Serikali ya Kikwete ni dhaifu kupita zote duniani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Kikwete ni dhaifu kupita zote duniani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by ibange, Mar 14, 2011.

 1. i

  ibange JF-Expert Member

  #1
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 1,545
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  serikali ya jk imeonyesha udhaifu mkubwa katika mambo mengi. lakini hili la loliondo limevunja record. hakuna serikali yoyote duniani inayoweza kuruhusu watu watumie dawa bila ku prove usalama wa dawa hiyo. hapa swala la imani halipo so long as watu wanakunywa dawa. ingekuwa kuombewa ndio ingekuwa imani. je ikigundulika baadae ina madhara watakufa watu milioni ngapi? je, mbona wasimpime mtu aliyepona na wakatoa taarifa rasmi? je, nchi inaweza kuishi kwa rumours tu? serikali makini ingechukua hatua muafaka
  http://www.google.com
   
 2. R

  Rutakyamilwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 27, 2009
  Messages: 1,869
  Likes Received: 1,161
  Trophy Points: 280
  I guess there is apoint here!!! serikali makini haiwezi kuruhusu kitu ambacho ni kinyume cha SHERIA. As long as imani inaingilia sheria ya nchi, basi sheria ya nchi ina-prevail over the other. Suppose dawa ya babu inaperpertuate cancer after 10 years, who will be to blame.
  ILA SIJUI KAMA SERIKALI YA JK NDIO DHAIFU KULIKO ZOTE DUNIANI
   
 3. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #3
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kemikali za kupimia hao waliotibiwa zitatoka wapi. Uwezo huo upo? Watu walishagundua kwamba nchi hii haina kitu. Ni kwa sababu hiyo kipimo chao ni kupona. Yanayokuja baadae kwa Mtanzania si muhimu.
  Ipo siku taifa zima litaangamia kwa sababu hizi hizi. Mkemia mkuu tunaye, lakini hebu kumbuka yale maji yenye mercury kule Mara majibu ya mkemia mkuu yalitolewa hadi leo? Kama sina hakika imepita miaka mitatu. Mercury inavipimo vyake vinavyojulikana duniani lakini kutoa majibu imechukua miaka mitatu.
  Kwa staili hii majibu ya madhara ya dawa ya babu wa Loliondo itachukua karne ngapi? Rafiki yangu sidhani kama unaifahamu Tanzania. Nchi hii ipo katika lindi la usingizi. Watu weke wamezama katika mashimo yaliyochini ya vilindi vya bahari je wataiona lini ile nuru?
  Acha kufikiri kama vile upo magharibi, hapa siyo. Nchi yetu ni hakuna, hakuna, hakuna kabisa.
   
 4. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #4
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,765
  Likes Received: 6,090
  Trophy Points: 280
  Ndugu, kwa maoni yangu una hoja ila si kwa kuwa serikali imechelewa/zembea kuchunguza dawa ya Babu bali kwa kuwa serikali yetu always inazembea kwenye mambo ya msingi yakiwamo yale yanayogusa afya za wananchi moja kwa moja. Wewe unakuwa na hofu na dawa ya Babu kwamba inaweza kuleta madhara baada ya miaka kadhaa; sawa inawezekana lakini madhara hayo, kama yatakuwepo ni madogo mno kulinganisha na madhara mengine mengi ambayo wananchi WOTE (na siyo wagonjwa wachache tu kama ilivyo kwa Babu) tunayapata katika maisha yetu ya kila siku bila serikali yetu kujishughulisha. Hebu fikiria mifano michache ifuatayo:-

  (i) Vyakula - nyama ya kuku wa kisasa:- Hivi unajua aina ya vyakula ambavyo kuku wa kisasa wanalishwa? Inadaiwa baadhi ya wafugaji wamefikia hata hatua ya kuwalisha ARVs, vidonge vya uzazi, na madawa mengine mengi ambayo yana madhara makubwa kwa binadamu. Je, ulishawahi kusikia serikali yetu angalau ikijishughulisha kufanya uchunguzi wa nyama ya kuku inayoingia sokoni? Ni maelfu ya watanzania wangapi wanaotumia nyama ya kuku kila siku?

  (ii) Vyakuala - Maziwa ya ng'ombe:- Hivi unajua baadhi ya wafugaji hawafuati masharti pindi ng'ombe wanapokuwa kwenye dozi? Serikali imewahi kujishughulisha kufuatilia ubora wa maziwa yanayoingia sokoni kila siku?

