.serikali ya jk kama ya idd amini au mobutu seseseko wa zaire | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

.serikali ya jk kama ya idd amini au mobutu seseseko wa zaire

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by meeku, Sep 4, 2012.

 1. meeku

  meeku JF-Expert Member

  #1
  Sep 4, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 571
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Najaribu kutafakari uongozi huu wa awamu ya nne na jinsi watu wanavyouawa na ndipo napata picha kuwa uongozi huu hauna tofauti na ule wa idd amini au wa mobutu seseko wa zaire.

  Hii picha naona kama ndo inaanza tena kwa kasi ya ajabu. Arusha wamepiga watu watatu risasi kisa maandamano ya chadema, ikafuata arumeru, muvi ikaenda mbeya, ikafuata Igunga, Mwanza, Morogoro na tena sasa ni Iringa.

  Wamemwekea sumu Mwakyembe, Mwandosya na juzi juzi tu kumsulubu Ulimboka. Yote haya ni kwamba mwananchi hapaswi kuhoji au kudai haki.

  Swali hawa Polisi wanapata wapi hii kiburi kama siyo kuagizwa na uongozi wa juu na zaidi kutoka ikulu?

  Serikali hii ndo imekuwa ya kifisadi pengine bora ile ya Mobutu. Mabilioni yanafichwa nje ya nchi na mikataba ndo kwanza inazidi kusainiwa tena mingine huko nje ya nchi. Watoto wa vigogo tena wa juu kabisa ndo wamekuwa wawekezaji kwa kujenga mahoteli, petrol stations, kumbi za starehe na mambo mengine mengi ya kutisha. (mwananchi usihoji la kifo kitakufuata).

  Ikulu sasa ni vita kuingia tena kwa kutumia vyombo vya dola wakiwamo hawahawa polisi.

  ni machache tu hayo. Unaweza kukumbusha mengineyo. mimi najiuliza kuna tofauti gani ya serikali ya JK na ile ya idi amini au mobutu?
   
Loading...