana ulipowasilisha bajeti ya serikali. Ulipowasilisha bajeti mwaka jana hukusema mapato ya kodi ni kwa ajili ya mishahara tu bali ni kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya serikali ikiwa ni pamoja na huduma za jamii, watumishi, maendeleo nk. na pengo lililopo linazibwa na misaada toka nje ya nchi mataifa wahisani. Kwa maana hiyo ulivyoainisha kwa waandishi wa habari ni usanii wa kutetea ucheleweshaji wa mishahara na posho za watumishi.

  Mwishoni mwa mwezi uliopita na mwanzoni mwa mwezi huu tumeshuhudia wengi wakilalamika kucheleweshewa misharaha na hata hapa jamii forum kulikua na thread inayolalamikia ucheleweshaji wa mishahara, na wewe Mkulo ulipoongea na vyombo vya habari hukufafanua ucheleweshaji huo ila umeendelea kumvaa Zito Kabwe na mishahara ya wabunge. Zito hakuweka wigo kwa mishahara ya wabunge tu ila tatizo la mishahara kitaifa kwa wafanyakazi.

  Serikali ya CCM naishauri iondokane na itikadi za zomea zomea kama wabunge wao walivyokwisha zoeleka bungeni, badala yake wajikite katika kutekeleza rasimu ya majukumu kwa wananchi na ilani ya uchaguzi. Kuzomea hakutaondoa matatizo yanayowakabili wananchi bali zomea inaonyesha mnavyoishiwa hoja ila kupitisha pitisha miswada bungeni kwa manufaa yenu badala ya maendeleo kwa Taifa letu.

  Nahitimisha kwa kusema CCM na serikali yake iwe flexable na mfumo wa upinzani kuwa na nguvu na kushika kasi. Inaelekea kasi ya upinzani inawashinda nguvu CCM na serikali yake ndio maana wanaibuka na dhana ya zomea zomea. Nilifikiri ni wabunge tu wanaofanya hiyo zomea zomea kumbe ni itikadi za serikali kutokana na kauli ya Mkulo kuhamasisha na kuchochea vyombo vya habari na wanachi kumzomea Zito Kabwe.


  Anayeishiwa na kushindwa hoja hutumia ngao ya kuzomea
   
 2. Shenkalwa

  Shenkalwa JF-Expert Member

  #2
  May 10, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 580
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nisingetegemea hata siku moja serikali ya ccm ikubali kuwa ina hali mbaya kifedha maana itakuwa aibu sana na kuumbuka juu ya wanavyoumbuka sasa. Watajitutumua tu na maneno ya uongo kuwaridhisha wadanganyika kumbe huko sirini wanajuta kumfahamu cdm. Si unajua sasa hivi zile fedha za EPA zimeshakwisha wameshakomba kila mahali sasa na hali hii mbaya kifedha lazima wanaunda mkakati wa kuchota. Sasa kama hazina yenyewe iko hoi sijui watachota wapi. Labda zile zinazotolewa misaada kutoka kwa wafadhili mbalimbali. Nchi inakwenda hiyooooooooooo
   
 3. S

  Shamwile Member

  #3
  May 10, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Shame upon you honorable Mkulo for things which you are speaking while even your conscious denies you!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  May 10, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Ni upotoshaji mkubwa kwamba pesa za kodi zinatumika kwa ajili ya mishahara wakati zina matumizi makubwa zaidi ya mishahara. Huduma za jamii, vyombo vya usalama, maendeleo nk hizo zote zinatoka wapi kama si hizo za walipa kodi? Hawezi kutudanganya kwa figure alizoleta kinyume na alivyoainisha lipowakilisha mswada wa bajeti ya serikali mwakajana. Watanzania tumeamka, hatudanganyiki tena.
   
 5. Y

  Yetuwote Senior Member

  #5
  May 10, 2011
  Joined: Jul 22, 2010
  Messages: 194
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kuwa watanzania wameishaelimishwa wakaelimika, ategemee kuzomewa.
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  May 10, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Ccm haina hata mtu mmoja mwenye akili timamu. Hakuna. Wote ni vilaza. Wanafikiri kwa miguu badala ya kichwa.
   
 7. Hassan J. Mosoka

  Hassan J. Mosoka JF-Expert Member

  #7
  May 10, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 647
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Kinyume chake wananchi waliofunguka macho tumeona wakiwazomea wabunge wa chama tawala si mmeona pale Muleba!!!!!!!!!!
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  May 10, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Honorable kwa ajili ya lile upara lake ??? silipendi hili zee kama nini
   
 9. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #9
  May 10, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Hata Mwakyembe kazomewa nyumbani kwao!
   