  (iii) Vyakula - Samaki:- Ni wazi kuwa baadhi ya wavuvi hutumia sumu kwenye uvuvi wao na hata usafirishaji na uhifadhi wa samaki haukidhi viwango. Je, serikali inajishughulisha kwa hilo?

  (iv) Vyakula - Nguruwe:- Kama ilivyo kwa nyama ya kuku, je, ni maelfu ya watanzania wangapi wanakula nguruwe ambao hawana ubora kiafya? Serikali inajali?

  (vi) Vyakula - nafaka:- Hivi unajua mbolea na madawa ya kilimo yakitumiwa bila kuzingatia viwango athari zake zinabaki hata kwenye vyakula vitokanavyo na mazao hayo - tena hapo ndio kansa imelala; fikiria DDT, n.k; Je serikali inajali kupima,kwa mfano unga unaosagwa pale Manzese na maharage yanayouzwa pale Tandale na kwingineko kama yana ubora kiafya?

  (v) Mfumo wa maisha - moshi wa magari:- Serikali yetu inajali kuhakikisha kwa mfano uchafuzi wa anga hauzidi viwango vianvyotakiwa? Moshi wa magari ni kansa tupu ile!

  (vi) Madawa ya binadamu:- Serikali inao udhibiti inavyotakiwa kwamba madawa yanayotumika nchini yana viwango vinavyotakiwa na yanatumika kama inavyotakiwa na kwa wakati?

  (vii) Vyakula vya viwandani:- Serikali inadhibiti kikamilifu vyakula vinavyozalishwa viwandani na je wananchi wanazingatia matumizi yake inavyostahili? Expiry dates, n.k. Hapo pia kansa imelala.

  (viii) Mifumo ya maisha - ulevi:- Serikali inadhibiti mifumo mbali mbali ya maisha kwa wananchi wake hasa kwenye suala la ulevi? Fikiria ni watu wangapi wamepata kansa kutokana na ulevi ikiwapo matumizi ya gongo, sigara, n.k.

  (ix) ... n.k., ... n.k. orodha ingeweza kuwa ndefu kadiri uanvyotaka.

  Kwa wenzetu Ulaya huwezi ukazalisha mavitu yako huko halafu ukalisha wananchi bila ukaguzi na udhibiti wa serikali makini. Labda ndio maana wenzetu hata "life expectancy" zao ni zaidi ya 80! Hapa kwetu nasikia tuko 46!

  Hivyo, msururu unaoonekana kwa Babu, kwa sehemu kubwa, ni matokeo ya kupuuzia hayo yaliyoorodheshwa hapo juu. Vinginevyo, tatizo lisengekuwa kubwa kama linavyoonekana hivyo pengine Babu leo hii asingekuwa na kazi ya kufanya. Kwa ufupi athari za dawa ya Babu, kama zitakuwepo, ni ndogo mno kulinganisha na athari tunazokutana nazo kwenye maisha yetu ya kila siku. Kitaalamu tungeweza kusema ni "negligible".

  Tafakari na chukua hatua!
   
 5. Babkey

  Babkey JF-Expert Member

  #5
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 10, 2010
  Messages: 4,256
  Likes Received: 2,079
  Trophy Points: 280
  Du! Ni dhaifu kuliko somalia!?
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Mar 14, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,789
  Trophy Points: 280
  unamaana waliokunywa wote wanaweza kusepa kwa sir GOD kwa wakati mmoja?
  Na nina uhakika hakuna atakayejiuzulu ati.
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,707
  Trophy Points: 280
  Ni dhaifu kuliko hata Somalia?
   
 8. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #8
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Kutokana na hoja tajwa hapo juu, ipo wazi kuwa serikali yetu ni dhaifu kuliko serikali zote duniani.
   
 9. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #9
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Uko sahihi mkubwa!! 100%
   
 10. N

  Nonda JF-Expert Member

  #10
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu.
  Ujumbe umefika ila nafikiri kichwa cha habari cha mada yako hakikukaa sawa.
  Kwa kawaida serikali dhaifu huanguka, huondoshwa kirahisi sana.
  sasa hii ya JK au serikali ya CCM si dhaifu.

