Serikali ya Kikwete ni dhaifu kupita zote duniani

Acheni ujuha nyie!!! Kwani serikali zote duniani hufanya utafiti wa dawa zote za mitishamba ambazo zinatumiwa na traditional healers? Sisi kule kwetu kuna mganga anaitwa Tagalu, huyu bwana huweza kuchemsha vichwa vya nyoka na kuvitumia kama dawa. Je ni serikali gani inayoweza kutathimini kujua kwamba vile vichwa vya Nyoka ni salama?

Kijijini kwenu kuna waganga wangapi wa jadi? Mizizi yote wanayotumia kutibia inapimwa? Hakuna serikali hata moja duniani ambayo huweza kufanyia utafiti dawa zote za kienyeji. Na sababu ya msingi ya kushindwa kufanya hivyo ni kutokana na kukosekana kwa ushahidi wa kisayansi unaoonyesha kwamba vitu hivyo vinavyotumiwa na waganga wa jadi, ni dawa. Vingi vinatibu kwa imani!! Kwa mfano, mkemia mkuu anawezaje kutafiti ufanyaji kazi wa hirizi? Kuna watu wanamezeshwa mdomo(beak) wa tai, je mkemia mkuu anawezaje kuthibitisha kwamba mdomo wa tai ni dawa? Ni mkemia gani anayeweza kuthibitisha kwamba mkia wa simba unatibu?

Angalieni hoja za kuilaumu serikali nanyi!!! Halafu siyo hekima kabisa kusema serikali ya Kikwete ndiyo dhaifu kupita zote duniani kwa kuwa eti imeshindwa kuingilia masuala ya imani! Kwa kusema hivyo ni kama kumtuma kikwete kujishughulisha na mambo yote yakiwemo ya ushirikina na imani juu ya Mungu. Kuna mkemia anayeweza kuthibitisha kwamba kuna Mungu?

Huyu ndo haelewi kabisaa! Si msome japo dudus apo juu,au naye hujamwelewa! Kuwa mkweli ndugu, hata ktk dini/imani huwezi tumia sumu/haraam kufanya tiba/halali. Plz soma vzr post ya dudus!
 
Ndugu, kwa maoni yangu una hoja ila si kwa kuwa serikali imechelewa/zembea kuchunguza dawa ya Babu bali kwa kuwa serikali yetu always inazembea kwenye mambo ya msingi yakiwamo yale yanayogusa afya za wananchi moja kwa moja. Wewe unakuwa na hofu na dawa ya Babu kwamba inaweza kuleta madhara baada ya miaka kadhaa; sawa inawezekana lakini madhara hayo, kama yatakuwepo ni madogo mno kulinganisha na madhara mengine mengi ambayo wananchi WOTE (na siyo wagonjwa wachache tu kama ilivyo kwa Babu) tunayapata katika maisha yetu ya kila siku bila serikali yetu kujishughulisha. Hebu fikiria mifano michache ifuatayo:-

(i) Vyakula - nyama ya kuku wa kisasa:- Hivi unajua aina ya vyakula ambavyo kuku wa kisasa wanalishwa? Inadaiwa baadhi ya wafugaji wamefikia hata hatua ya kuwalisha ARVs, vidonge vya uzazi, na madawa mengine mengi ambayo yana madhara makubwa kwa binadamu. Je, ulishawahi kusikia serikali yetu angalau ikijishughulisha kufanya uchunguzi wa nyama ya kuku inayoingia sokoni? Ni maelfu ya watanzania wangapi wanaotumia nyama ya kuku kila siku?

(ii) Vyakuala - Maziwa ya ng'ombe:- Hivi unajua baadhi ya wafugaji hawafuati masharti pindi ng'ombe wanapokuwa kwenye dozi? Serikali imewahi kujishughulisha kufuatilia ubora wa maziwa yanayoingia sokoni kila siku?

(iii) Vyakula - Samaki:- Ni wazi kuwa baadhi ya wavuvi hutumia sumu kwenye uvuvi wao na hata usafirishaji na uhifadhi wa samaki haukidhi viwango. Je, serikali inajishughulisha kwa hilo?

(iv) Vyakula - Nguruwe:- Kama ilivyo kwa nyama ya kuku, je, ni maelfu ya watanzania wangapi wanakula nguruwe ambao hawana ubora kiafya? Serikali inajali?

(vi) Vyakula - nafaka:- Hivi unajua mbolea na madawa ya kilimo yakitumiwa bila kuzingatia viwango athari zake zinabaki hata kwenye vyakula vitokanavyo na mazao hayo - tena hapo ndio kansa imelala; fikiria DDT, n.k; Je serikali inajali kupima,kwa mfano unga unaosagwa pale Manzese na maharage yanayouzwa pale Tandale na kwingineko kama yana ubora kiafya?

(v) Mfumo wa maisha - moshi wa magari:- Serikali yetu inajali kuhakikisha kwa mfano uchafuzi wa anga hauzidi viwango vianvyotakiwa? Moshi wa magari ni kansa tupu ile!

(vi) Madawa ya binadamu:- Serikali inao udhibiti inavyotakiwa kwamba madawa yanayotumika nchini yana viwango vinavyotakiwa na yanatumika kama inavyotakiwa na kwa wakati?

(vii) Vyakula vya viwandani:- Serikali inadhibiti kikamilifu vyakula vinavyozalishwa viwandani na je wananchi wanazingatia matumizi yake inavyostahili? Expiry dates, n.k. Hapo pia kansa imelala.

(viii) Mifumo ya maisha - ulevi:- Serikali inadhibiti mifumo mbali mbali ya maisha kwa wananchi wake hasa kwenye suala la ulevi? Fikiria ni watu wangapi wamepata kansa kutokana na ulevi ikiwapo matumizi ya gongo, sigara, n.k.

(ix) ... n.k., ... n.k. orodha ingeweza kuwa ndefu kadiri uanvyotaka.

Kwa wenzetu Ulaya huwezi ukazalisha mavitu yako huko halafu ukalisha wananchi bila ukaguzi na udhibiti wa serikali makini. Labda ndio maana wenzetu hata "life expectancy" zao ni zaidi ya 80! Hapa kwetu nasikia tuko 46!

Hivyo, msururu unaoonekana kwa Babu, kwa sehemu kubwa, ni matokeo ya kupuuzia hayo yaliyoorodheshwa hapo juu. Vinginevyo, tatizo lisengekuwa kubwa kama linavyoonekana hivyo pengine Babu leo hii asingekuwa na kazi ya kufanya. Kwa ufupi athari za dawa ya Babu, kama zitakuwepo, ni ndogo mno kulinganisha na athari tunazokutana nazo kwenye maisha yetu ya kila siku. Kitaalamu tungeweza kusema ni "negligible".

Tafakari na chukua hatua!

Dudus, basically anachosema Mlangaja ndicho unachosema wewe. hatuna serikali inayojali watu. Kama ni upigaji wa mpira basi ni ule unaoitwa bora liende.
 
Dudus, basically anachosema Mlangaja ndicho unachosema wewe. hatuna serikali inayojali watu. Kama ni upigaji wa mpira basi ni ule unaoitwa bora liende.
ni kweli serikali haiwezi kudhibiti dawa za asili zinazotolewa vijijini huko. Ila kwa hili ni tofauti sana. Huyu amenywesha dawa malaki ya watu na serikali inaunga mkono na hata mawaziri, wabunge na viongozi wengine wanaenda. Mimi naweza kwenda pia wala simpingi huyo mchungaji. Wasiwasi wangu tu ni pale taifa linaweza kupelekwa tu kama vile hamna kiongozi. Serikali inayojali ingepima kwanza dawa na kuwahakikishia wananchi kuwa haina tatizo. Pili ingewapima wanaosema wamepona na kuwahakikishia wananchi kuwa tiba hiyo inaponyesha. Hii dawa ni zaidi ya imani. Imani ni kama zile za akina Kakobe kwamba unaombewa tu. Hii ni dawa unakunywa na inaweza kuwa na side effect. Huyu mchungaji angekuwa Roman Catholic kanisa lisingemruhusu afanye kazi bila kuwa na uthibitisho wa kidaktari. Ndio maana hata mtu anaposema amepona kwa kutumia jina la mtu anayetarajiwa kuwa mtakatifu wanampeleka kwa daktari bingwa tena independent kuthibitisha. Huu ndio umakini unaotakiwa. Na kiukweli jamii ya kitanzania inapenda sana rumours. Hivi hushangai kwanini Sheih Yahya anapewa sana umuhinu na jamii? Tusipoangalia tutakuja kuzika mamilioni ya watu. Sidhani kama kuna serikali yeyote duniani iliwahi kuamini haraka hivi tena bila ushahidi wa kuaminika kuwa kuna mtu anatibu watu na wanapona. labda kama kuna mtu anajua aniambie. Kwa kuwa hii ndio serikali ya kwanza kufanya hivyo ndio maana nikasema ni serikali dhaifu kupita zote kwa sasa.
 
Ukipigwa na mkeo unalalama kuwa serikali mbona imekaa kimya, ukifumania mtu akim...... mkeo unalalama kuwa serikali haipo makini, ukibanwa haja, mbona serikali haizuii. Watu wa kutaka kila kitu wafanyiwe na serikali hawatapata maendeleo hata siku moja. Maendeleo unajitafutia mwenyewe na siyo kusubiria kufanyiwa. Kizazi hiki hakitaki kuwajibika na kufikiri kila kitu kitaletwa na serikali, huo ni uongo. Na kiongozi yeyote wa siasa anaye wadanganya watu kuwa kila kitu kitaletwa na serikali hebu tumpe mwaka mmoja tu tuone, atafulia.
CHANGANYA YA KUAMBIWA NA AKILI YAKO MWENYEWE................. Amkeni usingizini, fanya kazi siku sita utaona matokeo yake.
 
Back
Top Bottom