Serikali ya CCM yaingilia kati mgogoro wa Chadema, CCM

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
CCM11.jpg
CHADEMA.png


Fredy Azzah, Dar na Venace George, Kilosa

SERIKALI imesema itafanya uchunguzi juu ya baadhi ya vyama vya siasa na wanasiasa wanaodaiwa kupata fedha chafu kutoka kwa taasisi na watu binafsi walio nje ya nchi.

Kauli hiyo imekuja baada ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, kukituhumu Chadema kwamba kinapewa fedha chafu na wafadhili wa nje.

Wakati Nape akiibua tuhuma hizo, Katibu mkuu wa Chadema , Dk Willibroad Slaa wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika jimbo la Kilosa mkoani Morogoro juzi jioni, alisema fedha chafu ndiyo zilizomuweka Nape madarakani.

Akizungumza wakati akijibu swali la Mbunge Jimbo la Nkasi Kaskazini kupitia (CCM), Ali Kessy aliyetaka kujua Serikali imejipanga vipi kudhibiti vyama na wanasiasa wanaopata fedha chafu kutoka nje ya nchi.

Kessy aliuliza swali hilo katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu, ambapo alisema wezi wa magari na fedha chafu, sasa wameingia kwenye siasa na wanapata fedha hizo kutoka kwa watu binafsi na taasisi mbalimbali kutoka nje ya nchi.

Swali hilo lilionekana kuilenga Chadema kwa kuwa Agosti 11 Chadema chama hicho kilifanya harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kuendesha kampeni ya vuguvugu la mabadiliko (M4C).

Mara baada ya harambee hiyo, Nape alisema Chadema kinafanya kampeni za kuchangisha fedha ikiwa ni kuhalalisha mabilioni ya fedha wanazopewa na wafadhili wa nje ya nchi.

Alisema mkakati huo unafanywa kwa siri na wafadhili hao kuchochea machafuko nchini ili wafaidi kirahisi raslimali za Tanzania kama vile madini, gesi na mafuta ambayo yamegundulika kuwepo nchini.

Kauli hiyo ya Nape iliifanya Chadema kupitia kwa Mkurugenzi wake wa Fedha na Utawala, Anthony Komu kushitaki kwa Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, kumtaka Nape atoe maelezo juu ya madai yake.

Lakini jana, Pinda bila kutaja makundi hayo yanayolumbana, alisema serikali imepata taarifa hizo kupitia mtandao na imeamua kutozipuuzia na kuamuru vyombo vinavyo husika vifanye uchunguzi.

"Nadhani tuseme Serikali imejipanga kuchukua hatua stahiki gani, ni kweli kuna taarifa kama hizi kwenye mtandao, lakini tatizo langu ni kwa kiasi gani tunaweza kuziamini hizi taarifa kwa sababu hapa ni sehemu ambapo kila mtu anaweza kuandika kile anachojisikia," alisema Pinda na kuongeza;

"Lakini tumeona tusizipuuze na tumeagiza vyombo vinavyohusika vizichunguze juu ya fedha hizo chafu."

Nnauye akitoa tuhuma hizo alisema, CCM kimeshangazwa kuona Chadema kikiwahadaa Watanzania kufanya harambee ili kuhalalisha fedha walizonazo kutoka kwa wafadhili.

"Chama Cha Mapinduzi kimeshangazwa na kusikitishwa sana na usanii mkubwa unaofanywa na Chadema kwa kuwahadaa Watanzania kwa usanii wa kufanya harambee kuhalalisha uwepo wa mabilioni waliyopewa na wafadhili wao wa nje ya nchi."

Aliongeza; "Mfano mzuri wa usanii huu ni juzi siku ya Ijumaa (Agosti 11) kwenye Hoteli ya Serena ambapo ilifanyika harambee na kurushwa moja kwa moja na kituo kimoja cha televisheni."

Alisema CCM inao ushahidi wa kutosha unaoonyesha mabilioni waliyopewa Chadema na wafadhili kutoka nje ya nchi kwa lengo la kuendeleza operesheni mbalimbali nchini.

Alionya kuwa fedha hizo zinatokana na watu mbalimbali wanaomezea mate raslimali za Tanzania.
"Hebu tujiulize, kwa nini mabilioni haya yanatolewa kwa Chadema sasa ambapo nchi yetu imeendelea kufanya utafiti na ugunduzi wa rasilimali mbalimbali zikiwamo gesi na mafuta?

