Serikali ya kikwete imejidhalilisha kufanya kampeni za urais Kenya

Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
11,889
Points
1,250
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
11,889 1,250

Kitendo cha kongozi mwandamizi wa juu kutoka serikali ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Kikwete na Chama cha mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli kwenda kumfanyia kampeni za urais mmoja wa wagombea huko Kenya ni jambo ambalo halikubaliki kimataifa na mahusiano baina ya nchi na nchi, na kwa namna ya uwazi ni kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Iwe kwamba alialikwa binafsi au laa, taswira inayojitokeza ni Waziri wa Serikali ya Tanzania kufunga safari kwenda Kenya kumfanyia kampeni za urais mmoja wa wagombea kitu amacho ni kinyume cha taratibu za mahusiano ya kisiasa za kimataifa. Jambo kama hilo huwa watu wako makini sana hata kulitolea kauli ingawa kila mmoja binafsi huwa na mmoja anayemwunga mkono, kinachofanyika ni kumwunga mkono baada ya uchaguzi yule atakayechaguliwa na wananchi wa Kenya.

Kwa vyo vyote katika hili serikali ya Kikwete imeteleza na imejidhalilisha sana.
 
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
3,090
Points
1,225
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
3,090 1,225
Siasa za maji taka zinapovuka mpaka unategemea nini? Hivi kama huyo mpendwa wao ingawa ni maarufu sana Kenya hatashinda uhusiano wetu utakuwaje? Ingawa ni haki ya wanasiasa kutembeleana hata kusaidiana si wazi wazi namna hii. Huenda kuna tusichojua ambacho kiliwapa jeuri ya kufanya madudu haya. Ila ukweli ni aibu na tishio huko tuendako. Waombe Mungu Odinga ashinde vinginevyo kutakuwa na mtafaruko kideplomasia huko tuendako. Pia kwa Odinga kuonyesha kuwa ana uhusiano na magamba amejidhalilisha sana. Nilidhani watendaji wakuu wa magamba kama Magufuli wangekuwa wageni wa Kanu na NRM pale kwa Kaguta lakini si ODM. Kweli wanasiasa wakati mwingine hawana tofauti na dada zetu wa mitaani maarufu kama changu kama si wanahara...
 
Eric Cartman

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Messages
6,818
Points
2,000
Eric Cartman

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined May 21, 2009
6,818 2,000
Hivi huwaga haziruhusiwi mbona uchaguzi wa mwisho wa France it was clear "Anglea Merkel" favoured the incumbent government of the time hakutaka kabisa ' Francois Hollande' ashinde. It was not just clear in the two countries but the whole world understood her view point.

Labda waseme kwanini wanafavour hiko chama na ziwe political reasons.
 
Bucktooth Maftaha

Bucktooth Maftaha

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Messages
379
Points
225
Age
32
Bucktooth Maftaha

Bucktooth Maftaha

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2012
379 225
Siasa za maji taka zinapovuka mpaka unategemea nini? Hivi kama huyo mpendwa wao ingawa ni maarufu sana Kenya hatashinda uhusiano wetu utakuwaje? Ingawa ni haki ya wanasiasa kutembeleana hata kusaidiana si wazi wazi namna hii. Huenda kuna tusichojua ambacho kiliwapa jeuri ya kufanya madudu haya. Ila ukweli ni aibu na tishio huko tuendako. Waombe Mungu Odinga ashinde vinginevyo kutakuwa na mtafaruko kideplomasia huko tuendako. Pia kwa Odinga kuonyesha kuwa ana uhusiano na magamba amejidhalilisha sana. Nilidhani watendaji wakuu wa magamba kama Magufuli wangekuwa wageni wa Kanu na NRM pale kwa Kaguta lakini si ODM. Kweli wanasiasa wakati mwingine hawana tofauti na dada zetu wa mitaani maarufu kama changu kama si wanahara...
Unaona kimbelembele chako?

Huchelewi kudakia maada mpya ukiwa kama mchangiaji wa kwanza, tena mwenye hasira aka agression kubwa.

Rambling like a mad man.

Kwa hili credibility yako ipo mashakani.

You got some serious issues dude!
 
Hata kama huyo mgombea ni rafiki yake, hakupaswa kamfanyia kampeni kwa uwazi kutokana na wadhifa alionao Maguvuli serikalini. Shughuli kama hiyo waziri anapovuka mpaka wa nchi anatakiwa kupata ruhusa toka kwa mkuu wake wa serikali yaani Waziri Mkuu au Rais. Kwa utaratibu huo ni dhahiri waliidhinisha safari yake hiyo yenye kuleta utata siku za usoni uhusiano wetu kisiasa na nchi jirani. Kama Pombe hakupata kibali rasmi cha kwenda kufamfanyia Kampeni mgombea wa Kenya basi disciplinary action dhidi ya Maguvuli ichukuliwe vinginevyo ieleweke serikali iliridhia jambo hilo.
 
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Messages
4,550
Points
2,000
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2012
4,550 2,000
Unasemaje la marais wengi akiwepo wa Tz kumtakia ushindi mwema Obama wakati wa kampeni za urais? Hili limekaaje kwa wanaojua sheria za mahusiano za kimataifa?
 
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
11,889
Points
1,250
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
11,889 1,250
Hivi huwaga haziruhusiwi mbona uchaguzi wa mwisho wa France it was clear "Anglea Merkel" favoured the incumbent government of the time hakutaka kabisa ' Francois Hollande' ashinde. It was not just clear in the two countries but the whole world understood her view point.

Labda waseme kwanini wanafavour hiko chama na ziwe political reasons.
Mpaka aliovuka hapa Magufuli ni kufunga safari kwenda ndani ya Kenya kumfanyia kampeni mmoja wa wagombea kwani hilo kidiplomasia ni kosa lisilovumilika. Kuonyesha mapenzi binafsi kwa mgombea fulani ni jambo la kawaida na pengine vigumu kuepukika, ila ubaya pale kuingia ndani ya nchi kufanya kampeni ni jembo geni kabisa.
 
Sikushuhudia bado hilo, labda lilikuwa jambo binafsi kati ya mtu na mgombea, lakini sijashuhudia aliyetia mguu ndani ya Marekani kumfanyia kampeni Obama.
 
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2012
Messages
3,090
Points
1,225
Father of All

Father of All

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2012
3,090 1,225
Leo nina muda wa kutosha. Ukitaka kujua kuwa mimi si maji taka kama wewe angalia Comments za mtoa mada aliponi-quote ulinganishe na utumbo wako. Nijuacho ni kwamba imekuingia hadi umepagawa,. We kafanye kazi yako ya uganga wa kienyeji na ujuzi wako ni mambo ya ngono tu siyo kufikiri na kuja na majibu. Mijitu yenye akili za hovyo utaijua. Hoja hujibiwa kwa hoja si mitusi. Kama nilivyokuahidi ukifire nami nafire back. Nimefurahi kuwa imekuingia na umepagawa. Go ahead bring more vitriol I am ready for whatever as father of all especially in thinking.
Unaona kimbelembele chako?

Huchelewi kudakia maada mpya ukiwa kama mchangiaji wa kwanza, tena mwenye hasira aka agression kubwa.

Rambling like a mad man.

Kwa hili credibility yako ipo mashakani.

You got some serious issues dude!
 
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
86,275
Points
2,000
BAK

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
86,275 2,000
Na huyu fisadi Magufuli naye eti ni mmoja wa Marais watarajiwa toka magamba 2015!!!!
 
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined
Jan 26, 2012
Messages
4,550
Points
2,000
ITEGAMATWI

ITEGAMATWI

JF-Expert Member
Joined Jan 26, 2012
4,550 2,000
Sikushuhudia bado hilo, labda lilikuwa jambo binafsi kati ya mtu na mgombea, lakini sijashuhudia aliyetia mguu ndani ya Marekani kumfanyia kampeni Obama.

Kwani hili kisheria za siasa za kimataifa likoje?
 
Eric Cartman

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2009
Messages
6,818
Points
2,000
Eric Cartman

Eric Cartman

JF-Expert Member
Joined May 21, 2009
6,818 2,000
Mpaka aliovuka hapa Magufuli ni kufunga safari kwenda ndani ya Kenya kumfanyia kampeni mmoja wa wagombea kwani hilo kidiplomasia ni kosa lisilovumilika. Kuonyesha mapenzi binafsi kwa mgombea fulani ni jambo la kawaida na pengine vigumu kuepukika, ila ubaya pale kuingia ndani ya nchi kufanya kampeni ni jembo geni kabisa.
Inategemea, kama alifika kwenye political rallies za huyo bwana that is not accepted. Either way hupo sawa alikosea, lakini kitu ambacho nilipinga ni kusema hairuhusiwi kutoa support kwa nchi za nje.

