Serikali ya China kupiga marufuku vazi la Hijab

sexologist

JF-Expert Member
Dec 5, 2010
2,283
976
Hii sasa kali, Tanzania tusifike huko wala tusiwaze kabisa..

Serikali ya China kupiga marufuku vazi la hijaab

Serikali ya China imeanzisha sheria ya kutaka kupiga marufuku vazi la hijab kwa Waislamu wa jimbo la Xinjiang wanapokuwa nje kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kupambana na "siasa kali za Waislamu"

Sheria hiyo imekuja wakati serikali ya China ikiendelea na kampeni yake dhidi ya "siasa kali" zinazodaiwa kusababisha ghasia zilizopelekea mamia ya watu kufariki katika kipindi cha miezi 20 iliyopita.

Jimbo la Xinjiang lina idadi kubwa ya Waislamu wa asili ya Uighur ambao wamekuwa wakilalamika dhidi ya utawala wa kidhulma wa kichina unaowafanya Waislamu hao kunyimwa fursa za kiuchumi katika jimbo hilo.

Wataalamu wa masuala ya dini wanasema ufugaji ndevu na kuvaliwa kwa hijab hakuashirii chochote juu ya "siasa kali" bali ni utamaduni wa Kiislamu.

Wamesema hatua hiyo ya kuwapiga marufuku Waislamu" zinaweza kuwatia hamasa Waislamu wa Uighurs. Sheria ya kuwavua wanawake wa Kiislamu hijab imepingwa vikali na Waislamu wa Xinjiang.

Mwezi wa August mwaka huu, mji wa Karamay ulioko Kaskazini mwa Xinjiang ulitangaza kuwa wanaume wenye ndevu na wanawake waliovaa burgas au hijab hawataruhusiwa kupanda mabasi.

Polisi wa China wamekuwa wakivamia maduka mjini Xinjiang na kutaifisha mabuibui. Pia serikali imekuwa ikiwalazimisha wanafunzi wa Kiislamu kula mchana wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Serikali ya China imekuwa ikifanya kila juhudi kutaka udhalimu huu wanaowafanyia Waislamu usijulikane hasa katika mataifa yenye Waislamu.

Kwa mfano serikali ya China imekuwa ikisaidia vyombo vya habari vya Zanzibar ili visaandike habari kama hizi.

Pia imekuwa ikiwapa nafasi waandishi wa habari wa Zanzibar kutembelea China ili wasije wakathubutu kuandika kitu chochote dhidi ya serikali ya China.

Machina wanajifanya ni marafiki sana ili kuficha udhalimu wao wanaowafanyia Waislamu wenzetu.

Chanzo: Mzalendo.net
 
Ni chombo gani cha habari Zanzibar kinavuka mipaka? Hiho ZtV hata hapa bongo haishiki sembuse kuhabarisha dunia!!!
 
Mugu atabaki kuwa mungu
Jadiri mada na x kugusa dini ya mtu kwani dini zipo mungu yupo sie tupo na shetani pia yupo na hivi vyote vita zidi kuwepo hadi yesu atakapo rudi..Asantn na tujadiriane mada
 
kasome history vizur ujue mambo,kaangalie warumi waliyofanya kwa wayahudi, ivi unafikiri ukristo ulianza anza tu....waislamu duniani hawatakaa kimya kama mkiwachokoza kwa kile wanachokiamini, mkitaka amani basi itangazeni hiyo amani,na kwa taarifa yenu ambayo hamuijui ni hivi.....waislamu hii dunia wala hatuna maslahi nayo, maana hayajakuwa maisha ila ni upuuzi(wamal hayatal dunia ila matama ghurui)
 
zile ninja hazifai jamani alafu akiamua kujifunga vilipuzi utamjuaje?
 
Hiv kwa nini almost kila sehemu vurugu za kidini lazma waislam wahusike tu?
CHINA: Waislamu vs wabudha.
INDIA: Waislam vs wahindu.
AFRICA: Waislam vs Wakristo.
UARABUNI: Shia'h vs Sunni.
ISRAEL: Waislam vs Wayahudi.
SIRILANKA: Waislam vs (nimesahau).
Alafu eti kote wanadai wao wanadhulumiwa na vijiushahid vya kuunga unga, haya hata wao kwa wao hapakaliki bila m1 kuwatawala mwenzie kwa mabavu eg. Taliban(Afghanstan), Saddam (Iraq), Alshabab(Somalia), Abdullah (Saudia), Mubaraq (Misri)etc
 
Nawaunga Mkono Wachina maana ukiachia watu wanatembea mtaani wamejifunika uso mzima itakuwa ngumu sana kumtambua Gaidi.
 
Hiv kwa nini almost kila sehemu vurugu za kidini lazma waislam wahusike tu?
CHINA: Waislamu vs wabudha.
INDIA: Waislam vs wahindu.
AFRICA: Waislam vs Wakristo.
UARABUNI: Shia'h vs Sunni.
ISRAEL: Waislam vs Wayahudi.
SIRILANKA: Waislam vs (nimesahau).
Alafu eti kote wanadai wao wanadhulumiwa na vijiushahid vya kuunga unga, haya hata wao kwa wao hapakaliki bila m1 kuwatawala mwenzie kwa mabavu eg. Taliban(Afghanstan), Saddam (Iraq), Alshabab(Somalia), Abdullah (Saudia), Mubaraq (Misri)etc

Na ukristo unahusika na nini?hebu orodhesha
 
sasa si muondoke mtuachie....achenj kutusumbua

Back
Top Bottom