MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 20,897
- 63,783
Mahakama ya dunia al maarufu kama The International Court of Justice (ICJ) imetoa hukumu yake leo tarehe 3/10/2018 kwenye kesi ambayo Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilifungua mnamo tarehe 17/7/2018 dhidi ya Shirikisho la mataifa yaliyoungana ya Marekani (United States of America). Iran ilifungua kesi hii kupinga vikwazo ambavyo Serikali ya Raisi Donald Trump iliiwekea punde baada ya Marekani kujitoa kwenye Mkataba wa Nyuklia (The Joint Comprehensive Plan of Action).
Jamhuri ya Iran ilidai kwamba maamuzi hayo yanakwenda kinyume kabisa na Mkataba wa Urafiki uliosainiwa baina ya Serikali ya Iran na Marekani mnamo mwaka 1955 (The Treaty of Amity, 1955). Mkataba huo unazitaka serikali za Marekani na Iran kuheshimu raia, kampuni na mali za nchi zao wakati wote wa uhai wa mkataba huu.
Mahakama hiyo ya kimataifa, katika hukumu yake imeamuru kwamba Marekani iitolee Iran vikwazo kwenye bidhaa zote ambazo ni muhimu kwa uhai na usalama wa raia (Humanitarian Goods) na usafiri wa anga wa nchi hiyo: Hivyo vitu kama madawa, vyakula , bidhaa za kilimo na vyombo vya usafiri wa anga havitakiwi kabisa kuwekewa vikwazo na Marekani.
Hivyo jopo la majaji 15 wakiongozwa na Raisi wa Mahakama hiyo, Jaji Abdulqawi Ahmed Yusuf limeamuru Marekani isitishe hivyo vikwazo kwa muda.