Hatupo zama za ukombozi wa afrika, hila kumbuka kuna nchi zinatuma mpaka majeshi kutoa support ugenini kwa ajili ya mtu wao mifano hii wazi russia hawafichi kumpelekea silaha syria. Na wala Turkey na nuksi wengine hawafichi kuchoswa na Syria.

Tatizo naloliona kubwa ni kutokutuelewesha what do they see in that man kisiasa za EA mpaka bwana mkubwa amnadi kwanza hata kama alikuwa na idhini ya serikali au kimbelembele tu.
 
S

Seif al Islam

JF-Expert Member
Joined
Nov 14, 2011
Messages
2,158
Points
1,250
S

Seif al Islam

JF-Expert Member
Joined Nov 14, 2011
2,158 1,250
juzi tuu hapa si alienda china usiku wa manane kuweka mambo sawa.kwani huko hakudhalilika?
 
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2006
Messages
25,231
Points
2,000
Nicholas

Nicholas

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2006
25,231 2,000

Kitendo cha kongozi mwandamizi wa juu kutoka serikali ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Kikwete na Chama cha mapinduzi Dr. John Pombe Magufuli kwenda kumfanyia kampeni za urais mmoja wa wagombea huko Kenya ni jambo ambalo halikubaliki kimataifa na mahusiano baina ya nchi na nchi, na kwa namna ya uwazi ni kuingilia mambo ya ndani ya nchi nyingine.

Iwe kwamba alialikwa binafsi au laa, taswira inayojitokeza ni Waziri wa Serikali ya Tanzania kufunga safari kwenda Kenya kumfanyia kampeni za urais mmoja wa wagombea kitu amacho ni kinyume cha taratibu za mahusiano ya kisiasa za kimataifa. Jambo kama hilo huwa watu wako makini sana hata kulitolea kauli ingawa kila mmoja binafsi huwa na mmoja anayemwunga mkono, kinachofanyika ni kumwunga mkono baada ya uchaguzi yule atakayechaguliwa na wananchi wa Kenya.

Kwa vyo vyote katika hili serikali ya Kikwete imeteleza na imejidhalilisha sana.
CCM ni wajinga sana hakuna mwenye uwezo wa kuona hilo achilia mbali elewa kinachoelezwa hapa.Ki ukweli tumeingilia vibaya sana mambo ya nchi ya watu.Tulipaswa watakia uchaguzi mwema na wa amani, huku wakiwaasa wakenya wachague kiongozi bora.FULL STOP
 
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2011
Messages
9,939
Points
2,000
dudus

dudus

JF-Expert Member
Joined Feb 28, 2011
9,939 2,000
Hivi huwaga haziruhusiwi mbona uchaguzi wa mwisho wa France it was clear "Anglea Merkel" favoured the incumbent government of the time hakutaka kabisa ' Francois Hollande' ashinde. It was not just clear in the two countries but the whole world understood her view point.

Labda waseme kwanini wanafavour hiko chama na ziwe political reasons.

Angela Merkel alisimama jukwaani huko France kumkampenia huyo "mtu wake"? Kisichoeleweka kwenye sakata la Magufuli huko Kenya ni nini? Mbona tunapenda sana kupindisha pindisha mambo badala ya kuuona ukweli halisi na kuukiri?
 
Indian

Indian

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2012
Messages
824
Points
1,000
Age
38
Indian

Indian

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2012
824 1,000
Hapa kidiplomasia tayari tumeshaharibu, tujiandae kwa lolote litakalo tokea, mambo ya siasa na nchi zetu za kiafrika hamna siasa za kidemokrasi kwaiyo magufuli akishindwa kuingia ikulu nchini kenya itakua balaa.
 
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
11,889
Points
1,250
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
11,889 1,250
Kwani hili kisheria za siasa za kimataifa likoje?
Sheria za kimataifa haziruhusu nchi nyingine kuingilia shughuli za uchaguzi katika nchi husika. Pale tatizo litakapotokea kuna chombo cha umoja wa mataifa kitakachochukua jukumu baadha ya nchi wanachama kuridhia hasa yatokeapo machafuko.
 