"Je, ufadhili huu kwa Chadema licha ya kufichwa sana na kufanywa siri, una nia njema kwa nchi yetu na rasilimali za nchi yetu? Kwanini ufadhili huu wa mabilioni unafanywa siri ya watu wachache hata ndani ya chama chenyewe?"

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema, Komu, akizungumza na gazeti hili kuhusu madai yaliyotolewa na Nnauye, alisema chama chake, hakijawahi kufadhiliwa na wahisani kutoka nje na kwamba mapato yake yanatokana na ruzuku ya Sh235 milioni inayotolewa na Serikali kila mwezi.

Kauli ya Dk Slaa

Dk Slaa alisema Nape hana uhalali wa kufikiria kuwa kuna vyama vina takatisha fedha chafu kwa kupitia michango ya wananchi na badala yake anapaswa kuwaambia wana CCM wenzake namna Chama hicho kilivyotumia fedha chafu kuingia madarakani mwaka 2005.

"Nimemsika Nape akiendeleza madudu yaliyo kichwani mwake kuwa alikuwa anatoa tahadhari tu sasa ninamwambia Yule si saizi ya Chadema na Dk Slaa zaidi ninamkumbusha kuwa Fedha za Tangold, Kagoda na Meremeta ndizo zilizokiingiza chama chake madarakani hivyo awape tahadhari hao badala ya wananchi wanaokichangia Chadema kwa mioyo yao ya kutaka kujikomboa"alisema Dk Slaa

Alisema wameshamwandikia msajili wa vyama vya siasa amtake Nape na CCM wathibitishe namna Chadema inavyopata fedha chafu na kama ikishindikana basi jeshi la Polisi limchukulie hatua kwa kuwa ni kauli za uchochezi na chuki dhidi ya watanzania.

Aliongeza kuwa ni jambo la kusikitisha kuona mkuu wa Polisi nchini IGP Said Mwema na timu yake wameshindwa kuchukua hatua za awali wakati kuna mtu ana ushahidi wa kuthibitisha namna fedha chafu zinavyoingia nchini.

"Sitaki kuamini kama IGP ana maslahi katika hili lakini pia sisiti kuamini kuwa hii si kauli ya Nape ni ya kiongozi wake mkuu katika Chama, sasa kwa hili wanazidi kutudhihirishia kuwa nchi imewashinda kwa kuwa kuna vyombo vya usalama vinavyoongozwa na serikali ya CCM vimeshindwa kuchukua hatua na kuudhihirishia umma ukweli unaosemwa na Nape"alisema Dk Slaa.


Mwananchi
 

Nakumbuka walisha sema Mzee Malecela na pia JK Kikwete walisha pewa pesa toka Iran... Kulikuwa hakuna wa kuchunguza

Kwasababu POLICE nchini sio TRANSPARENCY kama POLICE mfano USA, ENGLAND, KENYA sababu zinachungwa na KATIBA zao

kufanya kazi Sasa Angalia POLICE ya CCM inaichunguza CHADEMA; Lakini POLICE ya CCM haichunguzi ni nani amewekeza pesa

USWISI sababu ni CCM
 
Hadithi njoo uongo njoo utamu kolea....Nafikiri wananchi wanaelewa kinachoendelea na nini hatma yao, hawahitaji kauli
ya mtu yeyote kwa hivi sasa ili waamini.
 
Pia Pinda asisahu kuchunguza wabunge WAUZA UNGA kama Munde Tambwe
 
ninamkumbusha kuwa Fedha za Tangold, Kagoda na Meremeta ndizo zilizokiingiza chama chake madarakani

kauli hii kila anapoitamka dr.slaa dhaifu anapandisha presha
 
mm nadhan badala ya kuanza kuhangaika na mengine wangeanza na zile zilizoko uswisi na kuwataja wenye nazo sio wanaanza kutuletea siasa kila mahali tushachoka na kauli za liwalo na liwe
 
