Lituye
JF-Expert Member
- Dec 27, 2015
- 1,862
- 5,680
Mkurugenzi wa Manispaa ya Temeke iliyopo Jiji la Dare Salaam Bwana Mwakibibi, ameagiza watumishi wote wa halmashauri hiyo kuchangia pesa za Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa na matundu ya vyoo katika harambee ambayo ameiandaa mwishoni mwa mwezi huu.
Akiongea katika kikao na walimu wake jana, mkuu wa shule mmoja jina tunalihifadhi aliwaeleza kuwa "tumeagizwa kila shule kuchangia laki mbili. Hivyo tutazigawa hizi lakimbili kwa idadi ya walimu tuliopo kisha tutajua kila mtu atachanga kiasi gani".
Aidha mkuu huyo alieleza kuwa Wakuu wa Idara wote wa halmashauri hiyo wameagizwa kutoa Milioni moja kila mtu na wasaidizi wao kutoa laki tano. Pia watumishi wengine wote kila mtu atachangia kiasi kisichopungua elfu kumi.
Harambee hiyo inatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mlimani City mwisho wa mwezi huu wa tatu na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais Mstaafu ndugu Jakaya Mrisho Kikwete.
Jambo la kushangaza zaidi kama sio vichekesho ni kuwa taarifa zinanyetisha hata bwana yule mnunua midege kwa pesa taslimu huku akiacha Wanafunzi wakijisaidia vichakani na kusomea chini ya miti na wengine kukosa mikopo elimu ya juu eti naye atakuwepo kuchangia harambee.
Huu ni ukatili mkubwa kwa watumishi wa umma hapa nchini kuwalazimisha kuchangia michango bila hiari yao. Watumishi ambao hawajapandishwa mishara takribani miaka mitano sasa wanaishi maisha magumu. Huku wengine wameongezewa deni la bodi ya mikopo elimu ya juu wanapewa mzigo wa kuisadia Serikali inayo jitapa kuwa inazo hela za kutosha.
Vyama vya wafanya kazi vipo kimya kabisaa vinaangalia tuu maagizo haya ya kinyama kwa watumishi wa umma yakitekelezwa.
Maendeleo hayana vyama.
Sent using Jamii Forums mobile app