Serikali ya CCM iliahidi kutengeneza njia nne mlima wa Mbalizi Mbeya hadi leo kimya, Dr. Tulia sasa wewe ndio mbunge wa Mbeya, unasubiri vifo vingapi?

Hakuna kitu kinakera kama ahadi za uwongo wa wanasiasa. Na mbaya zaidi ni pale ambapo wanaahidi uongo kwa vitu ambavyo vinagharimu maisha ya watu. Kwa nini wanasiasa wanapenda kusema uongo?

Tuchukulie huu mteremko wa Mbalizi unapotoka Mbeya mjini kwenda Songwe airport, Mbozi Tunduma na hata Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afrika Kusini, Congo nk. Ni barabara muhimu sana hii, na sehemu hii imeua watu wengi kutia ndani viongozi wa serikali na kuharibu mali za mabilioni ya fedha.

Kila inapotokea ajali, viongozi wanakuja na maneno matatu sana ya ahadi kurekebisha sehemu hii, ambayo ni fupi sana, kama kilomita moja na nusu tu. Miaka nenda miaka rudi hakuna kilichofanyika.

Mnataka nani afe hapo ili mchukue hatua, Waziri Mkuu? Au mnataka Watanzania wangapi wafe kabla ya kuchukua hatua?

Hii barabara si kwa ajili ya watu wa Mbeya tu, na kumbukeni kunapotokea ajali hata wasafiri wanaokwenda airport Songwe wanaathirika. Kama serikali ya CCM iliweza kutoa ahadi za papo kwa hapo kujenga barabara za lami zisizo kwenye mipango ya serikali wakati wa kampeni, mnashindwaje kutenga fungu ili kuweka njia nne katika hii sehemu ya barabara kuu Tanzania?

Kwako wewe Tulia kama Mbunge wa Mbeya. Umuhimu wa kuweka njia nne katika hii barabara ya Mbeya, kuanzia Uyole hadi sehemu ya Airport Songwe, haupaswi kuwa jambo ambalo unatakiwa uambiwe. Msongamano wa magari na ajali zinazotokea maeneo ya Mwanjelwa ni jambo lililowazi hata kwa mtu asiye na PhD, sasa kwa nini kwako liwe gumu kuliona?

Wiki hii imetokea ajali nyingine tena ambapo loli la shaba limegonga magari matano hivi. Vifo ambavyo vingeweza kutokea hapa inatisha kuwazia.

Natoa wito kwa wakazi wa Mbeya kwamba mnapaswa kuja juu kudai haki yenu ya kuendelea kuishi ili sehemu hii ijengwe njia nne. Daini kwamba tozo za miamala za mwezi ujao lazima zipelekwe hapa Mbalizi kujenga njia nne kwa sababu kuna hatari za vifo, papewe kipao mbele kwenye kutumia fedha za tozo.

Na kwa nini watu wa Mbeya mnaridhika na msongamano uliopo Mwanjelwa wakati uwezo wa kudai hii barabara ipanuliwe sehemu hii kuwa njia nne toka Uyole hadi Songwe airport serikali inao ila inawapuuza? Nyie ndio mnalisha karibu asilimia 50% ya Tanzania lakini serikali inakosa kuonyesha shukurani kwenu kwa kitu kidogo kama kurekebisha hii sehemu ya Songwe ili watu wasiendelee kufa. Mnakubali mabilioni yakajenge international airport Chato na kufanyiwa matamasha ya ngoma. Si mliambiwa mkimtosa Sugu mambo yenu yatanyooshwa? Wake up!

View attachment 1931739

Kenge huwa hasikii mpka damu zitike masikioni
 
Watu wa Mbeya hodari kwenye uchawi tu, lakini hapa ilikuwa piga ua hakieleweki hadi parekebishwe! Kila siku wanaahidiwa tu, lakini wanafurahia kuna tu viongozi wao wanakata viuno kucheza ngoma. Hakuna sehemu inanikera nikienda Mbeya kama hii sehemu wanaita Mwanjelwa. Msongamano wa watu, magari, machinga, baiskeli, daladala lakini wao wanajionea sawa tu. Sijui kama huyo Mbunge wao Tulia anatumia helikopta akiwa Mbeya haoni hizi kero?