Chadema wameumbuka big tyme wameufyata wameguswa

Kama ni kweli, walioumbuka wanafaida kwa nchi yetu maana wameingiza pesa za kigeni nchini mwetu na hivyo kuukuza uchumi wetu. Lakini Magamba yameweka hela Uswisi kuukuza uchumi wa Uswisi. Cha ajabu policeccm ambao hawjafaidika kitu kwa Magamba kuficha matrillioni Uswisi wanashabika kuwafainyia uchunguzi CHADEMA walioingiza pesa za kigeni kukuza uchumi wetu. Mapoazi zinakutosha kichwani?
 
mm nadhan badala ya kuanza kuhangaika na mengine wangeanza na zile zilizoko uswisi na kuwataja wenye nazo sio wanaanza kutuletea siasa kila mahali tushachoka na kauli za liwalo na liwe

Mkuu Kijereshi, hii ni janja ya Magamba kujaribu mlango wa kutokea kwenye kashifa ya mihela yao ya kifisadi waliyoificha Uswisi.
 
Chadema wameumbuka big tyme wameufyata wameguswa

Kweli Unaweza kusema hivyo na kulala kitandani bila kung'atwa ng'atwa na kunguni kwa kifisadi? yaani kweli CCM wamekufanya wewe kipofi na kiziwi?

Kweli Nchi yetu imeisha mpaka uone wazazi wako na ndugu zako wanakuja kwako hawana ARDHI ndipo utajua CHAMA CHAKO kilikuwa kinakubomoa eti?

AU ndio Wasomi wa CCM nyie? Be Real, Kukosoa Chama Chako sio kuwa Mpinzani; Ni kukifanya kiwe bora... Sasa Kweli Walipokuwa wanaongea bungeni

Kuhusu wewe kukatiwa UMEME na Wabunge wako wa CCM ili wawe Matajiri haikukuuma? au uliona ni cha kawaida; kuwasha kibatari na Mishumaa?
 
Ivi unaakili kweli?unajua cdm ni nini? Ngoja nikueleze,... Ndo chama chenye wanachaama wengi tz kuliko chama chochote,.. Mengine muongezeeni huyu mb. Pande
Chadema wameumbuka big tyme wameufyata wameguswa
 
Mkuu unazungumza na kiwiliwili... una moyo wewee dah! Tuna wenzetu wengi sana humu walishauza vichwa vyao na wengine waliomua kwa makusudi kuvitumia EXCLUSIVELY kufugia nywele. Watch out!

Kweli Unaweza kusema hivyo na kulala kitandani bila kung'atwa ng'atwa na kunguni kwa kifisadi? yaani kweli CCM wamekufanya wewe kipofi na kiziwi?

Kweli Nchi yetu imeisha mpaka uone wazazi wako na ndugu zako wanakuja kwako hawana ARDHI ndipo utajua CHAMA CHAKO kilikuwa kinakubomoa eti?

AU ndio Wasomi wa CCM nyie? Be Real, Kukosoa Chama Chako sio kuwa Mpinzani; Ni kukifanya kiwe bora... Sasa Kweli Walipokuwa wanaongea bungeni

Kuhusu wewe kukatiwa UMEME na Wabunge wako wa CCM ili wawe Matajiri haikukuuma? au uliona ni cha kawaida; kuwasha kibatari na Mishumaa?
 
Dah, ha ha haa, hizi kweli ni tamthilia za kichina. Uchunguze nini wakati serikali yako ndo inahusika kwa asilimia kubwa na fedha chafu? Kweli NYANI HAONI KUNDULE, CCM imeoza!
 
Mkuu unazungumza na kiwiliwili... una moyo wewee dah! Tuna wenzetu wengi sana humu walishauza vichwa vyao na wengine waliomua kwa makusudi kuvitumia EXCLUSIVELY kufugia nywele. Watch out!

Una Maana Gani kusema Watch Out!!
 
Kuhusu kikwete kama mnakumbuka Kuna gazeti la Uingereza lilisema wazi kama amepewa pesa ya kampeni kutoka Iran. Jamani hii kumbukumbu atukumbushe na ikadaiwa kwamba kikwete atawashtaki hao jamaa wa gazeti lauingereza vipi hadi leo mbona kimya hebu tukumbushane. Polisi haiko huru kabisa, uchunguzi wake hauaminiki. CCM wajisafishe kwanza, kabla ya kujidai wanafahamu sana habari za wenzao. Nape ni mchemfu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom