Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Katika taarifa ya habari ya ITV nimemsikia waziri Nagu, katika kampeni za Arumeru, akisema kuwa shughuli za maendeleo yaliyopangwa na serikali katika sehemu hizo, yatacheleweshwa (kwa makusudi) iwapo wanachi watamchagua mgombea wa chama cha upinzani. Binafsi mimi nimeona kuwa hii ni 'blackmail' inayofanywa makusudi na viongozi wa serikali ili kuwatisha wananchi na kuwalazimisha wachague mgombea ambao hao viongozi wa serikali wanamtaka. Maendeleo ni ya raia wote bila kujali muelekeo wao wa kichama.