Serikali ya China na Tanzania zatofautiana ujenzi wa bandari Bagamoyo

Hili naliunga mkono 100%. Ukiongeza na mafuta yanayotoka Uganda. Tanga itakuwa kitovu cha maendeleo kwa ukanda wa kaskazini.
Pia Mtwara kujengwe bandari kwa mizigo ya Southern Zone.
Kuhusu Tanga, nishaeleza mahali kwa urefu! In short, Tanga nako kuna miradi miwili ya bandari... mmoja wa TPA na mwingine wa VIP Engineering!! NI mwekezaji ndie alikuwa na mamlaka ya wapi ajenge bandari baada ya kufanya utafiti! China wakaona Bagamoyo, VIP wakaona Tanga!!!

Kuhusu Mtwara... uzuri wa pale ni natural habor lakini bado huwezi kuchanganya bandari ya kawaida na oil shippers terminal! Kwa gas boom iliyo kusini, biashara ikishachanganya bandari ya Mtwara itakuwa bize sana na mimeli ya kusafirisha gas na ile mimeli ni mikubwa mno... mtu akifunga nanga; wengine mnasubiri!!!

Hayo mambo ya kusubiri ndo asiyoyataka Mchina na ndio maana akaamua aanze moja! I guess hata kiusalama not advisable!

Kwahiyo, si kwamba bandari ya sasa ya Mtwara nayo inatakiwa kupanuliwa kwa ajili ya meli za mafuta lakini hata ukitaka kujenga bandari nyingine bado huwezi kujenga pale pale! Na ndio maana hata Dangote ametaka kujenga bandari yake kwa sababu inaonekana ana uzoefu wa bandari zinazohudumia meli za mafuta kwa sababu kule Nigeria zipo sana na karibu zote kama sio zote zinajengwa separately.

Or else, labda bandari kwa ajili gas exports ijengwe Lindi na hiyo ya Bagamoyo iende Mtwara! Na Lindi nako labda watafute eneo lingine kwa sababu ilipo bandari ya sasa hata meli za kawaida ni issue kutia nanga!!! Nadhani ndio bandari yenye kina kidogo kuliko zote hapa Tanzania!
 
Kupanga ni kuchagua... kwamba tuachieni bahari yetu hata kama hatuna uwezo wa kujenga na kuacha opportunities ziende kwingine au kusema kwanini niache pori limejaa simba wakati kuna watu wenye uwezo wa kulima nami nitapata percent kupitia miradi husika!!

Kwa maskini jeuri, anaweza kusema "acha pori liwe makazi ya simba!"

Masharti yapoje both you and I know kwamba si rahisi kufahamu inside out ya mikataba ya serikali!! Hata hivyo ambacho watu wamekuwa wakikisema sana ni huo mkataba wa China kutaka kuendesha bandari kwa 40 years. Suala la 40 years sioni tatizo kwa sababu mikataba ya Build Operate & Transfer (BOT) ndivyo ilivyo!! Mtu anajenga, anaendesha kisha anakurudishia mradi wako!! Hii tunafanya hata kwenye maaisha ya kawaida! Mtu anakuja kwenye kiwanja chako, anajenga mjengo ambao anaufanyia kazi kwa miaka kadhaa kisha anakurudishia nyumba yako!!!
Kama wako serious wakajenge Mtwara hapo bagamoyo kina siri iliyojificha ndo maana serikali tukufu imeshtuka
 
Kipi bora.ukope ujenge bandari ulipe kidogo kidogo.au ajenge China waiendeshe kwa miaka 50?
Hahahaa, nimecheka sana. Yumkini huna ufahamu wa mikopo ndio maana unasema hivyo, mbali ya ugumu wa kumthibitishia mkopeshaji kwamba project yako ina payback period nzuri na viable, madudu ya mikopo hii ya kimataifa ni hatari kuliko hata hiyo BOT.

Wewe jiulize, toka tuanze kukopa deni linapungua??? Unaona miaka 50 mingi? IPTL mliongia ina muda gani sasa, manufaa yake nini? Utalinganisha IPTL na bandari? Ni woga na kutofuatilia mambo tu yalivyo duniani ila hiyo miaka si mingi as long negotiated terms zitazingatiwa.
 
Ndiyo maana vema tujurishwe mashart ya mikataba hiyo ili tuchangie kwa kujiamini.maana hapa kila mwenye chuki na jk atasema anavyoweza kama yy ndo atanufaika na hiyo port badala ya nchi
Hofu yetu ni hiyo ile mikataba haikuwa open isije kuwa faida kubwa inaenda GSM
 
Kama wako serious wakajenge Mtwara hapo bagamoyo kina siri iliyojificha ndo maana serikali tukufu imeshtuka
Jiongeze hapa:
Kuhusu Tanga, nishaeleza mahali kwa urefu! In short, Tanga nako kuna miradi miwili ya bandari... mmoja wa TPA na mwingine wa VIP Engineering!! NI mwekezaji ndie alikuwa na mamlaka ya wapi ajenge bandari baada ya kufanya utafiti! China wakaona Bagamoyo, VIP wakaona Tanga!!!

Kuhusu Mtwara... uzuri wa pale ni natural habor lakini bado huwezi kuchanganya bandari ya kawaida na oil shippers terminal! Kwa gas boom iliyo kusini, biashara ikishachanganya bandari ya Mtwara itakuwa bize sana na mimeli ya kusafirisha gas na ile mimeli ni mikubwa mno... mtu akifunga nanga; wengine mnasubiri!!!

Hayo mambo ya kusubiri ndo asiyoyataka Mchina na ndio maana akaamua aanze moja! And I guess hata kiusalama, not advisable!

Kwahiyo, si kwamba bandari ya sasa ya Mtwara nayo inatakiwa kupanuliwa kwa ajili ya meli za mafuta lakini hata ukitaka kujenga bandari nyingine bado huwezi kujenga pale pale! Na ndio maana hata Dangote ametaka kujenga bandari yake kwa sababu inaonekana ana uzoefu wa bandari zinazohudumia meli za mafuta kwa sababu kule Nigeria zipo sana na karibu zote kama sio zote zinajengwa separately.

Or else, labda bandari kwa ajili gas exports ijengwe Lindi na hiyo ya Bagamoyo iende Mtwara! Na Lindi nako labda watafute eneo lingine kwa sababu ilipo bandari ya sasa hata meli za kawaida ni issue kutia nanga!!! Nadhani ndio bandari yenye kina kidogo kuliko zote hapa Tanzania!
 
Kuna uzuri mmoja. Naamini sisi sio nchi ya kwanza kuwa na project za aina hii. Wenzetu walionufaika kama nchi walifanya nini? Ni nchi gani hizo? Tungeanzia hapo ingekuwa muafaka sana.

Hatuhitaji kuvumbua kitu, ni kuiga kwa waliofanikiwa lakini kwa kuakisi mazingira yetu na mahitaji yetu. Pamoja daima
 
Bonge la point. Kujadili vitu vilivyo fichika ni kazi ngumu mno. Ni kama haiwezekani kabisa. Watu mnaishia kukisia tu. Kuna masharti gani humo?
Dah, yaani mtu ameweka hisia zake zinazotokana na hearsay wewe umeona point? Jamani msiangalie mwenzangu anapata nini siku zote angalia wewe unapata nini. Anyway, nchi yenu hiyo fanyeni mtakavyo.
 
Mlilalamika hapahapa jf kuwa huu mradi wa Bagamoyo port JK kaupeleka kwao wakati hauna mantiki kwa taifa,mbona leo mmekuwa vigeugeu namna hii??
 
Dah, yaani mtu ameweka hisia zake zinazotokana na hearsay wewe umeona point? Jamani msiangalie mwenzangu anapata nini siku zote angalia wewe unapata nini. Anyway, nchi yenu hiyo fanyeni mtakavyo.

Mkuu, wewe unajua masharti yote kwenye huo mkataba yakoje?
 
Watanzania tumeathirika na ndumba nyingi na ulozii,watu hawapendi mafanikio kila siku mtu atafurahi ukibaki kama ulivyo huna chochoteee......
Ufe tu huo mradi, hauna manufaa.
Hizo hela kama zipo basi zikarabati Bandari ya Tanga na ya Mtwara
 
Hahahaa, nimecheka sana. Yumkini huna ufahamu wa mikopo ndio maana unasema hivyo, mbali ya ugumu wa kumthibitishia mkopeshaji kwamba project yako ina payback period nzuri na viable, madudu ya mikopo hii ya kimataifa ni hatari kuliko hata hiyo BOT.

Wewe jiulize, toka tuanze kukopa deni linapungua??? Unaona miaka 50 mingi? IPTL mliongia ina muda gani sasa, manufaa yake nini? Utalinganisha IPTL na bandari? Ni woga na kutofuatilia mambo tu yalivyo duniani ila hiyo miaka si mingi as long negotiated terms zitazingatiwa.
Miaka 50.midogo? :oops: :oops: :oops: :oops: :oops: :oops: :oops: :oops: :oops:
 
Kuna watu wanatetea humu.ukiwauliza ile mikataba ilisainiwa kwa ajili ya nini?au kulitokea tukio gani hadi China na kikwete waingie ile mikataba hamjui.
 
Balozi wa Chinanchini, Dk Lu Youqing amesematofauti kati ya Serikali ya Tanzania na ubalozi wa China umesababisha kukwama kwa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo mkoani Pwani.

Mchakato wa ujenzi wa bandari hiyo ulianza kipindi cha Awamu ya Nne ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete na ulitarajiwa kuhusisha Serikali za Tanzania, China na Oman.

Akizungumza katika mahojiano na baadhi ya waandishi wa habari juzi jijini Dar es Salaam, Balozi wa China nchini, Dk Lu Youqing alisema, “Mradi wa Bandari ya Bagamoyo na ukanda wa viwanda wilayani humo ni uwekezaji mkubwa kati ya China na Tanzania katika miaka ya karibuni na umeorodheshwa katika Mpangowa Maendeleo wa Miaka Mitano(2016/17-2020/21).

“Kutokana na umuhimu wake unaohusisha Serikali za Tanzania, China na Oman, ushirikiano kati ya maofisa kutoka idara za Serikali ya Tanzania na ubalozi wa China wanazishauri pande zinazohusika kukunjua moyo nakumaliza tofauti ili uweze kuendelea kukiwa na makubaliano kwenye mambo yamsingi,” alisema Lu.

Hata hivyo, kwa sasa jitihada zinafanywa ili ikiwezekana makubaliano hayo katika nusu ya mwaka huu na ujenzi uanze ndani ya mwaka huu.Akizungumzia hilo kwa njia ya simu jana, Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Edwin Ngonyani alikiri kutofatiana na Wachina katika ujenzi huo.

“Unajua vitu vingine mnapenda kuvikuza bila sababu.

Sisi tuliiruhusu Serikali ya China kujenga Bandari ya Bagamoyo kwa kitu kinachoitwa PPP na uleujenzi ulikuwa na mambo mengikama maeneo ya viwanda ili kupata uhakika wa mizigo.

Wachina wakatuletea kampuni kwamba sasa ongeeni na kampuni hii, tukawa tunaongea tunaangalia terms au unataka tuwape hivi hivi? Alihoji.

Waziri Ngonyani alisema baadaye Wachina walileta Serikali ya Oman kwenye mradi huo.“Hivyo vingine vyote wanatafutatu sababu ya kutuchelewesha.

Mara ya mwisho tumewaambia lazima yale maeneo tuliyobishania tukubaliane ifikapo Februari 28. Kwa hiyo tunatarajia kupata taarifa ya mwisho ya ujenzi wa bandari hiyo kutoka kwa contractors wa China na Oman,” alisema.

Chanzo : Mwananchi Online
Hapa ndipo napomkubali Rais Magufuli kwa nguvu zote na MUNGU AMFANYIE WEPESI KATIKA KAZI ZA MIKONO YAKE yaani hainiingii akilini Tanzani tumejaaliwa Bandari kuuubwa na yenye kina kikuubwa pale Mtwara kuna ya Tanga haya hii ya hapa karibu na Ikulu dar es salaam badala ya kuboresha hizo eti tukajenge nyingine tena ikachimbwe kuongeza kina hata malaika walio Mbinguni wangetushangaa sana UZALENDO KWANZA MENGINE baayae
 
Huo mradi una manufaa sana sema watu tunauangalia kwa macho ya makengeza!!!

Kwa mfano kuna watu wanahoji suala la China kutaka kuendesha mradi kwa 40 years kabla hawajatuachia bandari yetu!!!

Hapa tunasahau bandari ya Dar es salaam ipo tangu mkoloni na bado inapiga mzigo kama kawaida!! Kwahiyo wala si kwamba baada ya 40 years haitakuwa tena bandari!!!

Lakini kubwa zaidi, hata kama wataendesha bandari kwa muda wote huo; bado kodi zetu zitakuwa pale pale!! Hata ukienda Bandari ya Dar es salaam, anayeongoza kuchukua mapato ya kufuru sio mamlaka ya bandari bali TRA ambao nao pia watakuwa bandari ya Bagamoyo kama kawaida kwa sababu, China kuendesha bandari haimaanishi hata kodi watachukua wao; no!

Na kwa kuangalia import and export targets za China, kuna uwezekano mkubwa sana bandari itakuwa busy sana kwa mizigo inayoingia na kutoka na hivyo kuzidisha mapato ya kodi maradufu!!!
Kwani bandari ya dar haiingizi na kupeleka mizigo ya uchina?
 
Hapa ndipo napomkubali Rais Magufuli kwa nguvu zote na MUNGU AMFANYIE WEPESI KATIKA KAZI ZA MIKONO YAKE yaani hainiingii akilini Tanzani tumejaaliwa Bandari kuuubwa na yenye kina kikuubwa pale Mtwara kuna ya Tanga haya hii ya hapa karibu na Ikulu dar es salaam badala ya kuboresha hizo eti tukajenge nyingine tena ikachimbwe kuongeza kina hata malaika walio Mbinguni wangetushangaa sana UZALENDO KWANZA MENGINE baayae
Unamkubali vipi katika hili, kwa sababu bandari nyingine zipo? hata kama ni hivyo kuna ubaya gani tukaongeza nyingine, na je unadhani hata hili la bandari ya bagamoyo lisipofanikiwa ndio kwamba zingine ndio zitaboreshwa zaidi??

Back
Top Bottom