Serikali ya Kenya yaamuru Wachina wanne waliomchapa Mkenya warudishwe kwao

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
1581657899763.png

Raia wanne wa Uchina waliokamatwa na Mkurugenzi wa idara ya upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) wanatarajiwa kurudishwa kwao baada ya amri iliyotolewa na Waziri wa mambo ya ndani wa Kenya Fred Matiang'i.

Agizo hilo lilisainiwa na Matiang'i Jumatano baada ya mahakama kuruhusu polisi kuwashikilia wachina wanne kwa siku 15 huku uchunguzi ukiendelea juu ya tukio la kumchapa viboko raia wa Kenya aliyekua akifanya kazi katika mgahawa ulioendeshwa na Wachina hao mjini Nairobi.

Raia hao wa Uchina waliotambuliwa kwa majina; Ou Qiang, Deng Hailan, Chang Yueping, na Yu-Ling; walitiwa nguvuni Jumapili baada ya video iliyoonyesha mmoja wa wahudumu wa mgahawa wa wachina akipigwa viboko na mmoja wao katika mgahawa wao kueneo kwenye mitandao ya kijamii.

Katika video hiyo mwanaume wa Kichina alionekana akimpiga viboko Mkenya aliyekua akifanya kazi katika mgahawa unaouza vyakula vya kichina Chez Wou Restaurant katika eneo la Kileleshwa jijini Nairobi.

Iliripotiwa kuwa Mkenya, Simon Oseko, alikua akichapwa viboko kwa kosa la kuchelewa kufika kazini.

Alipigwa viboko viwili na meneja huku wafanyakazi wenzake wakishuhudia kwa mbali.

Oseko aliripoti tukio hilo katika kituo cha polisi. Iliripotiwa kuwa mpishi wa Kichina katika mgahawa huo pia aliwatisha wafanyakazi wengine raia wa Kenya ili wasizungumzie kuhusu mateso wanayopitia katika mgahawa.

Walikamatwa kwa kumiliki vibali vilivyopitwa na wakati vya kuishi nchini Kenya na kufanya kazi nchini humo bila kuwa na vibali vya kazi. Baadhi walikua na vibali vya kutembea Kenya.

Balozi wa Uchina nchini Kenya Wu Peng amesema anaafiki hatua iliyochukuliwa na serikali ya Kenya dhidi ya Wachina hao wanne: ''Serikali ya Uchina na ubalozi wangu unawashauri Wachina binafsi na kampuni zinazowekeza nchini Kenya kufanya kazi kwa faida ya nchi iliyowapokea, na bila shaka kila mara tunawaomba raia wetu hapa kuheshimu sheria za Kenya na kuishi kwa amani na Wakenya, yeyote atakayevunja sheria atapata athari zake, uhusiano wa nchi zetu unategemea sio tu serikali zetu bali watu wa nchi zetu'' alisisitiza balozi Peng mjini Nairobi.

Chanzo: BBC Swahili

Pia Soma: Raia wa China wakamatwa kwa kumcharaza viboko mfanyakazi aliyefika ofisini kwa kuchelewa
 
Siungesema Kenya imeiga mlivowatimua wale wachina wawili ambao waliacha kijiji kizima cha watanzania na manundu baada ya kuwachapa kungfu za kufa mtu. Tena baada ya kuwafanyisha kazi ngumu bila mishahara.
 
Ndio maana tunachekwa sana nchi zetu hizi za dunia ya tatu,why DCI hakufanya uchunguzi wa kina kuhusu madi haya na kama walikuwa wametenda kosa ilikuwa wapelekwe mahakamani sio kuwarudisha kwao!but hii ndio Africa miaka kadhaa iliyopita nchini mwetu wageni wa nchi Fulani walituhumiwa kumlazimisha dada yetu afanye ngono na mbwa,walikamatwa wakawekwa pale oysterbay polisi station na kilichofuatwa tukaambiwa wanarudishwa kwao!sio kwenda kujibu kesi pale Kisutu.
 
Duh! Yaani hivi hivi unarudishwa kwenu huko kwa kirusi cha Makorona, ndio changamoto za kuishi ugenini kwenye nchi ya watu, unatakiwa uwe mkimya bila mbwembwe zozote hata usitake utani utani na wenyeji wala usiwe mgomvi, maana mkizinguana tu, moja kwa moja unafurushwa.

Japo mimi nilipokua mlevi mlevi kwenye bar za Bongo, nilikua na ukorofi fulani halafu full lafudhi ya kikwetu kwenye bar na makelele, tunazinguana na Wabongo kuhusu warembo, lakini nilijitahidi sikukumbana na hatari ya kuswekwa ndani ya kaladinga, maana yaani mapolisi wa Kiafrika wakikukamata, kwanza hata wanaweza wakachana vibali vyako yaani uvurugwe mpaka ukome ubishi.
 
Mbona walishawasilishwa mahakamani, mpo wazembe sana hata kusoma mnashindwa, kazi kubwatuka tu baada ya kusoma kichwa cha habari.
 
Japo mimi nilipokua mlevi Bongo, nilikua na ukorofi fulani halafu full lafudhi ya kikwetu kwenye bar na makelele, tunazinguana na Wabongo kuhusu warembo, lakini nilijitahidi sikukumbana na hatari ya kuswekwa ndani ya kaladinga, maana yaani mapolisi wa Kiafrika wakikukamata, kwanza hata wanaweza wakachana vibali vyako yaani uvurugwe mpaka ukome ubishi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu hivi unajua adhabu ya kimahakama kwa kosa la kumchapa mtu viboko, mimi sijui ila naamini itakuwa ndogo sana pengine ni kulipa faini chini ya 100k, kwangu naona ni vema warudishwe kwao kwanza watakosa mapato pili corona inawasubiri, hiyo ni adhabu kubwa kuliko kumfunga mwezi mmoja kisha anarudi kufanya biashara.
Ndio maana tunachekwa sana nchi zetu hizi za dunia ya tatu,why DCI hakufanya uchunguzi wa kina kuhusu madi haya na kama walikuwa wametenda kosa ilikuwa wapelekwe mahakamani sio kuwarudisha kwao!but hii ndio Africa miaka kadhaa iliyopita nchini mwetu wageni wa nchi Fulani walituhumiwa kumlazimisha dada yetu afanye ngono na mbwa,walikamatwa wakawekwa pale oysterbay polisi station na kilichofuatwa tukaambiwa wanarudishwa kwao!sio kwenda kujibu kesi pale Kisutu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona walishawasilishwa mahakamani, mpo wazembe sana hata kusoma mnashindwa, kazi kubwatuka tu baada ya kusoma kichwa cha habari.
Sorry bro alichomaanisha uyo jamaa ni kwamba walipopelekwa mahakamani hawakufungwa kutokana na kosa ilo kama unavyoona waafrika wenzetu wakikamatwa nchi za nje wanapelekwa mahakamani kwa kufungwa au kunyongwa ila sisi tunawarudisha kwao ndio hukumu yetu
 
Sidhani kama kuna kosa kumfukuza mgeni asiyefaa kuishi kwako.
 
Duh! Yaani hivi hivi unarudishwa kwenu huko kwa kirusi cha Makorona, ndio changamoto za kuishi ugenini kwenye nchi ya watu, unatakiwa uwe mkimya bila mbwembwe zozote hata usitake utani utani na wenyeji wala usiwe mgomvi, maana mkizinguana tu, moja kwa moja unafurushwa.

Japo mimi nilipokua mlevi mlevi kwenye bar za Bongo, nilikua na ukorofi fulani halafu full lafudhi ya kikwetu kwenye bar na makelele, tunazinguana na Wabongo kuhusu warembo, lakini nilijitahidi sikukumbana na hatari ya kuswekwa ndani ya kaladinga, maana yaani mapolisi wa Kiafrika wakikukamata, kwanza hata wanaweza wakachana vibali vyako yaani uvurugwe mpaka ukome ubishi.

Yote sawa, lkn swali linakuja mtu anawezaje kujiamini kiasi hicho mpaka kufikia hatua ya kumchapa viboko mwenyeji? I mean wewe ukienda China unaweza mchapa Mchina viboko hata kama ukitaka kufanya hivyo? Hiyo inawezekana sababu ya unyonge wetu tunathamini wageni klk wenyeji, mgeni akifika tu siku ya kwanza hata kama alikuwa hajioni superior sisi wenyewe tutamlazimisha ajione hivyo kwa kumpa upendeleo maalumu kila mahali matokeo yake anaota mapembe na kuwadharau kuwaona Watumwa, na mpaka sasa anafikia hatua ya kuwachapa viboko.

Hivyo kumfukuza hakutatui tatizo, mnapaswa kuangalia chanzo, ni nini kimempa huyo mgeni huo ujeuri kwenye nchi ambayo siyo yake? Kwa maana siyo mara ya kwanza.
 
Director of Criminal Investigation wa Nairobi ni kilaza hana mfano. Mahala pa kujaza COUNTY kajaza CHINA!
 
Director of Criminal Investigation wa Nairobi ni kilaza hana mfano. Mahala pa kujaza COUNTY kajaza CHINA!
Ulitaka waandike Kolomije wakati watuhumiwa ni wazawa wa Uchina? Au ulitegemea DCI waibuke na comedy ya picha kutoka kwa CCTV CameraMAN kama IGP wenu na vilaza wake?
untitled.png
 
Ulitaka waandike Kolomije wakati watuhumiwa ni wazawa wa Uchina? Au ulitegemea DCI waibuke na comedy ya picha kutoka kwa CCTV CameraMAN kama IGP wenu na vilaza wake?
untitled.png
🤣🤣 wazee wa Tz VS Ke. Kwani mambo mengine ukiamua kuyapotezea utapungukiwa nini? Hata hivyo, umenikumbusha hii drama ambayo scriptwriter hakuwa professional, hata director pia aliokotwa mtaani na hivyo kufanya movie isinunuliwe...
 
Sorry bro alichomaanisha uyo jamaa ni kwamba walipopelekwa mahakamani hawakufungwa kutokana na kosa ilo kama unavyoona waafrika wenzetu wakikamatwa nchi za nje wanapelekwa mahakamani kwa kufungwa au kunyongwa ila sisi tunawarudisha kwao ndio hukumu yetu

Nimekuelewa, ila adhabu ya kufurushwa ni hatari kuliko hata hiyo ya kupelekwa mahakamani, maana kule mahakamani zitafuatwa sheria na jamaa ataadhibiwa kama Mkenya yeyote, yaani kumchapa mwenzake viboko, haitaangaliwa kwamba mgeni Mchina kafanya kwa dharau wala nini.
Bora imechukuliwa kisiasa na waziri. Kama jinsi alivyofanya waziri wenu hapa Raia wa China watimuliwa kwa kuwapiga makonde Watanzania
 
wazee wa Tz VS Ke. Kwani mambo mengine ukiamua kuyapotezea utapungukiwa nini? Hata hivyo, umenikumbusha hii drama ambayo scriptwriter hakuwa professional, hata director pia aliokotwa mtaani na hivyo kufanya movie isinunuliwe...
Boss sio ligi wala hamna cha kuamua kuyapoteza, ni KUMBUKUMBU tu. Maproducer wamelala sana na tunangoja kwa hamu chapter ya pili ya hiyo filamu ya kukata na shoka, IGP Sirro & The CCTV Cameraman Sn2.
 
