Serikali ya Kikwete isiyaendekeze makampuni ya nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Kikwete isiyaendekeze makampuni ya nje

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Synthesizer, Jun 14, 2012.

 1. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #1
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Kilio changu siku zote ni jinsi serikali ya Kikwete - na hata zaidi iliyopita ya Mkapa, zimekuwa zikiyaendekeza makampuni ya kutoka nje. Maeneo matatu yanahusika sana;

  - Udanganyifu mkubwa wa mapato na kuikosesha serikali mabilioni ya fedha za kodi
  - Uajiri wa wafanyakazi wa nje kwa nafasi ambazo zinaweza kujazwa na Watanzania walio na sifa stahili
  - Unyanyasaji, ubaguzi wa rangi na mishahara na marupurupu (benefits) yasio ya haki kwa wafanyakazi Watanzania

  Japo tunapenda wawekezaji wa nje, lakini tumekuwa tukiwaendekeza sana katika mambo hayo ya msingi matatu. Yaani natamani angalau wangenipa nisimamie regulatory framework ya makampuni ya nje japo kwa miaka miwili tu! Wanatunyanyasa sana katika nchi yetu wenyewe.

  Kwa udanganyifu wa mapato kwa mfano, kitu gani kinatuzuia kuwa na sheria ya penalty ya zaidi ya asilimia 50% ya mapato ya kipindi cha miaka mitatu iliyopita? Suala ni kuwa na sheria ambayo mtu anajiuliza mara mia kabla hajadanganya, na jibu analopata ni kwamba usithubutu kudanganya.
   
 2. m

  mamajack JF-Expert Member

  #2
  Jun 14, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 1,162
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  wamegeuza hii nchi kuwa shamba la bibi,kila kitu ni chetu,mpaka mitaji wanakopeshwa na mabenki ya hapa kwetu,shukurani yao ni manyanyaso kwa wa tz.inauma sana.
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mkuu sio kwamba wanadanganya kwa bahati mbaya ni makusudi na kuna wakubwa wanalamba iyo ambayo haijaenda serikalini.
  Kuna kampuni wakati inakuja Tz kwa mara ya kwanza walitaka lipa kwa dola min dola 500 kwa mwezi kuna mdosi akawaambia mbola 300,000tshs kwa kuanzia sio mbaya!Mbaya zaidi akadaka iyo difference faster.
   
 4. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #4
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Ukiweka sheria kali, hata kama mtu akitaka kuwadanganya wataogopa kumsikiliza. Unakumbuka Nyerere aliwahi kumweka ndani muwekezaji mzungu aliesema amewaweka watanzania mfukoni? Nyerere akasema ana mfuko mkubwa kiasi gani cha kutuweka wote tukaenea humo? Alimuweka ndani, pamoja na yule mtanzania waziri wa sheria aliyekuwa akimtumia akawekwa ndani na kuchapwa viboko kumi na mbili akiingia gerezani, kumi na mbili akitoka - akamwonyeshe makalio yaliyoiva mkewe!

  Hivi karibuni, Waziri Mkuu wa Ethiopia, Zenawi, alimfunga miaka mitano jela rafiki yake wa karibu ambaye walikuwa naye msituni na alikuwa best man wake katika harusi kwa kosa la kukwepa kodi. Wa Ethiopia walipata ujumbe, kwamba kama raisi amemfunga rafiki yake wa karibu jela, fikiria akikukamata wewe mtu baki unakula rushwa au kukwepa kodi! Ethiopia bwana imenyoka na uchumi wake unakua kwa kasi inayoishangaza dunia!

  Sasa siku Watanzania wakisikia JK kamfunga rafiki au mtoto wake jela kwa kosa la rushwa au ufisadi, nadhani ujumbe utafika!
   
 5. F

  Fofader JF-Expert Member

  #5
  Jun 14, 2012
  Joined: Sep 28, 2011
  Messages: 838
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 45
  Nimeipenda synthesizer. Uko juu.
   
 6. F

  Froida JF-Expert Member

  #6
  Jun 14, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Huyu Raisi akiondoka madarakani kutakuwa na ugomvi mkubwa wa ajabu sasa hivi kila kitu anakitupa kwa wawekezaji haangalii mbele yatakayo tukuta si gesi,mafuta,uranium,makaa ya mawe na kila kitu siku hizi kama vile amerogwa nina hofu kubwa na jinsi anavyofanya mambo ya ajabu ajabu
   
 7. Synthesizer

  Synthesizer JF-Expert Member

  #7
  Jun 14, 2012
  Joined: Feb 15, 2010
  Messages: 4,334
  Likes Received: 3,130
  Trophy Points: 280
  Mkuu, ahsante sana. Kuna mambo bwana yanafanyika nchini yananiumiza sana, lakini hili la kudhalilishwa na kuibiwa na wageni kwangu mimi halikubaliki hata kidogo. Niliwahi kuwa kwenye mikutano nikiwa naishi nchi nyingine, na bila kujua mie ni Mtanzania jamaa wakawa wanatoa mifano ya kutubeza sana. Yaani walikuwa wanaongea kama vile sie Watanzania ni namba moja duniani kwa ulofa (gullible).
   
 8. s

  sanjo JF-Expert Member

  #8
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Hayo Mabenki yanawapa kwa kutumia ardhi waliyopewa na Tanzania Investment Centre! Kweli Tanzania imefanywa shamba la bibi.
   
 9. s

  sanjo JF-Expert Member

  #9
  Jun 14, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 943
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Na hii dharau inakorozwa na voingozi legelege ambao wako tayari kusaini mikataba mibovu kwa sababu ya kitu kidogo kama alivyofanya Chifu Mangungo enzi za kuja ukoloni wa Kijerumani.
   
Loading...