Tetesi: Serikali ya Kenya yawafidia wafugaji walioporwa mifugo yao na serikali ya Tanzania .

Habari zilizopo hewani ni kwamba serikali ya watu nchini kenya imeamua kwa moyo wa huruma kuwafidia wafugaji wa nchi hiyo ambao mifugo yao ilikamatwa na kupigwa mnada kwa bei ya kutupa nchini Tanzania .

Mungu ibariki Jamhuri ya watu wa Kenya .
Mmmmmm hiyo mifugo ilikuwa yake au ya familia za wanasiasa wa Kenya? Yule alikuwa mchunga ngombe tu .Kichwa cha habari kisomeke wanasiasa wa Kenya wamiliki ngombe zilizoshikwa Tanzania wawaibia wakenya kodi zao na wajilipa fidia ya ngombe zao walizokuwa wakilisha Tanzania kinyume cha sheria
 
Mmmmmm hiyo mifugo ilikuwa yake au ya familia za wanasiasa wa Kenya? Yule alikuwa mchunga ngombe tu .Kichwa cha habari kisomeke wanasiasa wa Kenya wamiliki ngombe zilizoshikwa Tanzania wawaibia wakenya kodi zao na wajilipa fidia ya ngombe zao.
Sihusiki na hizo porojo zako .
 
Mmmmmm hiyo mifugo ilikuwa yake au ya familia za wanasiasa wa Kenya? Yule alikuwa mchunga ngombe tu .Kichwa cha habari kisomeke wanasiasa wa Kenya wamiliki ngombe zilizoshikwa Tanzania wawaibia wakenya kodi zao na wajilipa fidia ya ngombe zao walizokuwa wakilisha Tanzania kinyume cha sheria
Justify kaka LA sivyo kutakuwa tunachamba kwa majani ya mgomba tu hapo..kwa kweli Yale hayakuwa maamuzi mazuri hata kidogo
 
Nawaonea wivu sana Wakenya .
Usilolijua ni kama usiku wa giza wafugaji wa Kenya mifugo yao inakufa kwa ukame kwa maelfu na ushahidi upo serikali ya Kenya haijawahi wafidia!!!! Wanajifidia wanasiasa wamiliki hizo ngombe hujiulizi swali dogo tu kwa nini mumiliki wa vifaranga mkenya vilivyopigwa moto Tanzania mbona hawajamfidia huyo mkenya mwenzao aliyemuuzia mtanzania? jibu huyo Muuza vifaranga mkenya sio mwanasiasa kule Kenya
 
Kuvuka na mifugo kutoka Taifa moja kwenda lingine ni makosa. Ila tutangulize hekima. Wamasai wana historia ambayo inazidi umri wa mipaka ya wakoloni. Tusijejikuta tunatengeneza tatizo kubwa badala ya kulimaliza lililopo. Nafikiri waanze kwanza na elimu baadae ndio sheria.
Ujinga ni adui mkubwa tuliyenaye tusikae kama haupo. Wanaofanya hivyo sijui kama wanazijua hizi sheria.
 
Hii ni KUFURU. Tafadhali Yehodaya mwombe Mungu wako msamaha. Kufuru hii adhabu yake ni KIFO.
Shetani alikuwa Jirani wa Mungu mbinguni au hilo hujui? Akaleta za kuleta akajikuta jehanamu na hajasamehewa hadi Leo anakiona cha mtema kuni.Yuda iskariote alikuwa jirani wa Yesu alipoleta za kuleta unajua kilichomkuta? Ujirani sio kufanyiana ushetani tafadhali usinilazimishe kuamini unachoamini .Jirani shetani anatakiwa ashughulikiwe kama baba yake shetani alivyoshughulikiwa mbinguni kwa imani yangu
 
Mkuu vile vifaranga aliepata hasara ni mtanzania na si mkenya Mtanzania alinunua vifaranga kwa mkenya na mtanzania kakamatwa na hivyo vifaranga kwa kuvipitisha mpakani kinyume cha sheria sasa mkenya amepataje hasara hapo?
Hakununua alikopa
 
12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom