Serikali ya Kenya isikae kimya tuhuma za ulimboka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya Kenya isikae kimya tuhuma za ulimboka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mjomba wa taifa, Jul 14, 2012.

 1. Mjomba wa taifa

  Mjomba wa taifa JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 232
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kamanda mkuu wa kanda maalum ya polisi, DSM Suleiman Kova ametoa taarifa ya kukamatwa kwa mtu anaesadikiwa kumteka na kumdhuru kiongozi wa jumuiya ya madaktari wa Tanzania Dr. Steven Ulimboka kuwa ni raia wa Kenya na anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

  Tuhuma kama hizi ni nzito zenye kuweza kuleta uhasama baina ya raia wa Kenya na Tanzania. Hali kama hii si inahatarisha maisha ya wakenya wote waliopo nchini bali hata watanzania wanaokwenda nchini Kenya maana kila upande utataka kulipiza kisasi.

  Nategemea Serikali ya Kenya italichukulia suala hili kwa uzito zaidi ikiwa ni pamoja na kutoa ushahidi kuwa mtuhumiwa huyo ni raia wa Kenya.

  Kama Serikali inalengo la kuficha ukweli juu ya Jambo hili isitumie nafasi hii kuwagombanisha watanzania na nchi jirani. Viongozi wa Serikali wanakuja na kuondoka madarakani lakini raia wapo milele katika nchi zao.

  Ni Matumaini yangu kuwa Serikali ya Kenya imekwishazipata tuhuma hizi za raia wao anaeshikiliwa na Kova na haitokaa kimya. Sitegemei Wakenya watavumilia kuchafuliwa kwa kufunika uozo wa serikali ya Tanzania.
   
 2. Asterisk

  Asterisk JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 215
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Walishafikiria yote hayo kabla hawaja engineer hilo tukio... Wanaweza wakashirikiana kumaliza hili tukio,
   
 3. m

  muchetz JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2012
  Joined: Aug 16, 2010
  Messages: 495
  Likes Received: 97
  Trophy Points: 45
  Kwa namna ya mambo wanavyofanya uwezo huo wa ku connect mambo ni mdogo sana...... sidhani kama walilifikiria hilo
   
Loading...