 10. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #10
  May 10, 2011
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,050
  Likes Received: 3,081
  Trophy Points: 280
  Sisi wafanyakazi tunamtaka huyu mh.uchwara Mkullo atoe maelezo kwanini siku hizi mishahara inavuka tarehe 23 zilizokuwa zimewekwa awali enzi za Mkapa,ni nini kinapelekea hali hii?na kwanini mpaka mwezi unaisha siku hizi bado mishahara haijatoka,ama siku hizi hazina imehamishiwa far-east?
   
 11. A

  Ame JF-Expert Member

  #11
  May 10, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Aise mbona unamkataza acha iwe hivyo tuone nani atakaye zomewa zaidi. Mbona tumeshashindwa kufuata sheria tangu zamani acheni tuingie kwenye level nyingine ya amani haiji ila kwa ncha ya upanga nahasa kama upanga wenyewe ni kuzomea basi mbona ni heri tu?
   
 12. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #12
  May 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Huyu Mkulo anafikiri watanzania bado ni wapuuzi kama walivokuwa miaka 10 iliyopita... Sisi tunaochangia humu na kumuunga mkono Mh. Zitto ni waathirika pia wa serikali ya Chama cha Magamba kukosa hela.... Kwani ni nani asiyejua kuwa toka October hamtoi tena OC kwenye ofisi za umma au na hilo ni uongo? IMF kutoa angalizo msichukue hela za miradi kulipa mishahara ni uthibitisho tosha kuwa hakuna hela za kulipia mishahara. Sasa unachobisha ni nini? Mkulo huongei na watoto wadogo kumbuka, tuna akili timamu na tunajua tunachokiongea nini na tunajua kwanini tunamuunga mkono Mh.Zitto! Mh. Mkulo utazunguka lakini nakuhakikishia TIME WILL TELL!!

  Angalizo: Hizo hela mnazotumia huko kwenye semina yenu si zingetosha kulipia mishahara ya robo ya wafanyakazi wa serikali?
   
 13. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #13
  May 10, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Najaribu kutafuta picha iwapo wabunge wa CHADEMA wangekuwa na kitabia cha kuzomea bungeni wangitwaje, kama kuandaa maandamano elimishi wanaitwa chama cha wahuni na wasio itakia mema nchi yetu, sijui siku moja wakianza zomeazomea wataitwaje. Lakini tusimshambulie mkulo bure hicho ni kiwango chake cha uelewa angekuwa na uwezo wajuu kidogo asinge ji-contradict.
   
 14. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #14
  May 10, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Utalipendaje wakati ni jizi na liongo? Lenyewe ndio tutalizomea likiingia kwenye anga zetu. Linakera sana hili li mtu halafu sio raia wa Tanzania. Upole wetu na slogan za kipumbavu za CCM za amani na utulivu ndio zinazofanya mizee mipumbavu kama Mkulo iendelee kutuletea kauli za kipuuzi.
   
 15. Jeremiah

  Jeremiah JF-Expert Member

  #15
  May 10, 2011
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 642
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Mkulo you are in deep shit.
   
 16. myhem

  myhem JF-Expert Member

  #16
  May 10, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Haya ndo matatizo ya kuwapa wageni nafasi nyeti kwani huwa hawana uchungu na nchi kabisa.Huyu waziri anatudharau watz na kutufanya sisi wapumbavu.Anafikiri sisi hatuna uwezo wa kupambanua mambo ndio maana anaongea upuuzi mtupu.Nchi zinaotufadhili hazina imani nahuyu waziri na hazimtaki kutokana na utendaji wake mbovu lkn sielewi kwanini JK anamng'ang'ania tu.

  Wa kuzomewa ni yeye mkulo na si Zitto.Ni bora Zitto amgeuzie kibao na kuwahamasisha wananchi wamzomee yeye kwani hana adabu hata kidogo.
   
 17. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #17
  May 10, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Nakuunga mkono kabisa hili zee jizi ndio la kulizomea na ikibidi kulipiga mawe likionekana kupita anga zetu.... sababu linataka kutufanya sisi wapuuzi kwamba hatuwezi kupambanua!!!
   
 18. k

  kagamba kadogo Senior Member

  #18
  May 10, 2011
  Joined: Apr 24, 2011
  Messages: 178
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hahahah my beer!!!!!!!!!!
   
 19. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #19
  May 11, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kiwango hiki cha Mkulo angelonga mbunge wa Chadema magazeti ya serikali ungesikia yanavyoshambulia. Halafu heshima ya uwaziri kwa umma haina zamana katika matamshi yake
   
 20. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #20
  May 11, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,612
  Likes Received: 82,204
  Trophy Points: 280

  ....Pamoja na Mkuu wake wa Kazi ambaye yuko tayari kumlaumu kila mtu kuhusu utendaji mbovu wa Serikali yake ya kisanii lakini hayuko tayari kujiona kama yeye kwa utendaji wake mbovu ndiye chanzo cha matatizo mengi yanayoendelea ndani ya nchi yetu
   
Loading...