Serikali ya ccm ni nini kinaendelea juu ya haya matukio ya kinyama??/

Eistein

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Messages
1,107
Points
1,195

Eistein

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2011
1,107 1,195
Ndugu zangu

Nimeona leo niulize hilo swali hapo juu,kwa sababu sasa ni zaidi ya wiki/miezi/miaka mingi imepita tangu kutokea kwa matukio ya umwagaji damu, vifo, na ukosefu wa amani katika maeneo mbalimbali nchini.. na punde matokeo hayo yalipotokea viongozi walikuja katika media na kutoa matamko makali sana na kuahidi kuwashughuikia wote waliofanya hayo matukio na watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria haraka sana.

Lakini mpaka sasa mimi binasfi sijui ni nini kinaendelea.. mwenye kujua haya masuala yamefikia wapi awajuze wanajukwaa kwa sababu watu hawa tuliowapa dhamana ya kutulinda wanalipwa mishahara na maslahi mengine kutoka kwenye kodi zetu..na wakati walipopewa dhamani za kazi hizo waliapa kuwatumikia watanzania na kuwalinda na mali zao.. Sasa inakuwaje hawatekelezi viapo vyao.. matukio mengine yanamiaka sasa..??

BAADH YA MATUKIO HAYO NI1. WALIOMTOA UHAI DR MVUNGI WAMEKAMTWA WANGAPI NA WAMEFIKISHWA MAHAKAMA GANI??

2. WALIO MPIGA RISASI SHEKHE PONDA WAMEKATWA WANGAPI NA WAMEFIKISHWA MAHAKAMA GANI?

3. WALIO WAMWAGIA TINDIKALI MABINTI WAWILI ZANZIBAR WAMEKATWA NA WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI??

4. WALIOMUUA MWANDISHI WA HABARI MWANGOSI WAMEKAMWATWA WANGAPI NA KESI INAENDELEAJE?/

5. WALIOLIPUA MABOMU MKUTANO WA CHADEMA SOWETO-ARUSHA WAMEKATWA WANGAPI?? KESI IMEFIKIA WAPI??

6. WALIOTILIISHA MAJI MACHAFU TOKA MGODI WA NORTH MARA KULEKEA MTO TIGITE (MARA) NA KUSABABISHA MIFUGO ISYOPUNGUA 200 KUFA NA KUDHURIKA KWA BINAADAMU WAMEKAMATWA WANGAPI??

7. WALIOMUUA ALLY ZONA (MOROGORO) WAMEKATWA??

8. WALIOFANYA MATUKIO YA KUMWAGIA TINDIKALI SHEKHE NA PADRI (MAUJI) ZANZIBAR WAMEKATWA WANGAPI??

9. WALIOLIPUA BOMU KANISANI OLASITI-ARUSHA WAMEKATWA WANGAPI?? NA KESI INAENDELEAJE???

........
.......
LEO NI ZAIDI YA MIEZI KADHAA IMEPITA NA VIKOSI KAZI VIMEUNDWA MBONA SIJASIKIA RIPOTI YOYOTE?? HAYA YATATOKEA HADI LINI NDUGU ZANGU....??

JE KUNA HAJA YA KUENDELEA KUWACHEKEA WATU HAWA WALIOSHINDWA KUSIMAMIA VIAPO VYAO WANAOLIPWA BURE BILA KUWAJIBIKA ??/

Hapa chini ni picha harisi za matukio hayo

BURNED 1.jpg BURNED 2.jpg shekhe_ponda 2.jpg View attachment 124281 View attachment 124282 View attachment 124283 View attachment 124284 View attachment 124285
 

Forum statistics

Threads 1,391,011
Members 528,343
Posts 34,070,168
Top