Serikali ya JK kuhamisha Wanakijiji kumpa mwekezaji ardhi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya JK kuhamisha Wanakijiji kumpa mwekezaji ardhi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Nov 26, 2009.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Nov 26, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Serikali yetu ni inashangaza. Jana TBC1 imeripoti kuwa mkuu wa wilaya huko Kilombero anasimamia mchakato wa kutaka kuhamisha wanakijji wa kijiji cha Namawala huko Kilombero kinyume na matakwa yao ili mwekazaji apewe ardhi ya kijiji kulima miwa.

  Yaani Wanakijiji watanzania wanaokaa katika kijiji kisheria wahamishwe kutoka kwenye ardhi yao yenye rutuba apewe Mnyonyaji. Hii tabia ya serikali inayoota mizizi inatofautiana vipi na wakoloni ambao walichukua ardhi yetu yenye utajiri wa maliasili? Hivi wanakijiji ndio wanaostahili kukaa maeneo yasiyofaa? Tumesikia huko Loliondo sasa wanaelekea Kilombero, hii ni serikali gani isiyojali wananchi wake kwa kiwango hiki? Hivi serikali inaajenda ya siri ya kurudisha ukoloni nchini kwetu? Wananchi wanataabika tayari kwa hali ngumu ya maisha, serikali ikiendekeza sera ya kunyangÂ’anya ardhi watanzania ambayo ndiyo tegemeo lao na kuwapa wanyonyaji hali itakuwaje?
   
 2. R

  Rodelite JF-Expert Member

  #2
  Nov 26, 2009
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 320
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Duh....Huu ni unyama sasa....!!!
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 26, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mumeangalia ile video ya Bulyankulu? Ndizo sera za serikali ya kifisadi hizo. Mzungu kwanza, fisadi anafuata na wananchi ole wenu.
   
 4. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #4
  Nov 27, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Tufanye nini sasa kujiokoa, manake wananchi hawataki, wanaharakati wanapinga lakini...
   
 5. M

  Mchili JF-Expert Member

  #5
  Nov 27, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Haya ndio waliofanyiwa Wazimbabwe na waingereza, Waafrica Kusini na Makaburu ikawaletea umaskini mpaka leo. Tusipoangalia vizuri tukiwaachia hawa viongozi wetu wenye njaa na ufinyu wa mawazo, tutajapigania uhuru wetu upya very soon. Kuna haja ya wanaharakati kungilia kati kuzuia operation kama hizi hata ikibidi kutumia nguvu.
   
 6. Kapinga

  Kapinga JF-Expert Member

  #6
  Nov 27, 2009
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 728
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ndo Kilomo Kwanza Hiyo imeanza!! Hamna kilichobaki kuuza wameona bora wauze ardhi sasa!!
   
Loading...