Serikali ya CCM yafanya kila mbinu kuikandamiza CHADEMA! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali ya CCM yafanya kila mbinu kuikandamiza CHADEMA!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by RealTz77, May 17, 2011.

 1. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #1
  May 17, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Tumesikia jinsi serikali inavyotaka kudhibiti ukuaji wa CDM na kuwabana mbavu wasipumue

  1. Marufuku kufanya mikutano ktk maeneo km mnazi mmoja, kidongo chekundu etc ati hata makongamano au maadhimisho yoyote.( wanalengwa CDM wakiingia na maandamano Dar)

  2. wizara ya elimu imepiga marufuku wanasiasa kwenda vyuoni kueleza sera zao na kupata wafuasi ( vyuo vyote ccm haikubaliki hivyo hapa tena CDM wanalengwa)

  3. Mengine mengi tu tutayasikia!! japo mi nasema haisaidii hii TZ kwa sasa ni PP (Peoples Power)!
   
 2. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #2
  May 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Source please!
   
 3. Steve Dii

  Steve Dii JF-Expert Member

  #3
  May 17, 2011
  Joined: Jun 25, 2007
  Messages: 6,416
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Ni serikali hiyohiyo ya CCM iliyo achia ujenzi holela katika jiji la Dar ufanyike. Viwanja vya michezo, mashule na maeneo ya kupumzikia karibia yote yameuzwa na kujengwa vitega uchumi vya watu binafsi.
   
 4. m

  mkulimamwema Senior Member

  #4
  May 17, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wahenga walisema mfa maji haachi kutapatapa
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  May 17, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,120
  Trophy Points: 280
  bujibuji tu amewashinda, je wataiweza Chadema?
   
 6. Amiliki

  Amiliki JF-Expert Member

  #6
  May 17, 2011
  Joined: May 6, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Hili la Jimbo la vyuo vikuu la CCM liangaliwe upya Send to a friend Thursday, 29 July 2010 11:37 0diggsdigg

  HIVI karibuni Chama cha Mapinduzi katika mkutano wake mkuu uliofanyika mjini Dodoma, walikubaliana kuunda jimbo maalumu kwaajili ya wanafunzi wa vyuo vikuu nchini.


  Kwa maana hiyo wanafunzi wa vyuo vikuu sasa watakuwa na nafasi yao katika Halmashauri kuu ya CCM na watakuwa na uongozi kama ilivyo kwa mikoa mingine.


  Hata alipokuwa katika mkutano wa kuwatambulisha wagombea urais wa chama hicho jijini Dar es Salaam, Rais Kikwete alitambulisha pia jimbo hilo.


  Hii ni njia mojawapo ya CCM kuwavuta wanafunzi waendelee kukipenda chama hicho.


  Siyo kwamba napinga wanafunzi wasishiriki siasa moja kwa moja, lakini naona sasa wanafunzi hasa walio wanachama wa CCM watashindwa kutenganisha muda wa masomo na shughuli za siasa.


  Nasema hivyo kwasababu, kuanzishwa kwa jimbo hilo pia kutaendana na kazi kama vile kuchagua uongozi, kutafuta wanachama, kuanzisha matawi na shughuli nyingine za kichama.


  Kwa mwanafunzi anayekabiliwa na masomo, ataweza kweli kuzingatia masomo hasa kama ni kiongozi wa chama ndani ya chuo?


  Jambo la pili ni ushabiki wa vyama ambao unaweza kuwafanya wanafunzi washindwe kujifunza. Kama wale wanafunzi wanaosoma Sayansi ya siasa, kama mhadhiri anaeleza mapungufu ya chama chao, watamwelewa, au watamwona kama ana chuki na chama hicho?


  Pamoja na kwamba baadhi ya wanafunzi wamelipokea suala hili kwa shangwe, wajue litakuja kuwaangamiza. Kwanza wangejiuliza, CCM hii iliyoshindwa kuwalipia ada, leo watu wanabaguliwa kwa matabaka kupewa mikopo ya elimu, kuanzishiwa jimbo ndiyo suluhisho?


  CCM inataka kutumia migongo ya wanafunzi wa vyuo vikuu kushinda uchaguzi, kisha itawatelekeza.


  Jumanne Madiga
  Dodoma

  Nimenukuu tu hiyo Habari ya CCM.

  Leo hii wameona wanafunzi wa vyuo vikuu hawaitaki tena CCM wanaitaka CDM ndo wanakuja na Mikakati ya Kijinga kama hiyo!
   
 7. s

  sawabho JF-Expert Member

  #7
  May 17, 2011
  Joined: Feb 25, 2011
  Messages: 4,504
  Likes Received: 946
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka ile miaka ya 90 matawi ya vyama vya siasa yalizuiliwa katika ofisi za Serikali na Mashuleni, je hii ya Jimbo maalum kwa ajili ya Vyuo vikuu ni tofauti matawi ya vyama vya siasa mashuleni?
   
 8. RealTz77

  RealTz77 JF-Expert Member

  #8
  May 17, 2011
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 742
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  just google utapata
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #9
  May 17, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Doesn't this pronouncement violate the right of people to freely assemble as stipulated in our constitution?

  This with reference to banning people not to assemble at both Jangwani and Kidongo chekundu grounds unless vetted by CCM functionaries.
   
Loading...