Serikali ya JK ikikataa kuanzisha mchakato wa katiba mpya Watanzania tunaweza kudai?

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
2,958
543
Inaonekana Serikali ya JK haina nia ya kuanzisha mchakato wa kuanzisha katiba mpya zaidi ya kuendelea kuiweka viraka.Je Wananchi tunaweza kutumia njia gani kudai katiba mpya?Wana JF tunaweza kuchangiaje mchakato huo?
 
Wanaharakati mtuongoze Watanzania kushinikiza Serikali ianzishe mchakato wa kuanzisha katiba mpya ili tuachane na katiba ya viraka.
 
inaonekana serikali ya jk haina nia ya kuanzisha mchakato wa kuanzisha katiba mpya zaidi ya kuendelea kuiweka viraka.je wananchi tunaweza kutumia njia gani kudai katiba mpya?wana jf tunaweza kuchangiaje mchakato huo?

umeuliza swali zuri sana. Tokea mwaka 1992 mfumo wa vyama ving ulipoanzishwa vyama vya upinzania vimekuwa na ajenda ya kudai mabadiliko ya katiba ambayo yatawashirikisha wadau wote ikiwemo asasi za kiraia, madhehebu ya dini, asasi za kitaalamu, asasi za wakulima, wafanyakazi, vijana, akina mama, walemavu, wazee n.k.

Baadhi ya vyama vya upinzani vilifikia hatua ya kuitisha maandamano juu ya suala hilo, lakini muitikio wa sisi watanzania ulikuwa ni mdogo sana kuweza kutuma ujumbe kwa serikali na jumuia ya kimataifa kuwa watanzania wanahitaji mabadiliko ya katiba kwa njia za amani.


badala yake ccm yenye wananchama karibu ya milioni nne imekuwa ikisisitiza kuwa katiba iliyopo haina tatizo lolote. Hivyo kwa kutumia wingi wawananchama wake imekuwa ikikumbatia katiba hii nyenye mapungufu makubwa, yenye kuweka tume isiyo huru ya uchaguzi n.k. Kama watanzania tunataka katiba ifanyiwe mabadiliko ni lazima tuhakikishe kuwa tunaelimishana ili kila mmoja aweze kuhsisha umaskini na uduni alionao na mapungufu ya katiba ili aweze kushiriki katika harakati za kudai katiba mpya iwe ni maandamano n.k

kwa bahati mabya watanzani tulio wengi tumekuwa tukivitegemea vyama vya siasa kwa kusukuma mabadailiko kama haya ya kudai katiba mpya. Haya ni mapungufu makubwa. Ikiwa wananchi tutaweza kuanzisha mjadala mpana kwa maan aya kima mtanzania kufikishiwa ujumbe na akatambua mapungufu yaliyoko katika katiba yana uhusiano wa moja kwa moja na matatizo yanayomkabili, ni wazi kuwa mabadiliko ya katiba itakuw ani ajenda ya kila mtanzania na vyama vya siasa vitalazimika kutupendeza kwa kubadili katiba ili vipate kura zetu.

Ili kufikia lengo hilo ni wazi kuwa ipo kazi kubwa ya kufanywa na wananchi ya kuelimishana wenyewe kwa wenyewe mapungufu ya katiba iliyopo na faid za kufanya mabadiliko ya katiba mpya
.

hatari iliyopo ya kutegemea vyama vya siasa kusukuma mabadiliko makubwa kama haya ni kuwa katiba iliyopo ni nzuri sana kwa mtawala yeyote awe ccm , cahdema, cuf n.k. Kutokana na kukerwa na chama kilichopo madarakani watanzania wanaweza kuiondoa ccm madarakani na kuingiza chama kingine huku katiba ikiwa bado na mpungufu yale yale kutokana na watanzania kutokujua kuwa mapungufu ya katiba ndio has chimbuko la matatizo yote tuliyonayo.

Kutokana na mapungufu ya kibinadamu viongozi wa chama hicho kipya nao wanaweza kuing'ang'ania katiba hii mbovu kutokana na ujinga wa watanzania walio wengi na tukaendelea kuumia vile vile.


muarobaini wa katiba mpya uko mikononi mwa watanzania wenyewe, vyama vya siasa vitaidaka ajenda hii kama watanzaniawalio wengi watakuwa wamelimishwa kudai katiba mpya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom