Serikali ya hovyo, Bunge la hovyo na Mahakama ya hovyo. Tumefika hapa kwa CCM kwa kuiba kura na kumlazimisha kuwa rais

Tuliambiwa hapa kazi tu. Imekuwa kinyume. Serikali hii ya Magufuli inaendelea kukopa pesa kwa matumizi yasiyo sahihi, kuna miradi inaendelea kufanywa bila idhini ya hilo bunge dhaifu la Ndugai. Huyu bwana naye amekuwa kichekesho.
Rais amekimbilia Chato wiki ya 7 bila ya maelezo ya kutosha (Kuna wapo wanaojaza mapovu kuwa rais ana haki ya kukaa popote. Mna matatizo ninyi ebu msome katiba inasema nini? Kuna wengine ni watukanaji ambao wapo kwenye payroll ya Polepole, nawataka hao watumie akili kidogo (kama wanazo) tunapojadili hili kwa maslahi ya nchi yetu.

Magufuli amekosa mikutano miwili ya SADC na EAC kujadili mambo muhimu ya kikanda, hatujui sababu. Magufuli hajawahi kwenda UN hata mara moja kwa kipindi alichokaa madarakani, aliyemwakilisha ni waziri asiye na experience yoyote na mahusiano ya kimataifa. Ni mtu wa ovyo anayejua diplomasia ya mitishamba, hakuna anachojua zaidi ya propaganda za levels za ujima.

Atakayesema kuwa hatujakosa lolote kwenye mikutano miwili ya EAC na SADC atakuwa ana shida kichwani, tena kubwa. Madereva wetu wanazuiwa mipakani kwenye nchi zinazotuzunguka, malori yapo mipakani na bidhaa (perishable) zinaendelea kuharibika na wengine ni wagonjwa hawapati matibabu bali wanarudishwa Tanzania kwenda kulundikwa lundikwa huko Amana au Mloganzila na kwenye makambi yasiyo na huduma.

Kwanini Magufuli anaficha namba za wanaougua? Madhara yake yanaeleweka vizuri. Tumekosa fedha za kukinga uchumi kutokana na madhara ya CORONA na kusaidia kuutokomeza ugonjwa wakati majirani zetu wamepewa. UKWELI NI KITU KIZURI SIKU ZOTE huyo Magufuli hajawahi kuwa mkweli.

Kwanini serikali inawazuia hata wafiwa waongelee huu ugonjwa? Je ni taboo kwa Wasukuma kuongelea ugonjwa? Kuna yanayoshangaza ambayo hayaeleweki. Wakati wa msiba wa Jaji Augustino Ramadhani, tuliwaona marais wastaafu wote pamoja na majaji wakuu/kiongozi wastaafu wa Tanzania/Zanzibar wote wakiwa wamevaa Masks, mbona Magufuli hakuonekana? Ana matatizo gani? Tunapaswa tujue kwa sababu sisi ndiyo tunaolipa mshahara wake.

Haya mambo ya kukwepa kwenda mikutano ya SADC, EAC, UN, AU, DAVOS hayaeleweki. Mwanzoni tuliambiwa anaogopa gharama, hizo gharama ni kubwa kiasi gani mbona Kabudi akienda UN anatumia gharama hizo hizo? Kama hata wakiongezeka walinzi watatu kwenye details yake, gharama zake ni kiasi gani? MAGUFULI USITUDANGANYE.
Tatizo kubwa inawezekana ni lugha ya Kiingereza haiwezi hata kidogo (Hizo theses zake sijui ziliandikwaje?) Haya ndiyo mambo ya undugunaizesheni hapo Mlimani yalivyo) Au ni tatizo la kiafya. Maana hatuelewi hivyo lazima tuhisi sababu. Angekuwa anakwenda halafu anatema yai, tungejua hilo si tatizo. Ila kuongea matusi anajua.

Ni rais wa nchi gani ana-control Bunge? Anawapangia cha kufanya, eti kisa Serikali ndiyo inatoa budget. Hajui hilo ni wajibu wa serikali kikatiba, Serikali kukusanya na kugawa budget siyo tija, hata bunge lingeweza kukusanya mapato, vile vile mahakama ingeweza. Magufuli anatumia mwavuli wa kutoa bajeti kwa mahakama na bunge ili kuwapa maelekezo ya kufanya, mmeona anayoyafanya, hakuna mahakama huru, tume huru, bunge huru (Eti spika anatuambia yeye ndiye mwenye uwezo wa kufukuza na kuwavua ubunge wabunge kwa sababu ndiye aliyewaapisha., ameshasahau na yeye ni mbunge na kama spika ana mipaka ya kazi yake....Atakumbukwa kwenye historia kama spika wa ovyo kutokea nchini kwetu)

LINI NCHI HII KUTAKUWA NA HAKI?

