Serikali ya Kikwete hoi kifedha: Wafanyakazi wakosa mishahara

Phillemon Mikael

Platinum Member
Nov 5, 2006
10,529
8,614
Katika kinachooonekana kuwa serikali ipo hoi kifedha kwa mara ya kwanza tangu tatizo la kuchelewesha mishahara kuwa historia nchi hii ..watumishi wa uma wameanza kupigwa kalenda kupewa mishahara katika tukio la karibuni hata polisi walilimwa barua za uvumilivu ....zikiwataka wawe wavumilivu kwa mishahara kuchelewa ...

Hali hiyo imeendelea kuwa tete hata sasa ambapo mishahara ya watumishi wa umma nayo imeanza kuchelewa....nadhani kwa kuwa humu watumishi tupo....tunaweza kuchangia vema hoja hii...
 
JK atawapaje wafanyakazi mishahara kwa muda muafaka wakati wanafanya kampeni kuitikia wito wake wa kukataa kura za wafanyakazi? Wafanyakazi watamnyima JK kura za urais naye anawaadhibu wafanyakazi kwa kuwacheleweshea mishahara.
 
sijuhi kama kutakuwa na mfanyakazi mjinga wa kuweza kumpigiakura kikwete,
KURA AMBAZO NINAUHAKIKA ATAZIKOSA KUTOKA NDANI YA CCM NI ZA
1) mWAKYEMBE NA FAMILIA YAKE,
2)SITTA NA FAMILIA YAKE,
3)MAGUFULI NA FAMILIA YAKE,
4)MWANDOSYA NA FAMILA YAKE,
4)SELELII NA FAMILA YAKE,
.
.
.
.
.
.
99) WARIOBA
100) SALIM A SALIM
 
yangu na familia yangu pamoja na mtu yeyote aliyeko kwenye payroll yangu
 
Me yangu macho kwa hali niiyonayo naona kura za Wafanyakazi ni za muhimu.
 
sijuhi kama kutakuwa na mfanyakazi mjinga wa kuweza kumpigiakura kikwete,
KURA AMBAZO NINAUHAKIKA ATAZIKOSA KUTOKA NDANI YA CCM NI ZA
1) mWAKYEMBE NA FAMILIA YAKE,
2)SITTA NA FAMILIA YAKE,
3)MAGUFULI NA FAMILIA YAKE,
4)MWANDOSYA NA FAMILA YAKE,
4)SELELII NA FAMILA YAKE,
.
.
.
.
.
.
99) WARIOBA
100) SALIM A SALIM

100. Wale wanafunzi wa UDOM, walioko mazoezini mkoani MWANZA.
 
Tumezoea. kipindi chote cha uchaguzi hili tatizo huwa linajitokeza. Na si kwa uchaguzi huu tu hata chaguzi zote zilizopita huko nyuma tangu vyama vingi vianze. Anyway Philemon huenda ukawa umeajiriwa juzi ndo maana hujawahi kuliexperiense hili tatizo. So sio kwa JK tu na wala si chuki na wafanyakazi kama mtanzania anavyotaka kuaminisha watu hapo juu. Ila siliungi mkono, serikali ijipange chaguzi zijazo lisijitokeze tena.
 
Tatizo ni nini kutowapa mishahara yao kwa wakati. Kuna chonzo chochote cha mapato ktk bajeti ya nchi kimebadilika? Na kwa kiwango gani? Kama sivyo basi ujue pesa imehamishiwa kwenye kampeni za 'mwezeshe Kikwete ashinde'
 
Mmesahau na marehemu mwl nyerere na mh kawawa wameapa kutowapigia ccm kabisa huko waliko nikiwemo na mie na familia yangu kama waungana nami sema amen
 
Kiwete atakosa kura nyingi sana kutoka mkoa wa Mbeya, kwani kwa kipindi cha miaka yake mitano madarakani moja ya ajenda zake ilikuwa kuuangamiza kabisa mkoa huo kimaendeleo na amefanikiwa kwa kiasi fulani. Alihakikisha amewapiga rungu wote waliomuunga mkono Mwandosya kwenye uchaguzi wa 2005 na kumbambikiza kibaraka Mwakipesile kama mkuu wa mkoa baada ya kushindwa ubunge. Wananchi wa Mbeya ,hasa wa kutoka Rungwe wameligundua hilo na inaelekea wanaendelea kukabiliana na uchuro huo vilivyo.
 
jamani wakumbuken na ATCL kwenye mishahara nao ni serikali wamechoka kupiga makelele ya njaa
 
Katika kinachooonekana kuwa serikali ipo hoi kifedha kwa mara ya kwanza tangu tatizo la kuchelewesha mishahara kuwa historia nchi hii ..watumishi wa uma wameanza kupigwa kalenda kupewa mishahara katika tukio la karibuni hata polisi walilimwa barua za uvumilivu ....zikiwataka wawe wavumilivu kwa mishahara kuchelewa ...

Hali hiyo imeendelea kuwa tete hata sasa ambapo mishahara ya watumishi wa umma nayo imeanza kuchelewa....nadhani kwa kuwa humu watumishi tupo....tunaweza kuchangia vema hoja hii...

Tunaomba Chanzo cha habari Tafadhali.
 
Tunaomba Chanzo cha habari Tafadhali.

Phillemon Mikael wa JF ndio chanzo................na huo ndio ukweli wenyewe............

Kuna wakati mishahara ilichelewa idara fulani kwakuwa Mkulu.........anasafiri..........damn
 
Labda wanazungusha pesa kwenye stock exchange ili wapata more money kwa uchaguzi !!!!!!!!kwa nini ichelewe kama sivyo?
Ahaaa zinakuwa NYSE.
 
yangu na familia yangu pamoja na mtu yeyote aliyeko kwenye payroll yangu

Una uhakika na kura yako tu,kuna jamaa Kenya alitaka kuwa diwani familia yake ya watu 12 lakini siku ya uchaguzi alipata kura 6 akafukuza wote nyumbani pamoja na mkewe na watoto
 
Wenzao wanajipunguzia mishahara kutokana mambo yalivyo magumu wao ndio kwaaanza wanajiongezea na kuiba juu.

kama hatujafika bado basi tunapoelekea ni kubaya sana .
 
Back
Top Bottom