Serikali ya CCM imeshindwa kupambana na wezi na mafisadi wanaparamia wapinzani

radika

JF-Expert Member
Jul 15, 2014
20,427
32,196
Nguvu kubwa inayotumia serikali ya CCM inayojinasabu kupambana na wala rushwa na ufisadi naona pumzi imekata hata wale wezi ambao Mheshimiwa rais Mgufuli aliwataja hadharani kuwa ni wezi wa madini yetu na makinikia hamna kitu tena nguvu zao wamezihamishia katika kuwadhibiti wale wanao wakosoa.

Hii nguvu inayotumika mkoani mbeya kwa mheshimiwa Sugu kwanini isingetumika kuwasaka wale waliolitia Taifa hasara na mikataba ya hovyo walioliingiza hili Taifa? Ina maana Mh. Sugu ni mtu hatari kuwashinda wezi wa Escrow na Makinikia?

Binafsi inafahamika jimbo la Mbeya linawauma CCM si kama wezi wanaolitia hasara Taifa ni ruksa kumwacha mwizi aendelee kudunda mtaani ila si mpinzani anaekosoa Taifa hili kwa nini msimuache Akson Tulia apambane kwa nguvu zake na sugu kuliko kuwaandalia mbeleko kila uchwao?

Ni rahisi mwizi na fisadi kuishi vizuri chini ya serikali ya CCM kuliko mpinzani ambae ataonesha kutoridhishwa na mwenendo mbovu juu ya serikali yake huyo ataitwa mchochezi na kumfungulia mashtaka haraka afungwe lakini si mafisadi.
 
Back
Top Bottom