Serikali ya Ivory Coast imefikia makubaliano na wanajeshi wa nchi hiyo kumaliza mgomo uliodumu siku mbili kushinikiza malipo ya ziada na mazingira bora ya kuishi kwa wanajeshi.
Rais wa nchi hiyo wakati akiongea na mawaziri wake amesema njia waliyotumia wanajeshi kufikisha madai yao sio nzuri na imeharibu taswira ya nchi yao.
Kufuatia hatua hiyo, wanajeshi waliozingira nyumba ya waziri wa mambo ya ndani wameondoka dakika chache baada ya Rais kutangaza kwenye televisheni ya Taifa kumaliza mgomo huo, Askari hao walisikika wagipiga kelele na kusema 'Tunahitaji malipo yetu sasa na sio wiki ijayo'.