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
11,889
Points
1,250
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
11,889 1,250
Inategemea, kama alifika kwenye political rallies za huyo bwana that is not accepted. Either way hupo sawa alikosea, lakini kitu ambacho nilipinga ni kusema hairuhusiwi kutoa support kwa nchi za nje.

Hatupo zama za ukombozi wa afrika, hila kumbuka kuna nchi zinatuma mpaka majeshi kutoa support ugenini kwa ajili ya mtu wao mifano hii wazi russia hawafichi kumpelekea silaha syria. Na wala Turkey na nuksi wengine hawafichi kuchoswa na Syria.

Tatizo naloliona kubwa ni kutokutuelewesha what do they see in that man kisiasa za EA mpaka bwana mkubwa amnadi kwanza hata kama alikuwa na idhini ya serikali au kimbelembele tu.
Dhahiri jambo hili lipo katika kusaidia baadhi ya nchi na imetokea Tanzania kuwa kinara na makao ya ukombozi barani Afrika enzi za wapigania uhuru. Kilichokuwa kinafanyika ni kuwakaribisha wahusika kisiasa kwa kuwahifadhi hata sheria za kimataifa huruhusu.

Kuunga mkono kikundi fulani ni jambo ambalo huwa halifanywi wazi wazi wakati ndani ya nchi kuna makundi kadhaa yenye kupigania haki zao, na wenye wajibu wa kuridhia chama chenye kuwavutia ni wapiga kura wake.

Jambo hili unaweza kuona hata ndani ya nchi makundi yenye kufanya kazi za kitaifa zaidi kama askari, wanasheria nk hawaruhusiwi kuwa wanachama wa chama fulani wala kutolea kauli ya kukipigia kampeni chama fulani, iweje serikali ya nchi itume waziri wake kwenda kumfanyia kamoeni mgombea urais ndani ya nchi husika?

Hata vyombo vya habari hufanya uchambuzi wa kina na pengine hata kutoa mapendekezo ya kuonyesha mwenye kuleta mvuto zaidi wa kisiasa au mwenye hoja zenye mvuto zaidi. Haya hufanya po pote ulimwenguni.

Hili la Bwana Magufuli kufunga safari hadi Kenya kumnadi mmoja wa ugombea urais wakati akiwa kiongozi mwanamizi ndani ya baraza la mawaziri la Tanzania ni kasoro isiyovumika, na ninachoshangaa serikali inakwepa kulitolea kauli jambo hili ambalo limeonekana kukera wengi.
 
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2010
Messages
11,889
Points
1,250
Candid Scope

Candid Scope

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2010
11,889 1,250
Hapa kidiplomasia tayari tumeshaharibu, tujiandae kwa lolote litakalo tokea, mambo ya siasa na nchi zetu za kiafrika hamna siasa za kidemokrasi kwaiyo magufuli akishindwa kuingia ikulu nchini kenya itakua balaa.
Serikali ilitakiwa kutolea ufafanuzi na kuweka kinga yake katika jambo hili kama Magufuli alifanya jambo hilo yeye binafsi bila serikali kuridhia. Jambo la kushangaza waziri hawezi kutoka nje ya mipaka ya nchi bila ruhusa ya waziri mkuu au Rais. Hali halisi inavyoonekana alitumwa na serikali kwa sababu serikali haijajenga utetezi wake katika jambo hili, na kukaa kimya ndiyo kudhihirisha kinachoendelea.

Magufuli anaonekana asivyo na busara kabisa katika kupima mambo nikikumbuka kauli na matusi aliyowatukana wakazi wa Kigamboni na kujenga utetezi wa kutoomba radhi. Magufuli amepwaya katika kutumia ubongo wake na hivyo kuonekana hekima na busara vilivyo mbali kabisa naye. Huyu ndiye anaweza kuwa mmoja wapo wa candidate wa CCM wa urais?
 
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2011
Messages
31,005
Points
2,000
BADILI TABIA

BADILI TABIA

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2011
31,005 2,000
Na huyu fisadi Magufuli naye eti ni mmoja wa Marais watarajiwa toka magamba 2015!!!!
hilo si ndo 'jembe' lenu watanzania? Heheheheh mnasikitisha sana......
 
Forum statistics

Threads 1,283,765
Members 493,810
Posts 30,800,166
Top