Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,883
Kitendo cha kongozi mwandamizi wa juu kutoka serikali ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Kikwete na Chama cha mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli kwenda kumfanyia kampeni za urais mmoja wa wagombea huko Kenya ni jambo ambalo halikubaliki kimataifa na mahusiano baina ya nchi na nchi, na kwa namna ya uwazi ni kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.
Iwe kwamba alialikwa binafsi au laa, taswira inayojitokeza ni Waziri wa Serikali ya Tanzania kufunga safari kwenda Kenya kumfanyia kampeni za urais mmoja wa wagombea kitu amacho ni kinyume cha taratibu za mahusiano ya kisiasa za kimataifa. Jambo kama hilo huwa watu wako makini sana hata kulitolea kauli ingawa kila mmoja binafsi huwa na mmoja anayemwunga mkono, kinachofanyika ni kumwunga mkono baada ya uchaguzi yule atakayechaguliwa na wananchi wa Kenya.
Kwa vyo vyote katika hili serikali ya Kikwete imeteleza na imejidhalilisha sana.