Serikali ya awamu ya tano ya mwenyekiti Dr magufuli inaumbuliwa kwa kasi. kinachoendelea nchini katika utawala huu na siasa zetu si hakikisho la amani na utulivu kama ambavyo watu wa imani na wanadini wanavyopiga kelele lakini naweza kusema inabebwa tu na busara na USTAARABU wa upinzani wa nchi hii.
Tulipo ni pabaya sana. Leo viongozi wa serikali wanapojipambanua kuvunja taratibu za wazi za chaguzi na kukaribisha mazingira ya uvunjifu wa amani bila kukemewa na viongoziu wa juu basi ujuwe ngoma inogile.
Uchafuzi huu wa chaguzi za marudio na kasi ya kile kinachoitwa wapinzani kujiuzulu na kummunga mkono rais na kuwepo taarifa za hujuma na mianya ya kifisadi wa kisiasa kufanywa mchana kweupe, kuvunjwa taratibu, Polisi kutumika kunyanyasa wapinzani kweupe si kuumbukuka kidogo kwa CCM na serikali yake.
CCM NA SIKIO LA KUFA.
Nchi inateketea kidogo kidogo kwa kupandikizwa chuki, CCM na tabaka tawala linafurahia kwa sababu ya maslahi yao. Vyombo vya dola kutumika kuharibu taratibu za chaguzi si jambo dogo. Viongozi wa serikali wakiwemo NEC na wakurugenzi wa halmashauri kutumika kuharibu taratibu wazi wazi si jambo jema kwa nchi. Tunataka tuwaulize wale CCM walio huru kiakili na maarifa hivi kweli leo CCM inapendwa kweli kweli kama tunavyoaminishwa ?
Mbona CCM inaimarishwa kwa misingi ya kuharibu taratibu za nchi na kwa kutumia mbeleko ya dola jee huku ndio kukubalika ?
Nani amseme mwenzake kuhusu huu ukimya wa viongozi wa juu na kinachoendelea kila kukicha?. CCM na uongozi wa dr Magufuli haukutosheka na kuzuia maandamano na mikutano ya kisiasa ya vyama ya wazi tu, lakini sasa inatumia vyombo vya dola na taasisi za serikali kuwahujumu wapinzani wazi wazi.
Mazingira yaliyopo hayaipi nafasi CCM kukubalika ndani ya nafsi za watu na kulazimishwa huku kwa nguvu za dola ni hatari sana kwa CCM. Juhudi za maarifa za kupandikiza itikadi sahihi za chama zilizofanywa na waliopita zinaharibiwa na viongozi waliopo leo madarakani. Hiki ndicho kifo cha CCM pale itakapofika siku mazingira yakibadilika. Pengine CCM hawaamini kuwa ipo siku mazingira yatabadilika.
Utafanye chaguzi kwa kukiuka taratibu na kuifanya CCM ishinde bila kupingwa ukiamini hicho ndicho kipimo sahihi cha kukubalika CCM?
Utatumiaje polisi kudhibiti wale wanaotaka taratibu zifuatwe ukiamini hizo ndio mbinu za kukifanya chama kukubalika kwenye jamii? SIKU CCM WAELEWA WAKISHTUKA TUTASHUHUDIA ZAIDI YA HAYA AKINA NAPE. Poleni CCM, nchi inaelekezwa kubaya kwa mikono ya wakubwa wenu na mnanyamaza kimya.
BUSARA HEKIMA AU ULEGEVU WA WAPINZANI ?
Watu wanahoji na kuwalaumu wapinzani kuwa labda wamelemaa sana. Mbinu za wapinzani za kutumia njia iliyopo leo inawafanya CCM wajianike wakiamini wameshawadhibiti wapinzani na wamefanikiwa kwa kuiacha CCM na serikali yake ijichore na kujidhihirisha MBELE YA DUNIA kuwa kweli inavunja haki za binadamu na kutoheshimu demokrasia. CCM imejiachia na dunia inashuhudia hilo sasa.
Wasioona mbali wanadhani kuwa mambo ni shwari. Mimi naona kama wapinzani wamefanya 'timing" tu. Hiki kinachoendelea hapa nchini bila ya kufanyiwa kazi basi mbele kuna giza nene. Naitafakari miaka hii mitatu ya Rais Magufuli kama Pilot kwa wapinzani. Naiona kama wametowa mwanya kwa watawala wajitafakari kwa haya wanayoyatenda. Picha imepatikana na naamini WATAALAMU NA WASOMI WA UPINZANI WATAKUJA NA JIBU HAPO BAADAE.
Tunachokiona kwa sasa walau hawa wapinzani wamekuwa waungwana sana kwa kutanguliza maslahi ya taifa ya kulinda amani na utulivu kwa vitendo kwa kutumia maarifa makubwa kutokubali kuingizwa kwenye mapambano ya kiuchokozi ya wazi. Nadhani wanajuwa walitendalo.
JEE HALI HII ILIPO ITAENDELEA HIVI MILELE ?
si dhani kuwa ni hivyo, kwanza hali hii inaipa picha Dunia nini kifanyike kuelekea uchaguzi wa 2020.Wapinzani wamefanikiwa kuionesha Dunia namna CCM na serikali ya dr Magufuli ilivyo. Lengine sidhani kuwa wapinzani hawana njia mbadala sidhani. La msingi watangulize maslahi ya taifa kwa kutumia mbinu zote zinazostahiki lakini....................
KUUMBUKA KWA SERIKALI NA CCM
wenyewe kujidhihirisha kuwa hawajali malalamiko yaliopo na kushindwa kuyafanyia kazi malalamiko ya chaguzi ndogo na kujirudia kila wakati.
Viongozi kutowa lugha tata na kuachia wasaidizi wao kuvunja taratibu bila kukemea na bila kuchukuliwa hatua
Vyombo vya serikali kugongana wenyewe unapoifika wakati wa kusimamia utatuzi wa jambo kila mmoja kutoa maelezo yake yanayopingana.
Wana CCM kusemana hadharani (baadhi) hii ni kuashiria kuwa kuna mambo hayako sawa.
Viongozi kushindwa kukemea uchafuzi wa wazi wa taratibu(chaguzi) na taratibu nyengine za uendeshaji kwenye mamlaka mbali mbali( kupindisha taratibu kwa maslaHI FULANI)
Wapinzani kuwa kimya na kuacha dhamira za watawala kutimia huku wakijidhirisha watawala peke yao kwa kufanya vitendo vinavyoashiria uvunjivu wa amani
MASWALI MUHIMU.
Jee kukubalika kwa CCM kunaendena na uhalisia au kuna kulazimishwa ?
Kuongezeaka kwa wapinzani kujiunga CCM kwa sasa Jee CCM inakuwa au inakufa ?
Tutarajie hatma gani kwa nchi kutokana na hali halisi ya mazingira ya kisiasa na kiutawala iliyopo?
MWISHO
Tunaamini CCM IMARA itajengwa kwa ustaarabu wa kutumia njia sahihi za kidemokrasia za kutumia ushawishi wa hoja na itikadi na si kwa nguvu na kutumia vyombo vya dola
waswahili wana msemo maarufu "MAPENZI HAYALAZIMISHWI"
Tunahitaji CCM imara, tunahitaji UPINZANI imara ili nchi isonge mbele.
Kishada.