Serikali ya JK na mikurupuko kwenye simu za mikononi. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya JK na mikurupuko kwenye simu za mikononi.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Indume Yene, Dec 17, 2011.

 1. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #1
  Dec 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Nimekutana na hii story kwenye Tanzania Daima, nimebaki nashangaa. Ni lini serikali yetu ilifanya research na ku-come with this finding. Soma mwenyewe.

  Mkuchika akataza simu shuleni

  na Halfani Lihundi, Arusha

  SERIKALI imepiga marufuku matumizi ya simu za mikononi kwa wanafunzi wa shule za sekondari wawapo shuleni, kwa maelezo kuwa simu hizo zinasababisha wanafunzi kutokufanya vizuri katika masomo yao.
  Kwamba simu hizo pia husababisha tamaa na vishawishi kwa wanafunzi kwani baadhi yao hulazimika kutafuta fedha za kununulia muda wa maongezi hata ikiwalazimu kufanya matendo maovu.
  Amri hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Kapteni mstaafu, George Mkuchika, wakati akifungua mkutano wa walimu wakuu kutoka mikoa yote nchini na nchi za jirani.
  Mkutano huo, una lengo la kujadili changamoto zinazokabili sekta ya elimu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki na maandalizi ya Tanzania katika kukabili changamoto hizo.
  Mkuchika alisema mwanafunzi anapojiunga shuleni kwa mara ya kwanza huwa zinachukuliwa taarifa zote za mzazi au mlezi ikiwemo namba za simu ili kuwasiliana naye panapotokea matatizo na kwamba hata mwanafunzi wa kutwa anaporudi nyumbani kila siku anaweza kueleza matatizo yako, hivyo hakuna sababu ya wao kuwa na simu wakiwa shuleni.
  Mkuchika alisema wizara yake ndiyo yenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya shule za sekondari, hivyo imezitaka bodi za shule kuandaa kanuni zitakazowabana wazazi na wanafunzi katika matumizi ya simu kwa wanafunzi na wizara itasimamia ili kuakikisha kuwa mkakati huo unafanikiwa.
  Akisoma risala ya wakuu hao wa shule za sekondari, Mwenyekiti wa Taifa wa umoja wao (Tahosa), Bonus Ndimbo alibainisha changamoto zinazowakabili na kusababisha kazi yao kuwa ngumu.
   
 2. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Mobile phones 'boost school standards'

  Schoolchildren should be allowed to use mobile phones in the classroom to boost education standards, according to researchers. Despite fears that mobiles and MP3 players are a huge distraction, it is claimed schools can get the most out of pupils by giving them full-time access to the latest gadgets.

  Academics said mobiles could be used for a wide range of educational purposes, including creating short movies, setting homework reminders, recording a teacher reading a poem and timing science experiments. New-style "smartphones", which can connect to the internet, also allowed pupils to access revision websites, log into the school email system, or transfer electronic files between school and home.

  Employing them as part of day-to-day lessons boosts pupils' motivation levels, it was claimed. The conclusions come despite high-profile calls from teaching unions for an all-out ban on the use of mobiles in schools. It is claimed that the technology is a distraction from pupils' work and fuels "cyber-bullying" - as children take compromising pictures and video clips of teachers or pupils and distribute them to friends.

  Mobile phones 'boost school standards' - Telegraph
   
 3. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Mia kwa mIa na support serikali, with hizi TIGO free talk usiku, wanafunzi hawalali ni wanatongozana usiku kucha na kupeana maneno ya mahaba.Hilo ni tatizo , ukizingatia vocha zenyewe za ku omba na hapo ndio matatizo yana zidi yakulipiwa vocha kw angono!
   
 4. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #4
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Tatizo ni wanafunzi kutolala usiku au kutongozana kwenye simu? Serikali imepiga marufuku matumizi ya simu za mikononi kwa wanafunzi wa shule za sekondari wawapo shuleni. Sio wakati wakiwa majumbani usiku unless unamaanisha wale wa boarding?
   
Loading...