Serikali Ya JPM Yaweka Historia, Yadhibiti Kikamilifu Biashara Ya Madawa Ya Kulevya Uwanja Wa Ndege Wa Mwalimu Nyerere

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956


Pic+dawa.gif


Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi wa Viwanja vya Ndege, Matanga Mbushi amesema wamedhibiti mianya ya upitishaji wa dawa za kulevya katika Viwanja vya Ndege vya Mwalimu Nyerere (JNIA).

Akizungumza na Mwananchi leo Mei 27, Mbushi amesema katika kipindi cha Februari hadi Mei mwaka huu miezi mitatu hawajakamata mhalifu yeyote wa dawa za kulevya.

“Hii ni kutokana na kudhibiti mianya ya usafirishaji wa dawa hizo, tofauti na zamani,” amesema.

Mbushi amesema kutokamatwa wahalifu hao JNIA huenda pia ni kiashiria kuwa wamebuni njia nyingine ambazo hazijatambulika.

“Wafanyabiashara hao haramu inawezekana wamebuni mbinu mpya nyingine ambazo hatuzifahamu hivyo tumejipanga na kuendelea kuwadhibiti ili uwanja wa JNIA usitumike kama uchochoro wa kupitisha dawa za kulevya,” amesema Mbushi.

Ametoa wito kwa wananchi washirikiane na vyombo husika wanapoona kuna mtu anajihusisha na dawa za kulevya kwa kuwa vita hii ni ya watu wote inatakiwa ushirikiano wa hali ya juu.
MCL



 
Siku vituo vya methadone vikizidiwa ndio tutajua madawa kitaa hakuna .Tena kama hamjakamata inabidi mjifikirie vizuri huenda they have outsmarted you na sembe inaingia kiulaini .

Mt
 
mtanzania akamatwa huko infia na mzigo wa 5B na huwenda alianzia hapo safari kabla ya kuunganisha kwenda huko
 
Kiukweli Mateja wanaanza kupungua, sema kuna ubunifu mpya wa kutengeneza
madawa ya kulevya nje ya yale yaliozoeleka hili litakuwa tatizo kubwa zaidi kwani
zinatumika bidhaa zipatikanazo hapa hapa nchini tena kwa unafuu zaidi.
 
Kiukweli madawa na bangi kwa sasa yamedhibitiwa kuingia na kutoka dar,sema nchi jirani ndio biashara zinafanyika ila bongo viva police wa Tz
 
Back
Top Bottom