Uchaguzi 2020 Serikali ya CCM imepoteza "credibility" ya kupambana na watoa rushwa

Mystery

JF-Expert Member
Mar 8, 2012
15,480
30,152
Tulisikia "maigizo" ya Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa, Humphrey Polepole, akieleza kuwa safari hii kwenye uchaguzi wa mwaka huu wa 2020, hawataruhusu hata kidogo watoa rushwa wenye nia ya kutaka kupendekezwa na chama hicho kwa nia ya kuwa wagombea kwa nafasi yoyote katika uchaguzi ujao mwisho wa mwaka huu, wakitoa rushwa kwa nia ya kuwashawishi wapiga kura ili wampigie kura za kuwa mgombea kwenye chama hicho.

Tulimsikia pia Katibu huyo wa uenezi wa CCM akiwasihi wananchi wote wawarekodi kwa kutumia simu zao na baadaye kuupeleka ushahidi huo kwenye chombo kinachopambana na rushwa nchini cha TAKUKURU ili washughulikiwe

Kuna "principle" moja kubwa katika sheria inayosema sheria haina macho na kumwangalia ni nani amefanya kosa hilo ikiwa na maana kuwa sheria ni msumeno unaokata pande zote, kwa maana nyingine ni kuwa kwenye sheria hakuhitajiki hata kidogo "double standards"

Nimekuwa nikijiuliza hivi ni lini chama hicho kimegeuka kuwa ni chama kinachopambana kwa dhati na watoa rushwa??

Bado tunakumbuka tukio lilitokea miaka michache iliyopita, ambapo aliyekuwa Mbunge wa Chadema, wa jimbo la Aru Meru Mashariki, Joshua Nassari, alimpomrekodi, aliyekuwa Mkuu wa wilaya hiyo wa wakati huo, Alexander Mnyeti akitoa rushwa waziwazi kwa madiwani wa Chadema, ili awashawishi wakiache chama chao cha Chadema na wajiunge na CCM

Mikanda hiyo iliyorekodiwa iliwasilishwa moja kwa moja kwa TAKUKURU ili ifanyiwe uchunguzi

Kilichotokea wananchi wote mnakumbuka kuwa kabla hata uchunguzi wa TAKUKURU haujaanza na kuona kama kweli huyo Mkuu wa wilaya alitoa rushwa hiyo, cha kustaajabisha badala yake, Rais Magufuli alimpandisha cheo "mtoa rushwa" huyo na kuwa mkuu wa mkoa wa Manyara!

Cha kushangaza zaidi ni kwa yule aliyetoa ushahidi huo wa mtoa rushwa huyo, aliyekuwa Mbunge wa Chadema wa jimbo hilo la Aru Meru Mashariki, Joshua Nassari, alivuliwa ubunge wake na Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai, kwa madai kuwa ni mtoro ambaye hajahudhuria vikao vitatu mfululizo vya Bunge!

Ndipo hapo ninaona chama hicho cha CCM hakina nia ya dhati ya kupambana na watoa rushwa hao na badala yake, ni kama kinafanya mchezo wa kuigiza kwa kuwatazama usoni watoa rushwa hao, na kuona kama ni watoa rushwa waliowekwa kwenye "black list" na chama hicho ili washughulikiwe au kama ni wale ambao ni vipenzi vya "Bwana mkubwa" ambao kamwe hawatakiwi kuguswa na mkono wa sheria

Kwa maana hiyo tusitegemee kamwe kama TAKUKURU itakuwa na ubavu wa kuwashughulikia watoa rushwa wa aina hiyo!
 
Huo ndio ukweli , uwazi na uwajibikaji ambazo ndio nguzo kuuza ya CCM na Serikali yake lakini Kuna chama zimefujwa bilioni nane na chenji yake Cha kushangaza mpaka Mwenyekiti wa tawi wa chama hicho anajitahidi kuficha
 
KARLO MWILAPWA
Hizo ni propaganda tu za watu wa Lumumba..........

Vipo vyombo vinavyoshughulikia kesi za aina hiyo, ambazo ni mahakama...........

Hivi mnashindwa nini nyinyi watu wa CCM kumburuza mahakamani huyo "mbaya wenu" ambaye mnadai kuwa kafuja hizo bilioni 8, ikiwa mnadai mna ushahidi wa kutosha kuwa huyo Mbowe, ametafuna pesa ya Chadema ya kiasi hicho??
 
Kwanza Dada umeolewa? Naona unaandika vitu kama mtu mwenye stress. Kwanza tambua hatua walizochukua Ccm kudhibiti mianya rushwa kwenye kura za maoni zinatakiwa kusifiwa. Sababu wameonyesha namna gani wanataka wagombea waadilifu.
Pili una uhakika video alizopeleka Nasari pale Pccb ni authentic? Au unalalamika kwa mhemuko wa kisiasa tu.
Tatu hujui kuwa Nassari alifukuzwa kwa utoro bungeni? Jambo ambalo lipo kwa mujibu wa katiba.
Huku kuleta tuhuma za kubahatisha hakuwezi kuisaidia Chadema.
Mmeshafeli
 
Takukuru wanashughulikia hili suala. Majibu yakitoka. Utajua mbivu na mbichi.
 
Hivi umechanganyikiwa? Unapochanganya tukio la mwaka 2017 na tamko la mwaka 2020 na kutoa conclusion huo si uhayawani? Au umekosa cha kuandika unaunga unga matukio. Nilitegemea utoe mfano wa tukio la jana si la wakati wa Nassari
 
Ukishapendwa na bwana mkubwa, upo huru kufanya chochote utakacho. Unashangaa rushwa tu wakati kuna hadi wanaopiga watu risasi?
 
Kwanza Dada umeolewa? Naona unaandika vitu kama mtu mwenye stress. Kwanza tambua hatua walizochukua Ccm kudhibiti mianya rushwa kwenye kura za maoni zinatakiwa kusifiwa. Sababu wameonyesha namna gani wanataka wagombea waadilifu.
Pili una uhakika video alizopeleka Nasari pale Pccb ni authentic? Au unalalamika kwa mhemuko wa kisiasa tu.
Tatu hujui kuwa Nassari alifukuzwa kwa utoro bungeni? Jambo ambalo lipo kwa mujibu wa katiba.
Huku kuleta tuhuma za kubahatisha hakuwezi kuisaidia Chadema.
Mmeshafeli.
Idugunde
Hebu nikuulize swali dogo tu wewe kada wa Lumumba, kama kweli Spika Ndugai angekuwa anatenda haki, ni kwanini hajamvua ubunge wake, Mheshimiwa Nimrod Mkono, ambaye hajaonekana kwenye vikao vya Bunge zaidi ya vitatu??
 
Idugunde
Hebu nikuulize wewe kada wa Lumumba, kama kweli Spika Ndugai angekuwa anatenda haki, ni kwanini hajamvua ubunge wake, Mheshimiwa Nimrod Mkono, ambaye hajaonekana kwenye vikao vya Bunge zaidi ya vitatu??
Nani kada? Taarifa kuwa Mh Nimrod Mkono anaumwa ofisi ya Bunge inazo. Kwani we hujui?
 
Back
Top Bottom