Serikali ya Kenya yafilisika, yachapisha pesa toka CBK

joto la jiwe

JF-Expert Member
Sep 4, 2017
26,117
46,613


Serikali ‘yachapisha’ pesa mpya kufufua uchumi​


NA FAUSTINE NGILA


SERIKALI ‘imechapisha’ fedha mpya za Sh15 bilioni katika kipindi cha siku saba kufikia Septemba 25, kulingana na takwimu kutoka Benki Kuu ya Kenya (CBK).

Serikali ilipokea Sh46 bilioni kama mkopo wa muda kutoka CBK ambazo ni ongezeko kutoka Sh31.3 bilioni wiki iliyotangulia.
Fedha hizo ndizo mkopo wa juu zaidi ambao serikali imechukua kutoka CBK kwa wiki moja, na ulijiri katika kipindi ambapo Hazina Kuu inashinikizwa kulipa riba.

Katika mpango wa aina hiyo, CBK kwa kawaida hutuma fedha kwa akaunti za serikali, mchakato ambao unaitwa ‘kuchapisha pesa’.

Lakini ikiwa pesa nyingi zimechapishwa, wananchi wanaweza kudai bidhaa nyingi sokoni, na iwapo kampuni zinaendelea kuwa na kiasi sawa cha bidhaa, basi zitalazimika kupandisha bei.

Hazina Kuu imekabiliwa na changamoto ya uhaba wa fedha kutokana na athari za virusi vya corona, na kulazimika kuomba pesa nyingi kutoka kwa soko la humu nchini kujairbu kuokoa uchumi.

Kufikia mwishoni mwa mwaka wa kifedha wa 2019/2020, serikali ilikuwa imeomba Sh47 bilioni.

Chanzo: Taifa Leo

========

MY TAKE: Hii ni hali ya hatari sana tutegee "inflation rate" kuongezeka na gharama za maisha kuwa juu sana. Kama hali isipotengemaa basi serikali itapoteza udhibiti wa uchumi wa nchi kitu kinachoweza kusababisha watu kuingia mabarabarani. Tuzidi kuwaombea majirani.
 
Kwahiyo ukichapisha pesa ndo unafufua uchumi!? Watanzania hivi nani aliyeturoga!?
 
Hawa opra news ni wa kupuuzwa siyo reliable source wana habari fake sana. Kwanza habari yenyewe haina hata maelezo.
Huo ni mtazamo wako hakuna wa kukupinga, ila kuna wenyewe mtazamo tofauti na wewe, wacha maisha yaendelee.
 
Sidhani kama una hata "idea" ya kuelewa kinachozunguzwa, ninakushauri ubaki kuwa mtazamaji unaweza kujifunza kitu kipya, dalili zote zinaonyesha huelewi mambo haya ya fedha na uchumi
Zilikua mbinu zinazofanikiwa ipasavyo zamani kutoa noti mpya Ili ufufue uchumi maana hii ilisaidia hata watu waliohodhi pesa ndani wapeleke bank kwa karne hii ya Sasa BADO hua naiona Kama mbinu dhaifu Sana na ufanisi wake Ni mdogo mno.
 
Zilikua mbinu zinazofanikiwa ipasavyo zamani kutoa noti mpya Ili ufufue uchumi maana hii ilisaidia hata watu waliohodhi pesa ndani wapeleke bank kwa karne hii ya Sasa BADO hua naiona Kama mbinu dhaifu Sana na ufanisi wake Ni mdogo mno.
Tofautisha kati ya kubadilisha pesa na kuchapisha pesa, hapo ndio unajichanganya.
 
Huo ni mtazamo wako hakuna wa kukupinga, ila kuna wenyewe mtazamo tofauti na wewe, wacha maisha yaendelee.
Hata kwa akili ya kuvuka barabara, lini chombo reliable kikaweka kichwa cha habari na picha ya gavana wa bank kikaishia hapo bila habari yenyewe? Hawa Opera news wameandika habari nyingi za uongo hata kuhusu Tanzania.
 
Hata kwa akili ya kuvuka barabara, lini chombo reliable kikaweka kichwa cha habari na picha ya gavana wa bank kikaishia hapo bila habari yenyewe? Hawa Opera news wameandika habari nyingi za uongo hata kuhusu Tanzania.
Ukinyamza hakuna atakeyejua uwezo wako wa kufikiria ni mkubwa kiasi gani. Kaka tulia unajidhalilisha bure. Wenzako wote wameweza kusoma habari nzima hapo imeandikwa kwa urefu na mapana.

Watu wanakushangaa unaposema wametoa pia ya Governor pekee na headings, uwe unauliza ili watu wakusaidie kama umeshindwa kuiona habari yote badala ya kujifanya mjuaji.
 
Ukinyamza hakuna atakeyejua uwezo wako wa kufikiria ni mkubwa kiasi gani. Kaka tulia unajidhalilisha bure. Wenzako wote wameweza kusoma habari nzima hapo imeandikwa kwa urefu na mapana.

Watu wanakushangaa unaposema wametoa pia ya Governor pekee na headings, uwe unauliza ili watu wakusaidie kama umeshindwa kuiona habari yote badala ya kujifanya mjuaji.
Unless PC yangu ina tatizo ila kila nikiifungua naambulia picha na kichwacha habari ngoja nirudi tena even though opera news bado ni wana fake news ila kuna muda hata shetanihutenda jema ngoja nikajaribu tena.
 
Mbna Tanzania tumechapisha pesa mpya Mara kadhaa Hivi ilitusaidia kunyenyua uchumi?
Unachapisha kisha unaziingiza miradi ya mabarabara, viwanda, etc, kisha unazitoa kwenye mzunguko, unabaki ja mabarabara na viwanda lukuki.🤑🤑🤑
 
Unachapisha kisha unaziingiza miradi ya mabarabara,viwanda ,etc,kisha unazitoa kwenye mzunguko,unabaki ja mabarabara na viwanda lukuki...
Mambo yamgekua rahisi hivo Mbna nchi nyingi zenye watawala wenda wazimu na madikteta zingefanya.
 
Dude you do not know economics or finance. The ignorance in your thread is mind boggling. Let me explain, this is normal it is called overdraft. The money is not printed as you think( technically it is called print money), instead CBK(Central Bank Of Kenya) credits treasury account with money, similar to how banks type your loan into a computer and like magic you have money.

By July 2020 GOK had cleared all overdrafts it owed CBK from previous year. every financial year GOK is entitled to $1 billion/kes 112 bilion overdraft from CBK.

Now you may ask why do this?

Unlike many african countries, Kenya's debt is majorly local debt about 54% (kes 3.8 trillion) and about 46%(kes 2.8 trillion) foreign debt, which means to pay interest on treasury bills and bonds( which is how government borrows locally. I know you do not know), GOK can simply tap into the overdraft facility at the CBK and pay off interest owed to Kenyans who have lent it money through bills and bonds. This is because about 54% of Kenya's loans are valued in Kenyan shillings.

The overdraft is charged interest at CBK rate which is lower than bills and bonds .

Modern Money Theory

Debt denominated in your own currency can simply be paid of by overdrafts from the central bank , then you can use taxes and bonds to control inflation and fund infrastructure, not to pay off debts.

Conclusion
You have serious personal problems with your obsession. You always comment on things you do not know and have no knowledge of.
Be more concerned with the commercial loans your government is asking for rather than Kenya borrowing from Kenyans and paying Kenyans.

NB: Hold your breath till Jesus comes!!! Actually your conclusion proves you know nothing about economics or finance.
 
Back
Top Bottom