Ndugai anafanya analotaka, yeye kazi yake kubwa ni kumfurahisha Magufuli kwa kupokea maagizo yake. Ina maana Magufuli anamsaidia kufikiri na kuendesha Bunge. Hivi rais haoni aibu kusema kuwa "AMELIAGIZA BUNGE" kama ni wizara ya serikali. Au anavyoliagiza mahakama kumaliza kesi haraka ili awape pesa za kumalizia miradi ya kujenga mahakama.

HIVI MAGUFULI ANAELEWA CONCEPT YA 3-PILLARS?

Kama haelewi kwa nini washauri wake hawamueleweshi? Jaji mkuu naye ni mtu mwingine mwenye tatizo na legelege. Nilimshangaa analivyokuwa anakataa suala la Tundu Lissu lisichunguzwe na wachunguzi huru. Tangu lini Jaji mkuu anahangaika na uchunguzi? Kweli anajua kazi yake?

Kama kungekuwa na tume huru tusingepata hilo tatizo la kuwa na rais anayekimbia kimbia hovyo.
Message sent and delivered successfully. Watakuja na vioja kupingana nawe lakini umewapa za USO.
 
Yani maoni ya mtu mmoja kama Wewe Unataka Watanzania tufikri km Wewe ?

Tanzania ni kisiwa cha amani duniani

Ukishiba sio lazima uje uandike pumba humu Mkuu
Mawazo yako ni mtu aliyeweka akili zake mfukoni harafu anakaa kwenye kahawa na kuanza kuimba Tanzania ni kisiwa cha Amani!!!!
 
Hivi jamaa hizi jumbe zinamfikia lakini!!??
Sana,amejiweka lock ila yupo anapata ujumbe toka ngazi zote yaani Mtanzania mmoja mmoja,Vitongojini,Vijijini,Mijini na kutoka Majiji yote,Kiwilaya,Kimkoa,Kitaifa,Kikanda na Kimataifa.Unafikiri kufanya analysis ya jumbe nzuri,mbaya,za washangiliaji, wakosoaji(a.k.a Wapinzani hasa CDM except NCCR.MAGEUZI ya KUB wa CCM Mh.Mbatia) ni kazi ndogo?Mzee yupo busy kinoma ndiyo maana hamalizi likizo,anachoka mno.
 
Yani maoni ya mtu mmoja kama Wewe Unataka Watanzania tufikri km Wewe ?

Tanzania ni kisiwa cha amani duniani

Ukishiba sio lazima uje uandike pumba humu Mkuu
Tupige kura uone kama yuko peke yake? Shetani kaikalia kooni nchi yetu kama corona ilivyoikalia vibaya Dunia.
 
Magufuli akupaswa kuwa Raisi sijui ccm waliwaza nini kumpa Uraisi mtu kama Magufuli.
Lengo kuu la ccm kumpa lilikuwa moja tu nalo ni kuua Upinzani Tanzania hasa Chadema. Lengo ambalo pia limemshinda.

Rais gani anaefikiri eti tukiweza kufanikiwa kuwanunua Wabunge na Madiwani wa Upinzani kwakuwa wanakubalika maeneo yale basi automaticaly wataweza kuwachukuwa na wale wafuasi wao.

Rais gani anaefikiri akiwatukana na kuwadhalilisha wengine basi watachukiwa na yeye kupendwa?? Matokeo yake kajaza maadui zake kila kona.

Rais gani anaemuagiza Spika awatimue Wabunge wa Upinzani Bungeni ili watakapozungumza nje ya Bunge basi aweze kuwashughulikia?? Na Spika nae bila aibu anatekeleza.

Yote hayo hayakumnufaisha kisiasa matokeo yake yeye ndiye kaonekana kituko. Kwa hesabu rahisi ya kuthibitisha hilo humu JF tuko members zaidi ya elfu moja(1,000). Lakini wenye mawazo kama ya kina "Bia yetu" (japo sipendi kulitaja hilo jina) hawafika hata ishirini(20). Kwa uwiano huo huo ndivyo ulivyo kwa Watz wa kawaida kabisa. Ndiyo maana tumaini lake kubwa liko kwenye Vyombo Vya Usalama.

Kuthibitisha hilo pia kwanini kwenye sakata la corona alizungumza na Wakuu wa Vyombo Vya Ulinzi na Usalama badala ya Wataalam wa Afya pamoja na Wataalam wa Fedha na Uchumi??

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii COVID-19 imekuja kuwaumbua watu!! Mambo ya ajabu kabisa yanafanyika bila hata aibu.
 
Back
Top Bottom