Kama kuna watu wanahitaji kukumbushwa wajibu wao kwa kupopolewa na mawe tena, basi na liwe! Mbeya hampaswi kuchezewa kama watoto wadogo, asee

ubunge wa tulia mbeya ni wa magumashi yye mwenyewe analijua hilo ni nguvu ya jiwe iliyompa ubunge,
 
Hili eneo inabidi kuongeza njia , mbali na hilo ni kufanya diversion ili gari ndogo na malori yapite njia tofauti, Mana Mara nyingi malori yanafeli breki yanaenda kusimamia ifisi,
 
Hakuna kitu kinakera kama ahadi za uwongo wa wanasiasa. Na mbaya zaidi ni pale ambapo wanaahidi uongo kwa vitu ambavyo vinagharimu maisha ya watu. Kwa nini wanasiasa wanapenda kusema uongo?

Tuchukulie huu mteremko wa Mbalizi unapotoka Mbeya mjini kwenda Songwe airport, Mbozi Tunduma na hata Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afrika Kusini, Congo nk. Ni barabara muhimu sana hii, na sehemu hii imeua watu wengi kutia ndani viongozi wa serikali na kuharibu mali za mabilioni ya fedha.

Kila inapotokea ajali, viongozi wanakuja na maneno matatu sana ya ahadi kurekebisha sehemu hii, ambayo ni fupi sana, kama kilomita moja na nusu tu. Miaka nenda miaka rudi hakuna kilichofanyika.

Mnataka nani afe hapo ili mchukue hatua, Waziri Mkuu? Au mnataka Watanzania wangapi wafe kabla ya kuchukua hatua?

Hii barabara si kwa ajili ya watu wa Mbeya tu, na kumbukeni kunapotokea ajali hata wasafiri wanaokwenda airport Songwe wanaathirika. Kama serikali ya CCM iliweza kutoa ahadi za papo kwa hapo kujenga barabara za lami zisizo kwenye mipango ya serikali wakati wa kampeni, mnashindwaje kutenga fungu ili kuweka njia nne katika hii sehemu ya barabara kuu Tanzania?

Kwako wewe Tulia kama Mbunge wa Mbeya. Umuhimu wa kuweka njia nne katika hii barabara ya Mbeya, kuanzia Uyole hadi sehemu ya Airport Songwe, haupaswi kuwa jambo ambalo unatakiwa uambiwe. Msongamano wa magari na ajali zinazotokea maeneo ya Mwanjelwa ni jambo lililowazi hata kwa mtu asiye na PhD, sasa kwa nini kwako liwe gumu kuliona?

Wiki hii imetokea ajali nyingine tena ambapo loli la shaba limegonga magari matano hivi. Vifo ambavyo vingeweza kutokea hapa inatisha kuwazia.

Natoa wito kwa wakazi wa Mbeya kwamba mnapaswa kuja juu kudai haki yenu ya kuendelea kuishi ili sehemu hii ijengwe njia nne. Daini kwamba tozo za miamala za mwezi ujao lazima zipelekwe hapa Mbalizi kujenga njia nne kwa sababu kuna hatari za vifo, papewe kipao mbele kwenye kutumia fedha za tozo.

Na kwa nini watu wa Mbeya mnaridhika na msongamano uliopo Mwanjelwa wakati uwezo wa kudai hii barabara ipanuliwe sehemu hii kuwa njia nne toka Uyole hadi Songwe airport serikali inao ila inawapuuza? Nyie ndio mnalisha karibu asilimia 50% ya Tanzania lakini serikali inakosa kuonyesha shukurani kwenu kwa kitu kidogo kama kurekebisha hii sehemu ya Songwe ili watu wasiendelee kufa. Mnakubali mabilioni yakajenge international airport Chato na kufanyiwa matamasha ya ngoma. Si mliambiwa mkimtosa Sugu mambo yenu yatanyooshwa? Wake up!

View attachment 1931739
Mbioni kuanza👇

Screenshot_20220408-205429.png

Screenshot_20220408-205554.png
 
Subiri 2025 Sugu akichukua Jimbo lake.
Figisu za Chalamila kutomtaja Sugu kwamba ndio mshindi halali ndio zimesababisha yote haya.
 
Moja kioindi kigumu chadema wanapitia Ni Cha sas HV mnk hela wanataka ruzuku wanataka ila hawataki wabunge kuwafukuza kina mdee inataka ujasiri na ikiwa mbowe na kina lissu atawatetea bas jueni kuwa huku mtaani hamtaeleweka na chama hcho huwenda ikapasuka vipand vinne
Skm gang
Msoga gang
Lissu gang
Mbowe gaga
 
Back
Top Bottom