Sidhani kama kuna kosa kumfukuza mgeni asiyefaa kuishi kwako.
sijasema ni kosa always try to read to understand,kumrudisha mtu kwao baada ya kutuhumiwa ametenda kosa ni kutafsiri sharia vibaya,hawa wachina wametuhumiwa kutenda kosa ilitakiwa wapelekwe mahakamani ili kesi yao isikilizwe na hakimu aamue,kama wako huru au wametenda kosa(ndivyo ilivyotakiwa kufanywa)sasa wewe nenda China na utende kosa kama hili tuone kama China watakurudisha kabla ya kupanda kwenye mahakama zao.
 
Mkuu hivi unajua adhabu ya kimahakama kwa kosa la kumchapa mtu viboko, mimi sijui ila naamini itakuwa ndogo sana pengine ni kulipa faini chini ya 100k, kwangu naona ni vema warudishwe kwao kwanza watakosa mapato pili corona inawasubiri, hiyo ni adhabu kubwa kuliko kumfunga mwezi mmoja kisha anarudi kufanya biashara.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umenifurahisha sana mkuu,ok tuwe makini nao kumchapa mtu hilo ni kosa kubwa mno kisheria maana umemdhalilisha kama binadamu,umedhalilisha utu wake,ndio maana hawa wangekuwa huku niliko Lingusenguse wangepanda mahakamani,mahakama ingeamua na baada ya hapo waliodhalilishwa kwa kuchapwa viboko wangefungua kesi ya madai dhidi ya watuhumiwa(hukumu ikitoka in their favour ,wachina hawa mali zao zingepata msukosoko mkubwa),hapa Lingusenguse hata ukimpiga mtoto wako kisheria umetenda kosa na unaweza kuhukumia kifungo jela.
 
sijasema ni kosa always try to read to understand,kumrudisha mtu kwao baada ya kutuhumiwa ametenda kosa ni kutafsiri sharia vibaya,hawa wachina wametuhumiwa kutenda kosa ilitakiwa wapelekwe mahakamani ili kesi yao isikilizwe na hakimu aamue,kama wako huru au wametenda kosa(ndivyo ilivyotakiwa kufanywa)sasa wewe nenda China na utende kosa kama hili tuone kama China watakurudisha kabla ya kupanda kwenye mahakama zao.

Walishashitakiwa na kuamriwa wafukuzwe nchini Kenya, isitoshe bila shaka wamefwata Sheria Kenya inavyosema kuhusu mgeni vinginevyo hao wageni wangepinga Mahakamani kufukuzwa, hata hivyo mimi siyo Mwanasheria.
 
Mbona walishawasilishwa mahakamani, mpo wazembe sana hata kusoma mnashindwa, kazi kubwatuka tu baada ya kusoma kichwa cha habari.
sometimes kujibia hoja kama hii nako ni kujidhalilisha,mtoa hoja ameelezea kuwa mahakama ilitoa kibali cha kuwashikilia watuhumiwa hao(wenzetu wanajielewa kuwa huwezi kumshikilia mtuhumiwa zaidi ya 14 days bila ya kibali cha mahakama)ili mtoa hoja hajatuambia kuwa hawa wachina walishafunguliwa mashitaka na mahakama kuamua hatima ya kesi hii,please usome tena huu uzi na mtoa hoja katuambia kuwa vile vile wachina hawa working permits zao zilikuwa sio halali,na walikuwa na visitors visa (ambazo haziruhusu kufanya kazi au biashara)sasa hili ni kosa kubwa ,hapa nilipo Lingusenguse tuhuma kama hii ni kubwa ,unapelekwa mahakamani kwa kuchapa watu viboko,then kwa kuwa na hati batili,makosa haya unakwenda jela na baada ya hapo systems inakupa hati ya kutoruhusiwa tena kuingia hapa na unarudishwa kwenu siku umemaliza kutumikia adhabu yako,jitahidi kusoma kwa kuelewa sio kuuliza maswali,next time mkuu.
 
Back
Top Bottom