  Usahihi ni kuwa utendaji wa serikali ni mbovu una mapungufu mengi..lakini serikali yenyewe si dhaifu. wanatenda walitakalo bila kupingwa. kwa hiyo wayafanyayo si kwa bahati mbaya..ndio style yao ya kuongoza..kama tunaweza kusema huko ndio kuongoza.

  Wananchi wa TZ ndio dhaifu kupita wananchi wa nchi yoyote duniani.Ungesema hivi basi tungekubaliana 100% kwa mia.
   
 11. Mzuzu

  Mzuzu JF-Expert Member

  #11
  Mar 14, 2011
  Joined: Jul 11, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Kwani Somalia kuna serikali siku hizi? Tangu lini?
   
 12. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #12
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  si kweli ni uzushi huu.
   
 13. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #13
  Mar 14, 2011
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri wewe ndiye mdhaifu kuliko wote duniani kwa kigezo changu mimi kama ulivyotumia kigezo chako kwa kikwete. Huko ni kuongeza chumvi pasipo sababu.
   
 14. The Analyst

  The Analyst JF-Expert Member

  #14
  Mar 14, 2011
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 464
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  That's one of the best replies I've ever read. Keep it up Ndugu yangu! JF itanufaika sana kama members wengi tutachukua muda kujibu au kujadili hoja za msingi kwa namna yako. Congrats!
   
 15. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #15
  Mar 14, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,072
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  ni kwa sababu yeye mwenyewe pia ni mdhaifu
   
 16. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #16
  Mar 14, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Acheni ujuha nyie!!! Kwani serikali zote duniani hufanya utafiti wa dawa zote za mitishamba ambazo zinatumiwa na traditional healers? Sisi kule kwetu kuna mganga anaitwa Tagalu, huyu bwana huweza kuchemsha vichwa vya nyoka na kuvitumia kama dawa. Je ni serikali gani inayoweza kutathimini kujua kwamba vile vichwa vya Nyoka ni salama?

  Kijijini kwenu kuna waganga wangapi wa jadi? Mizizi yote wanayotumia kutibia inapimwa? Hakuna serikali hata moja duniani ambayo huweza kufanyia utafiti dawa zote za kienyeji. Na sababu ya msingi ya kushindwa kufanya hivyo ni kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba vitu hivyo vinavyotumiwa na waganga wa jadi, ni dawa. Vingi vinatibu kwa imani!! Kwa mfano, mkemia mkuu anawezaje kutafiti ufanyaji kazi wa hirizi? Kuna watu wanamezeshwa mdomo(beak) wa tai, je mkemia mkuu anawezaje kuthibitisha kwamba mdomo wa tai ni dawa? Ni mkemia gani anayeweza kuthibitisha kwamba mkia wa simba unatibu?

  Angalieni hoja za kuilaumu serikali nanyi!!! Halafu siyo hekima kabisa kusema serikali ya Kikwete ndiyo dhaifu kupita zote duniani kwa kuwa eti imeshindwa kuingilia masuala ya imani! Kwa kusema hivyo ni kama kumtuma kikwete kujishughulisha na mambo yote yakiwemo ya ushirikina na imani juu ya Mungu. Kuna mkemia anayeweza kuthibitisha kwamba kuna Mungu?
   
 17. C

  CHESEA INGINE Senior Member

  #17
  Mar 14, 2011
  Joined: Nov 7, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Dudus! Umeiweka vizuri mno! Hongera na asante! Hakuna cha kuongeza!
   
 18. U

  Uswe JF-Expert Member

  #18
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,201
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  naunga mkono hoja
   
 19. M

  Membensamba Senior Member

  #19
  Mar 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Haya ndiyo matokeo ya serikali isiyotokana na watu na isiyokuwepo kwa ajili ya watu. Viongozi wake wapo kwa ajili ya maslahi yao binafsi, na hivyo hawana ile "sense of responsibility" wanaendesha dola kama kuendesha kioski binafsi tu. Kukosekana kwa uzalendo kwa viongozi kumeitumbukiza nchi mahali pa aibu kwenye maswala mengi sana, na kama hali hii ikiendelea huko tuendapo hakutabiriki.
   
 20. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #20
  Mar 15, 2011
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 9,003
  Likes Received: 585
  Trophy Points: 280
  jamani mbona nasikia hata UNCLE mwenyewe ameenda kunywa kikombe cha juice ya babu??
   
Loading...