Serikali ya JK na Mkakati wa Kilimo Kwanza- PowerTiller | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya JK na Mkakati wa Kilimo Kwanza- PowerTiller

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tony Almeda, Jan 18, 2012.

 1. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #1
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi hii nchi ina wataalam kweli? Kutuingiza watanzania mkenge kwa kutuletea powertiller ambazo haziwezi kulima labda kubeba majani ya ngo'mbe. Ni heri ulime kwa plau kuliko haya mapowertiller yao.

  Hizi powertiller zimejaa katika Halmashauri za miji, Nyingi ziko chini ya kiwango na hii ni mikopo kutoka serikali ya watu wa China kwa Tanzania na mpango wao wa kilimo kwanza.

  Hivi wataalam wetu wa kilimo hawajaona kama hizi powertiller zinavyolima kwenye mashamba ya mpunga ya kule China, Wakafananisha na kwenye ardhi yetu ya mbuga tulime kilimo cha pamba au mahindi? ni vitu viwili tofauti.

  Kwa mpango huu huo mkakati wa kilimo kwanza si utaishia kwenye midomo ya viongozi huku uhasilia tofauti? na hili ni deni lingine tumejipa sisi na vizazi vyetu.
  Eti wametuletea huku Shinyanga tulime kilimo cha pamba, yaani kumaliza heka moja kuilima utadhani umelima hekali mia, hamna kitu kabisa. vibovu mara kanapinduka, vijembe vidogo, yaani kero tupu.
   
 2. N

  Nyalutubwi JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 1, 2012
  Messages: 572
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 45
  Ni yale yale ya ujanja ujanja.Fuatilia kilimo kwanza na SUMA JKT utagundua ya kuwa kuna ajenda za siri zimejificha nyuma yake.Kile ambacho mimi nakiona SUMA JKT ni ni wajanja kuitumia taasisi hiyo ili kufanya biashara yenye nafuu ya kodi kutokana na ukwepeshaji wa kodi hasa kwenye Mafuta na vilainisha mitambo.Nakumbuka kule Mza kuna kampuni moja ya mafuta ambayo kwenye miaka ya 1999/2000 ilikuwa mbia wa Suma JKT ikiagiza mafuta bila kulipia kodi kwa ajili ya Suma Jkt lakini yote yaliuzwa kwenye soko la kawaida na naamini hali hii bado ipo.
   
 3. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wao wakishajihakikishia ten percent yao tu basi hawaangalii madhara yatakayosababishwa na hiyo kamisheni waliyovuta. Nchi hii inahitaji sheria kali za kuwabana viongozi wataotuingiza mkenge.
   
 4. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Lakini kiujumla uwekezaji katika kilimo ni wa msingi sana! Labda tupeana mawazo tu, hayo matiller yapatikanaje na wakulima wayatumie!
   
 5. Atubela

  Atubela JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2012
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 637
  Likes Received: 549
  Trophy Points: 180
  Kilimo cha Tanzania hovyo hizo kauli mbiu tushazichoka tangu enzi ya siasa ni kilimo, kilimo cha kufa na kupona, kilimo ni uti wa mgongo n.k bado tatizo letu ni katika utekelezaji, kama huu mpango wa kilimo kwanza na powertiller ambazo sidhani kama walifanya utafiti wa ardhi na aina ya kilimo labda mpunga na ardhi isiwe mfinyanzi.
   
 6. L

  Lung'wando Member

  #6
  Jan 18, 2012
  Joined: Dec 11, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Pita pale Dodoma uone namna yalivyorundikwa. Yanapauka na jua tu.
   
Loading...